Lipumba: Nchi isipotawalika kuwapo demokrasia ni muhali;kauli za Chadema kuidhalilisha Serikali

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Wednesday, 16 March 2011 00:11

prof%20lipumbanew.jpg
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba

TAMKO lililotolewa hivi karibuni na Chadema kuwa hakiwezi kushirikiana na vyama vingine vya upinzani bungeni kwa sababu, vimeungana na CUF ambayo ‘imefunga ndoa’ na CCM na kuunda serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, lilikuwa mwiba mchungu wa CUF.

Katibu Mkuu Chadema, Dk Willibrod Slaa, anasema Kamati Kuu ya Chadema, imeona chama hicho hakiwezi kuwa na ushirikiano wenye tija na vyama hivyo bungeni, na kumwagiza kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, kuunda baraza kivuli la mawaziri la wabunge wa Chadema pekee.

Dk Slaa alikaririwa akisema Kamati Kuu imezingatia kuwa, CUF na CCM wamejiunga kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar na kwa kuwa, sheria inayoruhusu uwepo wa vyama vya siasa inahusu pande zote za Muungano, inaamini CCM na CUF ni wamoja hata Bara.
Tamko hilo liliibua mvutano mkubwa wa kisiasa kati ya CUF na Chadema na kuwafanya viongozi mbalimbali wa CUF kuitupia lawama Chadema kwa madai kuwa haikutenda haki ya kidemokrasia.

Hivi karibuni, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba wakati anazungumza kuhusu masuala ya Uchumi, siasa na Usalama anasema Chadema inaendesha siasa zinazoweza kuibua vurugu nchini.
“Kitendo cha Chadema kuibeza serikali ya umoja wa kitaifa ya Zanzibar ni kuwadharau Wazanzibari na kuwatakia shari, Zanzibar ni sehemu moja kati ya mbili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chuki za Chadema haziutakii mema muungano wetu,” anasema Profesa Lipumba.

Profesa Lipumba ambaye tangu mwaka 1995 mpaka sasa amekuwa akiwania urais kwa tiketi ya chama hicho anasema kitendo cha Chadema kuifananisha CUF na CCM ‘B’ kwa sababu ya kushiriki katika serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar ni dharau kwa Wazanzibari.

Anasema kabla ya kura ya maoni ya Wazanzibari, Kituo cha Demokrasia Nchini (TCD), chini ya uwenyekiti wa Chadema kiliandaa tamasha visiwani Zanzibar kuwahamashisha Wazanzibari kupiga kura ya ndiyo ili kuwepo na mabadiliko ya katiba yatakayoleta Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

“Serikali ya Umoja wa Kitaifa inatokana na kura ya Wazanzibari iliyoungwa mkono na Chadema. Katiba ya Zanzibar inaelekeza kuwa chama chochote cha siasa kitakachopata asilimia 5 au zaidi ya kura zote kitakuwa na haki na wajibu wa kushiriki katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa,” anasema Profesa Lipumba.

Anasema Chadema ilishiriki katika uchaguzi wa Zanzibar ikielewa wazi katiba ya Zanzibar.
“Kama ingepata alau asilimia 5 za kura, wawakilishi wao wangeshiriki katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa, sasa wanapobeza serikali hii ni kuwadharau Wazanzibari na kuwatakia shari,” anasisitiza Profesa Lipumba.

Anasema serikali hiyo imeleta amani katika siasa za Zanzibar na kwamba kauli za Chadema kuidhalilisha Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar haiitakii amani Zanzibar inalenga kuuvuruga Muungano.
“Watanzania wote wanaopenda amani wanastahiki kulaani kauli za Chadema,” anasema.

Anasema katika mfumo wa vyama vingi na nchi yenye serikali katika ngazi mbalimbali ni jambo la kawaida kwa chama kushirikiana katika ngazi moja wakati vyama hivyo hivyo vinapingana katika ngazi nyingine.

“CUF ilipokuwa na wabunge wengi ilishirikiana na Chadema, Chadema imekataa kushirikiana na CUF na vyama vingine vya upinzani. Hii inaonyesha kuwa Chadema haina lengo la kujenga umoja wa Watanzania,” anasema Profesa Lipumba.

Anasema kauli za viongozi wa Chadema katika mikutano ya hadhara mkoani Mwanza ambapo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alionya kama Rais Kikwete hatachukua hatua kuinusuru taifa yaliyotokea nchini Misri, Libya na Tunisia yanaweza kutokea Tanzania, ni kauli ambazo zinaweza kuchochea vurugu za kisiasa.

“Pamoja na mapungufu ya katiba na Tume huru ya uchaguzi, uhuru wa kisiasa uliopo Tanzania ni mkubwa kuliko hali ilivyokuwa Tunisia, Misri na Libya,” anasema Lipumba.
Anasema kufanya maandamano kwa malengo ya kuifanya nchi isitawalike hakusaidii kujenga misingi ya demokrasia.

Anasema wanaotaka kuingia madarakani kwa kuiangusha serikali kupitia maandamano hawana nia ya kuwakomboa Watanzania na kujenga msingi imara ya demokrasia.

“Hawa wanahitaji kuwatumia wananchi kuingia madarakani na wakishapata madaraka hawatakuwa na lengo la kujenga demokrasia ya kweli na hawatakubali kung’olewa kwa kura,” anasema Lipumba.Anasema wanasiasa wenye malengo halisi ya kujenga demokrasia wanastahiki kujikita katika kudai Katiba mpya na Tume Huru ya Uchaguzi.

