Ochu
JF-Expert Member
- May 13, 2008
- 975
- 47
Lipumba aishangaa IMF
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amelishangaa Shirika la Fedha Duniani (IMF), kummwagia sifa, Rais Jakaya Kikwete, kwa jinsi anavyoshughulikia suala la wizi wa fedha katika Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA).
Lipumba ameonyesha hali hiyo, ikiwa ni siku moja tu imepita, baada ya Mkurugenzi wa IFM, Dominique Strauss-Khan, kutoka Washington, Marekani, kummiminia sifa Rais Kikwete kwa jinsi uongozi wake ulivyosimamia urejeshwaji wa fedha za EPA, zilizoibwa kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana, mwenyekiti huyo, alisema kitendo cha Rais Kikwete kutotumia ipasavyo madaraka yake kukabiliana na wezi na wahujumu uchumi wa nchi, hakipaswi kupongezwa kwani ni ukiukwaji wa utawala wa sheria.
Profesa Lipumba ambaye ni mtaalamu wa mambo ya uchumi, alisema kashfa ya EPA, haijawahi kutokea katika benki yoyote duniani.
Tukio kama hilo halijawahi kutokea katika benki yoyote ile duniani, lakini IFM wanapongeza hatua za rais za kutowachukulia hatua wezi hao, hili kwa kweli linanishangaza, alisema Lipumba.
Akikaririwa na vyombo vya habari juzi, Mkurugenzi wa IMF, alisema tukio kama la wizi uliofanyika BoT, linaweza kutokea popote duniani, jambo ambalo Profesa Lipumba alipingana nalo.
Mapema mwezi uliopita, CUF iliandaa mkutano na waandishi wa habari ambapo Lipumba aliwalaumu wahisani wakubwa wa Tanzania kama Benki ya Dunia (WB) na IMF, kwamba wamekuwa nyuma kuisaidia serikali katika vita dhidi ya ufisadi na badala yake wamekuwa wakiisifia kwa kila jambo, hali inayochochea kuongezeka kwa vitendo vya ufisadi.
Akilihutubia Bunge mjini Dodoma Agosti 21 mwaka huu, Rais Kikwete alisema serikali imekamata mali za wamiliki wa kampuni 13 kati ya 22, waliothibitika kuhusika na uchotaji wa sh bilioni 133 kwenye Akaunti ya EPA, ambapo kiasi cha sh bilioni 53.7 zimekusanywa, huku hati zao za kusafiria zikishikiliwa.
Rais Kikwete alisema watuhumiwa hao wameongezewa siku 72 kuanzia Agosti 21 ili wawe wamerejesha sh bilioni 74, baada ya muda huo kupita watachukuliwa hatua za kisheria.
Kutokana na hatua hiyo, viongozi wa kambi ya upinzani na makundi kadhaa ya wanaharakati, walipinga, na kuitafsiri kuwa ni sawa na kutangaza msamaha kwa wezi hao.
source: Tanzania Daima