Lipumba na Mbatia wahutubia wana CCM Kigoma

Ni vyema tukajaribu kutafuta na kuujua ukweli. Cuf na NCCR ni wazi wanasubiria serikali ya umoja wa kitaifa.

Ni imani yao kwamba serikali ya umoja wa kitaifa ni jambo la lazima na ni suala la muda. Wao hawaamini kwamba inawezekana CCM kuondoka madarakani ila ni rahisi kuungana nao.

Nasikitika sana. Inatia huzuni kwamba hawa ndio watu ambao watanzania wanatakiwa kuwategemea na kuwaona ni wakombozi.

Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki CHADEMA.
mkuu.
Hilo liko wazi. Kwa muundo wa utawala tulio nao..CCM kuwa chama dola ni wazi kuwa hawako tayari kuachia madaraka. Sio siri kuwa CCM wameshindwa kila uchaguzi kule Zanzibar..lakini uchama dola wa CCM, tume za uchaguzi,vyombo vya usalama, jeshi vinahakikisha CCM inarudi madarakani.
Kwa hiyo, kama CHADEMA wanataka kuingia madarakani kwa amani ,bila ya kumwaga damu basi Serikali ya kitaifa ipo njiani kwa bara pia...Mimi napenda niite Serikali ya kitaifa Tanganyika.
Kuna thread ya waberoya ilionya CHADEMA wasibeze hii dhana ya serikali ya kitaifa huenda wakaihitaji.
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...lahi-ya-taifa-they-are-just-another-tool.html
 
Ni vyema tukajaribu kutafuta na kuujua ukweli. Cuf na NCCR ni wazi wanasubiria serikali ya umoja wa kitaifa.

Ni imani yao kwamba serikali ya umoja wa kitaifa ni jambo la lazima na ni suala la muda. Wao hawaamini kwamba inawezekana CCM kuondoka madarakani ila ni rahisi kuungana nao.

Nasikitika sana. Inatia huzuni kwamba hawa ndio watu ambao watanzania wanatakiwa kuwategemea na kuwaona ni wakombozi.

Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki CHADEMA.

Mkuu naona unawauliza NCCR na CUF: je mnataka Serikali ya umoja wa Kitaifa!? kabla ujajibiwa naona unajijibu mwenyewe na Thread ya majibu inaendelea, nimeona Mkutano wao wa Kigoma walichosema wanatakiwa waunganishe nguvu waing'oe CCM madarakani, kuhusu Serikali ya mseto wameiongelea ya Zanzibar, kuhusu Serikali ya mseto Tanzania Bara umeamua kuwalisha hayo maneno
 
mie nilibahatika kuhudhuria,watu walikuwepo wengi tu ila sio ka nyomi la cdm,
usiseme waliohudhuria walikuwa watoto,
mwana shika adabu yako,
Basi nisamehe mkuu.....nilikuwa usingizini.... lakini sasa nimeshaamka na akili iko sawa
 
Msando,

Kwa nini unasema kwamba CUF na NCCR ni ''wazi wanasubiria serikali ya umoja wa kitaifa''?

Well, in any case serikali ya ''umoja wa kitaifa'' kwa nchi zetu za Africa imeprove failure. Kiukweli ni kwamba kiongozi/chama kilichoshindwa au kinachoelekea kushindwa kimekuwa kikivihadaa vyama pinzani ili waungane na kuunda serikali ila kimsingi lengo lao ni kuendelea kubaki madarakani na baada ya kushika dola, life goes on as usual.

Mifano ipo hai - Zimbabwe (mvutano wa Mugabe na Tsvangirai), Kenya (vurugu kati ya Odinga na Kibaki) na najua hata Zanzibar Seif Shariff yupo yupo tu na hana say pale.
Mkuu.
Kwa hiyo hakuna mfumo unaofaa Afrika? Mfumo gani gani wa serikali unaofaa kwa nchi za kiafrika?

Demokrasia imekuwa failure Afrika? Au hatujawahi kuwa na demokrasia bali tuna domokrasia tu?

Mfumo upi wa serikali unaotufaa Afrika? je kuna nchi ambayo unaona mfumo wao wa serikali unafanya kazi vizuri katika bara laAfrika ili tuige huko?
Au wewe unapendekeza mfumo upi tuufuate?
 
Ama kweli siasa za Tanzania! Lipumba na Mbatia wanazungukia maeneo ambayo Operation Sangara haijapita -- wakiwaponda Chadema! sasa wako Kigoma!

La kushangaza ni kwamba habari za wawili hao zimebahatika kupata ukurasa wa mbele leo katika gazeti la CCM la Uhuru tu (according to mapition ya magazeti ya Channel 10).

Wawili hawa wanafanyakazi ngumu ya kujibu CDM kwa niaba chama hicho tawala -- kwani wao CCM hawawezi. Sababu moja kubwa CCM hawawezi ni kwamba wenyewe kwa wenyewe wanapingana kuhusu kuijibu Chadema!!