Anasema Rais Kikwete amekubali kuanzisha mchakato wa kupata katiba mpya hivyo ni wakati wa vyama vya siasa kutoa mapendekezo ya mambo ya kuzingatiwa katika mswada wa sheria utakaopelekwa bungeni kwa lengo la kuanzisha mchakato wa kupata katiba mpya ikijumuisha kuundwa kwa tume ya kuongoza mchakato huo.

“Ni wakati wa kuandaa na kupeleka serikalini hadidu rejea za Tume itakayosimamia mchakato wa kupata katiba mpya,” anasema Lipumba.

Anaongeza,” Ni wajibu wa viongozi makini kumuunga mkono Rais Kikwete katika jambo hili jema na kushiriki kikamilifu kuhakikisha tunapata katiba mpya. Hatuwezi kupata katiba yenye misingi ya demokrasia ikiwa Chadema watafanikiwa kuifanya nchi isitawalike”.

Anasema kuandaa vyema uchaguzi mkuu 2015 kunahitaji kuwepo kwa Tume huru yenye mfumo unaofika kwenye majimbo ya uchaguzi.Anasema serikali inapoonekana kuyumba, wanaotaka nchi isitawalike watapata fursa ya kufanikisha malengo yao.Mvutano wa vyama vya upinzani ni mzito, ni ndoto kwa vyama hivi kuweza kushirikiana kama Watanzania wengi wanavyoota kila kukicha.

Nchini Kenya vyama vingi vilipoanzishwa havikufua dafu kwa chama tawala (KANU).
Baada ya chaguzi mbili za vyama vingi, vyama vya upinzani vikaamua kuungana kwa mujibu wa sheria ya nchi yao na hatimaye wakapata rais mpya aliyetokea upinzani, ndiyo ukawa mwisho wa chama tawala.

Pamoja na hayo, kukazuka mgogoro wa chama hiki kudai kuwa kimepewa mawaziri wachache, kile kikidai kunyimwa wizara nyeti, hiki kikidai makubaliano yamekiukwa mpaka wakagombana.

Walisambaratika na kumlazimisha rais aliyetokana na upinzani kuanzisha ushirikiano mpya na rais aliyeondoka madarakani na hivyo kufifisha vita dhidi ya ufisadi na kusababisha serikali iliyokuwa madarakani ionekane ya ufisadi sawa na ile serikali iliyokuwa imepita. Je, Huo ndiyo ushirikiano wa vyama vya upinzani unaotafutwa na Watanzania?
 
Nakubaliana na Prof. Lipumba hususan juu ya msimamo wa Chadema dhidi ya vyama vya upinzani kwa maoni yangu msimamo wao sio sahihi. Ikiwa vyama vyengine vya upinzani vimepata majimbo baadhi ya maeneo ina maana vinakubalika kwenye maeneo hayo au wagombea waliowasimamisha wanaaminika si vizuri kuwabeza. Pia mtizamo wao dhidi ya Serikali wa Umoja wa kitaifa Zanzibar sio wa busara wao walitakaje? watu waendelee na uhasama? wangetuambia labda njia gani bora wanayofikiria ingetatua mgogoro wa Zanzibar vyenginevyo hatutowaelewa
 
source: msikitini
 
source: msikitini

Are u serious?
Sasa naanza kuamini kweli udini upo, yaani akiongea mtu wa CUF wewe unaconclude msikiti umehusika.
Sikubaliani na Lipumba kwa kuwa najua anatimiza wajibu wa kumpamba bosi wake Maalim Seif Sharif Ahmad kwakuwa najua anajua moyoni ni ulafi wa madaraka wa Seif ndo umemuweka pale maana anajua kuwa Maaalim alitakiwa awe Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na pale cHAMA cHA mAFISADI KILIPOIFIOSADI NAFASI YAKE ILIBIDI AKUBALI KUCHUKUWA NAFASI YA uMAKAMU AMBAYO LEO WANAITETEA ATI NI KWA SABABU YA UMOJA WA KITAIFA NA KUEPUSHA SHARI,

Prof Lipumba inatakiwa akiri ya kuwa Seif pamoja na CUF nzima wamewadhulumu wana Zanzibar walioipigia kura CUF itawale Zanzibar.

Haiwezekani na sipendi nijifanye nakubaliana eti Lipumba anaweza kumzidi kura Maalim Seif Zanzibar.
 
hivi cuf mwenye uwezo wa kugombea urais ni mmoja tu?mtu keshashindwa kwenye chaguzi nne lakini bado mnamng'ang'ania,au kwa vile anaitwa profesa??kapoteza mvuto ndo maana anaionea wivu CDM,na wanasiasa mfilisi wote wanaishia kuishi kwa hisani ya ccm kama cheyo na mrema,uchaguzi uliopita cuf waliisapoti ccm na kuishambulia cdm,..wapinzani gani hao???kupingana na cdm ni sawa na kupingana na umma,na umma always unashinda..
 
Lipumba hana influence hata kidogo so aongee vyovyote ni upepo tu.

Lipumba akajaribu kugombea ubunge kwao tuone kama atapita.
 
chadema wangepata 5% yakura zanzibar wangekuwepo kwenye serikali ya umoja wakitaifa. na wao wanajua hilo na walipigia kampeni kwenye kongamano waliloliongoza wao kule zenji, ila kwasababu hawakupata ndo haya tunayoyaona. read btn the line myie watu.
chadema ni popo. wanaonekana ndege kumbe sio.
 
mkuu wewe ndo unanishawishi niitupe kadi ya ccm na kuchukua ya cdm! SASA KATI YA CDM NA CUF NANI POPO!!???
 
Back
Top Bottom