Lissu, Bulaya wamliza Wassira

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza, imetupilia mbali maombi mawili yaliyopelekwa kortini kupinga matokeo ya Ubunge wa Jimbo la Bunda mjini katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana,anaandika Moses Mseti.

Maombi hayo yalipelekwa na wapiga kura wanne, Magambo Masato na wenzake watatu dhidi ya Ester Bulaya (Chadema).

Katika kesi hiyo namba moja ya mwaka 2015, maombi hayo yalipelekwa na wapiga kura hao, kumtetea aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo, Steven Wassira kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kwenye uchaguzi huo Wassira aliangukia pua.

Uamzi huo umetolewa jana na Jaji Lameck Mlacha, baada ya kupitia hoja zilizotolewa na Bulaya kupitia wakili wake, Tindu Lissu kupinga kupokelewa kwa maombi ya wapiga kura hao.

Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki, aliweka mapingamizi matatu ambayo ni kukosewa vifungu vya sheria vya kupeleka maombi kortini na kifungu cha 10, A na B ambavyo havijatolewa maelezo ya kutosha.

Pingamizi lingine ni kifungu cha 11 kinachotaja vitendo vya rushwa vilivyofanywa na mfuasi wa Bulaya katika maelezo ya wapeleka maombi hao lakini hawajavionesha licha ya kumtaja mfuasi huyo.

Katika maelezo ya Lissu kortini hapo, alidai kuwa katika hoja ya kwanza ya kukosewa vifungu vya sheria kwamba, vimekosewa na haviipi mahakama nafasi ya kutenda haki na mteja wake kutafuta ushahidi.

Pingamizi la pili Lissu, alidai limekiuka sheria na hakuna maelezo ya kutosha huku hoja ya tatu ikipigwa chini kwa maana sheria haimtambui mfuasi bali anayetambuliwa ni mgombea (Bulaya) ama wakala wake ambao wangetajwa ubunge ungeweza kutenguliwa.

Jaji Mlacha akitolea uwamzi mapingamizi hayo alidai kuwa, kufuati kupitia hoja za pande zote mbili zilizotolewa Agosti 17 mwaka huu, anakubaliana na Lissu kwa kufuta hoja ya kwanza na tatu.

Jaji Mlacha amesema kuwa, pingamizi la pili lililokuwa limewekwa na Bulaya kupitia wakili wake Lissu, anakubaliana naye katika baadhi ya vipengele ambavyo ni pamoja na wapeleka maombi kushindwa kutoa maelezo ya kutosha huku akitoa nafasi ya kuendelea kusikilizwa kwa kesi hiyo.

“Paragraph (Aya) ya 11 ilitakiwa kusema vitendo vya rushwa ambavyo vimefanywa na mfuasi wa Bulaya (Emmanuel Nteleja) na mgombea (Bulaya) akiwa anafahamu vitendo hivyo licha ya hivyo, aya hiyo ina mapungufu.

“Pamoja na hayo tayari uwamzi katika pingamizi la kwanza lililokuwa likibishaniwa tayari Jaji Gwae (Mohamed Gwae) alishalitolea uwamzi na nanuku maelezo yake;

“Mwombaji lazima aoneshe ameleta maombi kwa kifungu gani na sheria gani ili kuirahisishia Mahakama katika kutoa maamzi,” alinukuu Jaji Mlacha.

Jaji Mlacha amesema kuwa, kuna baadhi ya vifungu ambavyo vinaipa mahakama nafasi ya kuendelea kuisikiliza kesi hiyo, huku akidai kwamba, kesi hiyo itapangiwa siku na Jaji mwingine wa kuisikiliza.

Wakati maamzi hayo yakitolewa kortini hapo, upande wa mjibu maombi namba moja uliwakilishwa na Wakili Onyango Otieno huku mlalamikaji ukiongozwa na Wakili Constantine Mtalemwa.
 
Huyu Wassira itakuwa Mtukufu kaamua kumkaziaaa, pamoja na kuandaa ilani ya chama lakini wapiii, labda ilani imekuwa ngumu kutekelezeka ndio maana mtukufu nae kaamua kutia kisuuuu
Umri wote ule anataka nini hasa bungenii??
 
Wassira anahangaika bure,Magu hawapi wadhifa wowote WAZEE
Anapaswa kuelewa enzi zake wakati wa Mkapa na JK zimekwisha
 
Kesi inaendelea ikiwa imebaki na vifungu/aya dhaifu. Mmenikumbusha kesi ya Mpendazoe ( ng'ombe asiye na mkia) dhidi ya Mahanga ( mtu nisiyemkubali kabisa); kesi yao vifungu muhimu vilifutwa kwa kukiuka sheria na kesi ikaendelea na vifungu/aya dhaifu zilizobaki.
 
Back
Top Bottom