Lissu asimama kizimbani kwa masaa 3:30

Hivi ni kwa nini Watanzania wanapenda sana ku-rely kila kitu kwa Mungu? Mungu yuko bias kiasi hicho? Basi na wale waliomshinda Lema nao walimwachia Mungu? Au Lema mwenyewe hakumwachia kesi yake Mungu?

Ni kutokana shetani anavyotenda kazi kupitia watawala wetu. Viongozi wanagharimia uovu kwa gharama yoyote na ndiyo Mungu hataibariki Tz ikiwa Watawala wetu wataendelea kumtumikia Shetani. Pili Mungu ni baba yetu tunapoonewa ni lazima tumwambie labda kama wewe siyo zizi hili ndiyo utalalamika kama hivi.
 
Nakutakia ushindi wa kishindo Lissu usiwe na shaka utashindaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!
 
Hivi hii ni cancer gani? Na imeingia lini kwenye mahakama zetu...? Na kinachonisikitisha ni jinsi kuliko na watu makini sana ktk idara hii lakini wanaamua kuweka pamba masikioni..hukumu ya lema imeidhalilisha sana idara hii...
 
Hivi ni kwa nini Watanzania wanapenda sana ku-rely kila kitu kwa Mungu? Mungu yuko bias kiasi hicho? Basi na wale waliomshinda Lema nao walimwachia Mungu? Au Lema mwenyewe hakumwachia kesi yake Mungu?

We ulitaka wakuachie wewe?
 
Niliaminishwa kuwa mahakama ni chombo huru kisichoingiliwa na mtu yeyote. Sasa hivi naamini vinginevyo.
Mahakimu wanaongozwa kwa remote na serikali ya ccm.
 
Pesa nyingi sana zinatumika wakati wa kampeni na kwenye kesi kama hizi wakati kuna watoto wanakaa chini, mashule na barabara hazipitiki, kuna wananchi sasa hivi wamekwama barabara mbovu , hizo pesa zakurudia kufanya kampeni Singida zingekwenda kufanya maendeleo . Nadhani hiyo kesi ya Mhe, Lissu wangeitupilia mbali
 
kama lema eti kashindwa ile kesi!anything can happen,.how long shall they kill our prophets!
 
Ni kutokana shetani anavyotenda kazi kupitia watawala wetu. Viongozi wanagharimia uovu kwa gharama yoyote na ndiyo Mungu hataibariki Tz ikiwa Watawala wetu wataendelea kumtumikia Shetani. Pili Mungu ni baba yetu tunapoonewa ni lazima tumwambie labda kama wewe siyo zizi hili ndiyo utalalamika kama hivi.


Hakuna hela yoyote inayotoka kwa viongozi. Ni hela zetu wananchi ndio zinachezewa kuendesha kesi kama hizi.

Ndio shukrani za CCM kwa wananchi!
 
Mungu atawalaani hawa ccm hawa wewe ngoja tu,na nna hasira nao sana yani mpaka nashindwa kuelezea,na mtakufa viongozi wote wa CcM mnaopindisha haki ndani ya nchi hii
 
Lissu apangua hoja za CCM kwa masaa 3 na nusu (3:30) : kauli ya mwisho anayosema ni kuwa katika tuhuma zote zilizoletwa mahakamani, hakuna ushahidi hata mmoja wa mawakala wa CCM, au wapiga kura wa CCM waliolalamika kuwa kulikuwa na vitendo vya uvunjaji wa sheria.

Hakuna hata wakala mmoja wa CCM aliyejaza fomu namba 14 ya kutoridhika na upigaji kura. Sheria za uchaguzi zinasema wakala ajaze fomu kuonyesha kuwa ameridhika au hajaridhika na kulalamikia tuhuma iliyoletwa mahakamani.


Jambo la pili Hakuna wakala hata moja aliyejaza fomu namba 16 ambaye hakuridhika na zoezi la kuhesabu kura na kutangaza matokeo

Tatu: Hakuna ushahidi wowote wa nyaraka, kuonyesha kuwa CCM au mgombea wao wa Ubunge, au diwani, au wakala wao aliyelalamika kwenye kamati ya maadili ya uchaguzi ya Jimbo la Singida mashariki, au kwa jambo lolote lile.

Na hakuna ushahidi wowote uliotolewa wa malalamiko yeyote. Ushahidi uliotolewa wa Bw. Robert Kimanda, anadai kuwa aliwahi kusema kuwa alijaza. Lakini shahidi aliyefuata alisema kuwa baada yakugundua kuwa CCM wameshinda katika kituo alichosimamia, aliichana fomu hiyo. Kuna malalamiko mengi lakini mengi yanatokana na umbumbumbu wa kutojua sheria za uchaguzi.

Kutokuwepo kwa malalamiko kunaonyesha kuwa hakukuwepo tatizo, kesi imetengenezwa baadaye na watu walioshindwa kwenye uchaguzi. Mheshimiwa jaji, Mashahidi walipingana, wengine walisema walioleta mashataka ni waongo.

Kama mashahidi wa upande wa walalamikaji wanaitana waongo mheshimiwa jaji, kuna nini chakuongeza? Shahidi namba 16, alisema waleta maombi ni waongo.
asante mkuu isango nimeipenda hiyo na nadhani kuna umuhimu kweli wa kukata rufaa na kutumia vifungu vya sheria kama hivi ili kumkomboa mwanaharakati mwenzetu lema kwani kama mawakala hawakujaza fomu sote za kuonyeshwa kuto ridhishwa mara nyingi kesi za magamba ni za kupikwa na wanajua mahakimu wao wanapakua na wao magamba watakula kwa ubua
 
CCM jiangalieni sana, kila Mtanzania anawalaani hakika hamtadumu, na ninyi mliosoma kwa kodi zetu na sasa kulipwa kwa pesa za wavuja jasho, mwisho wenu utakuwa mbaya kwa kutumiwa na CCM kupindisha haki huku mkijua wazi hamkutenda haki. Majaji na polisi ole wenu kwa kwa kujifanya ninyi wajinga katika hili.

Tundu kamanada wetu njia ipo nyeupe utashinda mafisi hawa wataaibika
 
Kila hila ina mwisho wake, mwisho halisi wa hila hizi ni hasira ya walipa kodi. Tunalipa ili tupate huduma bora za msingi za kijamii, tuliowapa madaraka wanazitumia kujikita madarakani na kuendeleza dhuluma. Wakati hauko mbali ama tutagoma kulipa kodi au tutawang'oa kwa nguvu ya umma. We are no longer fools, we know what are our rights.
 
Back
Top Bottom