Profesa na Mbatia wamekubali kufanya kazi hiyo chafu na ya kujidhalilisha!!! kwa niaba ya CCM. Profesa anasahau Mbatia huyo alifanya usaliti mkubwa dhidi ya CUF hjuko Pemba wakati wa marudio ya uchaguzi 2004 pale alipoweeka pingamizi kwa wagombea wake na hivyo viti vyote kuchukuliwa na CCM! ANASAHAU KABISA!

Nakiri Profesa alikuwa kipenzi changu sana kisiasa hasa baada ya matukio ya mauaji Pemba ya 2001 walipoonewa na pia wafuasi wake kuuwawa na polisi wa CCM! Lakini anasahau yote hayo!

Kwani akikaa kimya angalau angejitunzia heshima yake iliyobakia kuliko kufanya anachokifanya sasa. Na kama ana ubavu wa kuikabili CDM aende akawapiku kule kanda ya ziwa sangara ilikopita. CCM wenyewe wanaogopa kwenda kule kujibu mapigo.

Lakini pengine kwa uchu wa pesa na jinsi walivyokwishapoteza utu wao inawezekana wakaenda kule kufanya kazi ya Bwana Mkubwa!!
 
Mtumbwi ni chombo muhimu huko Zenji ila ni gogo la kuachwa shambani litafunwe na mchwa huku Tabora so issues za CUF na NCCR mara zote ni gogo kwa waelewa (tabora) .................simply dont bother about mtumbwi in tabora
 
Ama kweli siasa za Tanzania! Lipumba na Mbatia wanazungukia maeneo ambayo Operation Sangara haijapita -- wakiwaponda Chadema! sasa wako Kigoma!

La kushangaza ni kwamba habari za wawili hao zimebahatika kupata ukurasa wa mbele leo katika gazeti la CCM la Uhuru tu (according to mapition ya magazeti ya Channel 10).

Wawili hawa wanafanyakazi ngumu ya kujibu CDM kwa niaba chama hicho tawala -- kwani wao CCM hawawezi. Sababu moja kubwa CCM hawawezi ni kwamba wenyewe kwa wenyewe wanapingana kuhusu kuijibu Chadema!!

Profesa na Mbatia wamekubali kufanya kazi hiyo chafu na ya kujidhalilisha!!! kwa niaba ya CCM. Profesa anasahau Mbatia huyo alifanya usaliti mkubwa dhidi ya CUF hjuko Pemba wakati wa marudio ya uchaguzi 2004 pale alipoweeka pingamizi kwa wagombea wake na hivyo viti vyote kuchukuliwa na CCM! ANASAHAU KABISA!

Nakiri Profesa alikuwa kipenzi changu sana kisiasa hasa baada ya matukio ya mauaji Pemba ya 2001 walipoonewa na pia wafuasi wake kuuwawa na polisi wa CCM! Lakini anasahau yote hayo!

Kwani akikaa kimya angalau angejitunzia heshima yake iliyobakia kuliko kufanya anachokifanya sasa. Na kama ana ubavu wa kuikabili CDM aende akawapiku kule kanda ya ziwa sangara ilikopita. CCM wenyewe wanaogopa kwenda kule kujibu mapigo.

Lakini pengine kwa uchu wa pesa na jinsi walivyokwishapoteza utu wao inawezekana wakaenda kule kufanya kazi ya Bwana Mkubwa!!

Kulikuwapo moves za CUF kujitenga yaani kuwepo CUF-Bara baada ya kuingia serikali ya CCM+CUF huko Zenj -- yani kumeguka kwa chama hicho.. Hizo moves zimefikia wapi? Wana-CUF huku Bara wanaona muunganoi huo huko Zenj utachelewesha sana ukombozi wa watu wa Bara kutoka udhalimu wa mamlaka za CCM --achilia mbali CUF kupoteza umaarufu (kitu ambacho tayari kinatokea kutokana na matokeo ya uchaguzi mwaka jana).

Nadhani polepole watu wanaanza kubaini kuwa serikali ya pamoja ya CCM+CUF huko Zenj ni mradi kabambe wa CCM kuendelea kubakia madarakani daima dumu.
 
Hizi ni siasa uhuru liko kwa ccm kama mwanahalis kwa chadema wala sio issue ni siasa
 
Ni vyema tukajaribu kutafuta na kuujua ukweli. Cuf na NCCR ni wazi wanasubiria serikali ya umoja wa kitaifa.

Ni imani yao kwamba serikali ya umoja wa kitaifa ni jambo la lazima na ni suala la muda. Wao hawaamini kwamba inawezekana CCM kuondoka madarakani ila ni rahisi kuungana nao.

Nasikitika sana. Inatia huzuni kwamba hawa ndio watu ambao watanzania wanatakiwa kuwategemea na kuwaona ni wakombozi.

Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki CHADEMA.

mkuu watanzania tunachojua ni kwamba hatutakaa tuwe na serikali ya umoja wa kitaifa. Uku bara ni Ccm au cdm na 2015 ndo ivo ivo,aidha cdm ichukue au ccm igang'anie kama 2010. Watasubiri sana. Naona nccr na Cuf wamechagua resistance by collaboration,which can hardly mean opposition. Ila mi nawapongeza maana option iliyokuwa imebaki kwao ni either kuacha siasa au kuungana na adui ccm. Wamewaacha wanaume cdm na cdm wanyukane wao wakijificha chini ya meza kumsubiri mshindi. Wasubiri waone picha halisi,cdm ndo wapinzani pekee wa kuitetea nchi.
 
consultant,

Nimemsikia Prof Lipumba akihutubia Kigoma. Anasema serikali ya kitaifa Zanzibar iheshimiwe na imeleta amani na manufaa kwa wazanzibari. James Mbatia akasupport na kusema hayo hayo.

Kimsingi wanasema inawezekana kufanya kazi na CCM naitakuwa kwa manufaa ya wananchi. Wanataka kufanya
kazi kwa ushirikiano ili kuleta maendeleo.

Wao CCM sio wabaya wana mapungufu tu ya kibinadamu.
Hivyo kwa kuunganisha nguvu wanaamini maendeleo
yatapatikana.

Hiyo ndio sababu nalazimika kujiuliza hawa ni kwamba
wanasubiri kuundiwa serikali ya umoja wa kitaifa lengo ikiwa
na wao wawe watawala!
Msonda, hivi ni Chama kipi cha Siasa ambacho Viongozi wake hawana Lengo la kuwa Watawala? Mi naona tofauti iko Kwenye Strategies tu za kufikia Lengo. Serkali ya Mseto ni Hatua kubwa kwa Chama cha Upinzani kuelekea kushika Madaraka kamili, mfano Mzuri ni pale Nyerere alipopigania TANU ikubali kura ya Mseto ingawa wenzake Wote walikataa, Strategy yake ilikuwa ni kuwa wanaTANU waingie kwenye Legislative Council, japo utaratibu wa Kura 3 haukua wa Haki, Kisha wapate Legal Recognition na Mandate ya kuendesha Harakati zao za kudai Uhuru, walifanikiwa bila Kumwaga damu! Zanzibar kuwa na Serkali ya Mseto, sio Seif kuwa Makamu tu, Bali kuna Wizara kadhaa pia wanaziongoza, they are Halfway Through kushika Madaraka kamili, walijaribu Kuandamana na Kumwaga damu lakini haikusaidia sana. Mbinu za Kibaba zinazotaka kutumiwa na Chadema ili kuwaondoa watawala zilikwisha jaribiwa na Babu zetu kina Mtemi Mirambo, Chief Mkwawa, kina Kinjeketile na Mbinu ya Majimaji Warfare nk Nyerere alikuja na Mbinu ya Kutumia Dialgue na akafanikiwa kupata Uhuru!
 
Ama kweli chadema ndio chama pekee cha upinzani chenye nguvu kwa sasa. Ukiangalia watu waliohudhuria mkutano huo ni wachache ukilinganisha ya cdm kule kanda ya ziwa, ama kweli cdm wanakubalika licha ya shutma zinaenezwa na ccm na washirika wake. Cha ajabu TBC wameripoti mkutano huo lkn hawakuripoti hata ck moja mikutano ya cdm kanda ya ziwa. Ama kweli hii ni TBCCM, cdm songa mbele

Ndivyo mnavyojifariji hee.

Poleni
 
Nilieleza kuwa Mbatia sio mpinzani tangu mwanzo hamajanielewa huyu anakazi maalumu ya kuuwa vyama
 
Yangu macho Nili mshauri sana Matatiro CUF hakumfai aondoke kabla wananchi hawaja mkatia tamaa hasikii ...................Mtatiro chakula ipo CDM huko uliko njaa itakuua mwachie lipumba kibalaka wa zench aendelee na hilo boya ambalo nusu limesha zama majini

Alaaaaa !!!!!!!!!!!!!!! Sasa umenifumbua masikio, Kumbe kelele zote hizi ni kutafuta chakula tu, wala hamna cha siasa wala nini!!!!!! Hebu nitonye na mimi, hiyo chakula huko CDM bei gani. Kama siasa ni kutafuta chakula ya watoto, basi msiwalaumu hata hawa Lipumba na Mbatia, wanaganga njaa. Ama kweli, siasa za TZ hizi ni kudanganyana tu, siku ukifulia tu unatoswa. Basi, tangu leo mimi na siasa bye bye.
 
kazi kweli kweli nimewaona jana hawa watu nikajiuliza huu si ni muendelezo wa umamluki,na sijui safari hii wameahidiwa kupewa kitu gani masikini,mikutano haina hata mvuto wala wasikilizaji ni wachache sana.....kazi wanayo kutufikia CDM na nguvu yetu ya umma:smash::smash::smash:
 
Masikini Mbatia! Kafuliiiiia! Duh! hana mvuto hata kidogo. Jana nilipomtizama akihutubia anaonyesha sura ya kukata tamaa, lakini basi tena ndo afanyeje. Mtumikie kafiri upate ujira wako.......Kama ujira wenyewe upo lakini!
 
Back
Top Bottom