Lissu anamaanisha nini kuhusu "udikteta"

kabamanya

Senior Member
Jun 20, 2013
163
44
Udikteta ni dhana pana sana na pengine haina tafsiri ya moja kwa moja, nadhani maana halisi ya udikteta ni hisia.

Tukisema udikteta kwa maana ya sheria je sheria hiyo imejitosheleza kujumuisha matakwa ya kila mtu na hisia za kila mtu?

Je, sheria yenyewe haiwezi kuwa athari kwa hisia za wengine?

Lakini kama sheria ndio kipimo, je mapinduzi ya kiutawala yanawekwa upande gani? Mfano yaani mmehamua kuandamana, pasina kufuta sheria kupinga utawala dhalimu labda, je nyie mtakuwa madikteta?

Jambo la pili udikteta unanzia wapi na kuishia wapi? Ni yapi matendo ya udikteta na matendo yasiyo ya udikteta, Je ipo orodha ya mambo hayo?

Nafikiri ipo haja ya kufikiria zaidi juu ya dhana hii, "udikteta"
 
Mkuu uje huyu bwana anatumiwa kuwaimbisha wasiojua hii nyimbo,na Watz wachache wenye reasoning capacity ndogo wameingia kichwakichwa pasi nakujua,embu atueleze tumwelewe anataka kutuambia nini,wenzetu democrasia walianza kupractice baada ya mapinduzi ya kilimo na viwanda,coz hata wanazuoni wakubwa walioandika kuhusu democracy ya aina yetu wanasema inakua acampaned na uchumi imara,taasisi imara na mifumo tengefu sasa sisi badala yakufanya kazi tukuze uchumi mnataka kuandmana ucku na mchana,HAIKUBALIKI na kama shida ya Lissu na wenzake ni maandamano wazipeleke familia zao na sio kuwapeleka vijana wa masikin ili wakafe wapate mtaji wa kisiasa SAY NO TO UKUTA
 
Nonsense, woga wa kike!
 
Kwa nini wafe vijana
 
Mzee vijana awapelekwi kwenye maandamano bali vijana wote tumechoka kupelekwapelekwa na maccm kwa hiyo sept 1 tutatoka wenyewe majumbani kwetu kwenda kufanya maandamano ya amani ya kupinga udikteta uchwara
 
Alimaanisha hivi!
image.jpg
 
Watumishi wa Bwana wanatekeleza Amri ila wanajitia KUSAHAU SERIKALI IPO.Na Nchi haiwezi kuwa na watu wawili wanatoa Amri.AMIRI JESHI MKUU ALIYEAPA Ndiyo mwenye Mamlaka.Hao wengine wanatuletea fujo za kutimiza Ulaji wao.
 
Udikteta ni dhana pana sana na pengine haina tafsiri ya moja kwa moja, nadhani maana halisi ya udikteta ni hisia. tukisema udikteta kwa maana ya sheria je sheria hiyo imejitosheleza kujumuisha matakwa ya kila mtu na hisia za kila mtu? Je sheria yenyewe haiwezi kuwa athari kwa hisia za wengine? Lakini kama sheria ndio kipimo je mapinduzi ya kiutawala yanawekwa upande gani? mfano yaani mmehamua kuandamana, pasina kufuta sheria kupinga utawala dhalimu labda, je nyie mtakuwa madikteta?

Jambo la pili udikteta unanzia wapi na kuishia wapi? ni yapi matendo ya udikteta na matendo yasiyo ya udikteta, Je ipo orodha ya mambo hayo?

Nafikiri ipo haja ya kufikiria zaidi juu ya dhana hii, "Udikteta"

Dictator definition, a person exercising absolute power, especially a ruler who has absolute, unrestricted control in a government without hereditary succession.
 
Kwa uelewa wangu, Udikteta ni aina ya utawala wenye tabia zifuatazo:
· Maamuzi na uendeshaji wa mambo ambao hayatokani na utashi wa wananchi kwa mujibu wa katiba na sheria bali hutokana na matakwa ya mtu mmoja.

· Kugandamiza uhuru wa watu kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari, vyama vya siasa vya upinzani na asasi za kiraia ili kuzima mawazo yanayojaribu kukosoa utawala.
· Watawala hupenda kusifiwa, hulazimisha wananchi wawatii na hawapendi kukosolewa na kujifunza.

· Kuingilia uhuru wa mihimili mingine ya dola (bunge na mahakama) kwa watawala kupandikiza vibaraka katika mihimili hiyo au kwa kuingilia mihimili hiyo kwa mabavu.
· Matumizi ya ulaghai wa kutatua matatizo ya nchi au wananchi katika kugandamiza uhuru wa wananchi na kujiimarisha katika utawala.

· Matumizi makubwa ya vyombo vya dola kupeleleza wale wasiokubaliana na utawala, kuwakamata, kuwaweka mahabusu, kuwatesa na wakati mwingine kuwaua ili kuwatia hofu wananchi na kuzima upinzani. Udikteta huwa ni utawala wa mabavu.

· Watawala kutokuheshimu mifumo iliyopo na mipango ya wasaidizi wao bali utendaji huwa ni wa zimamoto au kukurupuka kutokana na wasaidizi kuwa na hofu ya watawala.

· Pamoja na kwamba udikteta huleta utulivu kwa muda, hujenga chuki miongoni mwa wananchi, moyo wa kulipiza kisasi na hatimaye kuleta maafa makubwa ya maasi na umwagaji damu.

· Kuzuia au kuvuruga chaguzi ili wapate kura nyingi na kuonekana wanaungwa mkono na wananchi wengi na kujihalalishia kuendelea kutawala.

