Hata mie sijui,ndio nini hiyo red??
Kumbe ni hatari kukimbilia kauli za wanasheria! Lissu aliitisha kikao na waandishi wa habari huku kukiwa na sakata la wabunge kutuhumiwa kula rushwa huko TANESCO. Akawataja wabunge kadhaa tukadhani ametaja waliokula rushwa lakini leo anasema hakusema kuwa Mwijage (Aliyetajwa) amekula rushwa. Anasema alichokisema ni kuwa Mwijage ana mgongano wa masilahi kwa kuwa ni mshauri wa Puma! Patamu hapo.
'TL: Unajua nilichokisema?
Mwijage: Kwani ulisema nini?'
Sasa mh Mwijage kama hujui alichokisema umeshitaki nini?
Pole. Maana wewe na Mwijage wala hamna tofauti. Wote hamjui Tundu Lissu alisema nini hasa. Mtaendelea kuingizwa kingi. Suala la msingi ambalo ungeweza kuhoji hapa, ni kwa nini kwenye habari za tv hayakusikika hayo maneno ambayo yaliandikwa kwenye 'headlines' za baadhi ya magazeti kesho yake!
Nikupatie kitu kidogo tu hivi; siku hiyo ya habari hizo zikiwa zimepamba vyombo vya habari, nilikuwa najadiliana na mwanahabari mwenzangu mmoja hivi. Nikamwuliza mbona umeandika maneno mengine tofauti na yale aliyosema Lissu, akajibu "sasa unafikiri wananchi wataelewa nini ukiandika mgongano wa maslahi, hilo wasomaji hawajui, unawaandikia kile wanachojua." Nilitamani kulia.
Kila la heri Mwijage na hawa akina Kimbunga.
Bwana mdogo kama huna pointi ya kuandika waachie wenye akili wakuandikie.Inaonekana wewe ni Gamba na kada harufu wa Chama cha mabwepande na nadhani wewe ni wassira na msura wako wakifisadi ule Lisu ni mpiganaji wa uhakika na tunategemea awe Tz prezoo wa 2020 baada ya slaa!Gamba we!
Habari za mujini zinaanza kufika Bungeni.. saafiiii.....Nimekutana na Mwijage akaniambia amenishtaki na mimi nimemuuliza ‘unajua nilichokisema?' na yeye akaniuliza kwani ulisema nini? Nimemweleza kuwa mimi nawajibika kwa maneno yangu kuwa yeye ana mgomgano wa kimasilahi kwa kuwa consultant (mshauri) wa kampuni ya Puma. Siwezi kumwita mtu mla rushwa kwa kuwa sina ushahidi na hilo," alisema