Lissu asimama kizimbani kwa masaa 3:30

Isango

R I P
Jul 23, 2008
295
450
Lissu apangua hoja za CCM kwa masaa 3 na nusu (3:30) : kauli ya mwisho anayosema ni kuwa katika tuhuma zote zilizoletwa mahakamani, hakuna ushahidi hata mmoja wa mawakala wa CCM, au wapiga kura wa CCM waliolalamika kuwa kulikuwa na vitendo vya uvunjaji wa sheria.

Hakuna hata wakala mmoja wa CCM aliyejaza fomu namba 14 ya kutoridhika na upigaji kura. Sheria za uchaguzi zinasema wakala ajaze fomu kuonyesha kuwa ameridhika au hajaridhika na kulalamikia tuhuma iliyoletwa mahakamani.


Jambo la pili Hakuna wakala hata moja aliyejaza fomu namba 16 ambaye hakuridhika na zoezi la kuhesabu kura na kutangaza matokeo

Tatu: Hakuna ushahidi wowote wa nyaraka, kuonyesha kuwa CCM au mgombea wao wa Ubunge, au diwani, au wakala wao aliyelalamika kwenye kamati ya maadili ya uchaguzi ya Jimbo la Singida mashariki, au kwa jambo lolote lile.

Na hakuna ushahidi wowote uliotolewa wa malalamiko yeyote. Ushahidi uliotolewa wa Bw. Robert Kimanda, anadai kuwa aliwahi kusema kuwa alijaza. Lakini shahidi aliyefuata alisema kuwa baada yakugundua kuwa CCM wameshinda katika kituo alichosimamia, aliichana fomu hiyo. Kuna malalamiko mengi lakini mengi yanatokana na umbumbumbu wa kutojua sheria za uchaguzi.

Kutokuwepo kwa malalamiko kunaonyesha kuwa hakukuwepo tatizo, kesi imetengenezwa baadaye na watu walioshindwa kwenye uchaguzi. Mheshimiwa jaji, Mashahidi walipingana, wengine walisema walioleta mashataka ni waongo.

Kama mashahidi wa upande wa walalamikaji wanaitana waongo mheshimiwa jaji, kuna nini chakuongeza? Shahidi namba 16, alisema waleta maombi ni waongo.
 
Ni kwanini ccm wanafikiria kuwavua wabunge wote makini wa cdm ubunge?Huu ni ushahidi kuwa wanaiogopa sana nguvu ya umma.Kulazimisha kuwa Lisu ana kesi ya kujibu ni ulimbukeni na uzuzu wa ccm.Ni wakati mahakama zetu zitende haki kwa maslahi ya wananchi
 
Isango!!

Usiwe kimya Kamanda wetu,,,,,,,,,,,,,,,,,tupe Updates ya hapo mahakamani


Ni nini kinaendelea mpaka majira haya Kamanda?????????????????
 
Mdogo wangu lissu, wewe umeshamaliza sehemu yako! Kwa sasa mwachie mungu akuteteee,biblia inasema haki huinua taifa,bali dhambi ni aibu ya watu wowote(mith;14:34) haijalishi ni jaji,rais,hakimu au waziri mkuu.
 
Big up Lissu nakukubali sana Kamanda jinsi unavyojipanga na kutoa mashambulizi yenye kugonya bongo na n.y.e.ti za magambaz.
 
Isango..... ikipata muda tupe kwa kirefu mzee tujuze camanda Lisu alivyopangua hoja za magamba
 
wanajua hawatashnda ila wameamua kumpotezea muda wake ili asi report mjengoni kpndi hki.
 
Najisikia kufa kufa ninaposikia hii kesi isiyo na kichwa wala miguu. Iko siku tutaingia msituni wenyewe bila kuambiwa na mtu. Magamba subirini siku yenu inakuja
 
CCM jiangalieni sana, kila Mtanzania anawalaani hakika hamtadumu, na ninyi mliosoma kwa kodi zetu na sasa kulipwa kwa pesa za wavuja jasho, mwisho wenu utakuwa mbaya kwa kutumiwa na CCM kupindisha haki huku mkijua wazi hamkutenda haki. Majaji na polisi ole wenu kwa kwa kujifanya ninyi wajinga katika hili.
 
Back
Top Bottom