· Kwa kuwa na hurka ya matumizi ya mabavu na kukosa mbinu za kidiplomasia, udikteta humomonyoa ushirikiano wa kimataifa na wakati mwingine kusababisha kutengwa na jumuia ya kimataifa pasipokuwa na sababu za kimsingi.

· Kwa ujumla udikteta ni mfumo mwovu kwani watawala wanaokuwa na matendo ya kidikteta huwa hawakubali kuitwa madikteta. Ni kama ambavyo mwizi hakubali kuitwa mwizi ma ambavyo mchawi hakubali kuitwa mchawi.
 
Hakuna aliye juu ya Sheria Ukiforce utatia aibu tu,hiki ndicho kinachotokea ktk serkali hii ya awamu ya 5 kitendo cha raisi kujitahid sn kuwa juu ya sheria kwa makusudi kwa maamuzi binafsi huku akiweka kando sheria zilizo ndani ya katiba na badala yake kutumia amri zake kitu ambacho wafuatiliaji na wasimamiaji wa sheria kwa kutambua na kuheshimu taaluma zao za sheria wawapo kazini(mahakamani) wanapoamua kuzisimamia sheria kwa mujibu wa kiapo walichokula wakiapa kulitumikia Taifa na watz wte kwa ujumla pacpo kujali itikadi za Vyama vyao,dini zao wala mihemko na hisia wala Chuki zao bnafsi,tumekuwa tukiona sheria zikiiwajibisha na kuiumbua serikali na kutueleza kuwa matamko binafsi,hisia,Chuki na maamuzi binafsi haviwezi kuongoza wala kuiendesha nchi Bali ni sheria peke yake,hii inazidi kutufundsha kuwa Cheo hakimfanyi mtu kuwa juu ya sheria ku
 
Kwa uelewa wangu, Udikteta ni aina ya utawala wenye tabia zifuatazo:
· Maamuzi na uendeshaji wa mambo ambao hayatokani na utashi wa wananchi kwa mujibu wa katiba na sheria bali hutokana na matakwa ya mtu mmoja.

· Kugandamiza uhuru wa watu kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari, vyama vya siasa vya upinzani na asasi za kiraia ili kuzima mawazo yanayojaribu kukosoa utawala.
· Watawala hupenda kusifiwa, hulazimisha wananchi wawatii na hawapendi kukosolewa na kujifunza.

· Kuingilia uhuru wa mihimili mingine ya dola (bunge na mahakama) kwa watawala kupandikiza vibaraka katika mihimili hiyo au kwa kuingilia mihimili hiyo kwa mabavu.
· Matumizi ya ulaghai wa kutatua matatizo ya nchi au wananchi katika kugandamiza uhuru wa wananchi na kujiimarisha katika utawala.

· Matumizi makubwa ya vyombo vya dola kupeleleza wale wasiokubaliana na utawala, kuwakamata, kuwaweka mahabusu, kuwatesa na wakati mwingine kuwaua ili kuwatia hofu wananchi na kuzima upinzani. Udikteta huwa ni utawala wa mabavu.

· Watawala kutokuheshimu mifumo iliyopo na mipango ya wasaidizi wao bali utendaji huwa ni wa zimamoto au kukurupuka kutokana na wasaidizi kuwa na hofu ya watawala.

· Pamoja na kwamba udikteta huleta utulivu kwa muda, hujenga chuki miongoni mwa wananchi, moyo wa kulipiza kisasi na hatimaye kuleta maafa makubwa ya maasi na umwagaji damu.

· Kuzuia au kuvuruga chaguzi ili wapate kura nyingi na kuonekana wanaungwa mkono na wananchi wengi na kujihalalishia kuendelea kutawala.

· Kwa kuwa na hurka ya matumizi ya mabavu na kukosa mbinu za kidiplomasia, udikteta humomonyoa ushirikiano wa kimataifa na wakati mwingine kusababisha kutengwa na jumuia ya kimataifa pasipokuwa na sababu za kimsingi.

· Kwa ujumla udikteta ni mfumo mwovu kwani watawala wanaokuwa na matendo ya kidikteta huwa hawakubali kuitwa madikteta. Ni kama ambavyo mwizi hakubali kuitwa mwizi ma ambavyo mchawi hakubali kuitwa mchawi.

MADIKTETA NA UZALENDO BANDIA
Mara nyingi madikteta hujinasibu kuwa na mapenzi makubwa kwa mataifa wanayoyaongoza. Hata hivyo, ukichunguza kwa undani utagundua kuwa mapenzi wanayokuwa nayo huwa ni yamejaa ubinafsi kwa kupenda kuridhisha nafsi zao pasipo kujali umuhimu wa watu wengine. Wao ndio hujigeuza kuwa taifa na kwao usalama wao ndio huwa usalama wa taifa na si usalama wa raia. Kwao uzalendo ni wananchi konyesha mapendo kwao, kuwashangilia na kuwatii. Wanaamini katika uwezo wao wa kutenda na si katika uwezo wa wananchi. Wanashindwa kuelewa kuwa taifa hujengwa na wananchi na hivyo mzalendo wa kweli hutanguliza mapenzi ya wananchi kuliko nafsi yake, huwaamini wananchi kuwa ndio wanajenga nchi, huamini kuwa taifa ni la wananchi na si la mtawala au kundi la watawala. Mzalendo wa kweli hufanya jitihada kuleta furaha kwa wengine kuliko kufurahisha nafsi yake. Madikteta ni mafisadi wa kimaadili (they are morally corrupt) na hawana sifa ya kuitwa wazalendo kwa kuwa uchu wao wa madaraka huleta mateso kwa wengine.
 
Back
Top Bottom