Lipumba na Mbatia wahutubia wana CCM Kigoma

muhosni

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
1,108
152
Umati wao ulijaa watu waliovalia kijani na njano. Wamewaasa wanachama hao kuepuka vyama vinavyochochea vurugu

source: ITV taarifa
 
Ama kweli chadema ndio chama pekee cha upinzani chenye nguvu kwa sasa. Ukiangalia watu waliohudhuria mkutano huo ni wachache ukilinganisha ya cdm kule kanda ya ziwa, ama kweli cdm wanakubalika licha ya shutma zinaenezwa na ccm na washirika wake. Cha ajabu TBC wameripoti mkutano huo lkn hawakuripoti hata ck moja mikutano ya cdm kanda ya ziwa. Ama kweli hii ni TBCCM, cdm songa mbele
 
Hata mie nimewaona kupitia ITV.......lakini hawana mashiko yoyote.....walikuwa wanawahubiria watoto tu
 
Hata mie nimewaona kupitia ITV.......lakini hawana mashiko yoyote.....walikuwa wanawahubiria watoto tu

mie nilibahatika kuhudhuria,watu walikuwepo wengi tu ila sio ka nyomi la cdm,
usiseme waliohudhuria walikuwa watoto,
mwana shika adabu yako,
 
Ama kweli chadema ndio chama pekee cha upinzani chenye nguvu kwa sasa. Ukiangalia watu waliohudhuria mkutano huo ni wachache ukilinganisha ya cdm kule kanda ya ziwa, ama kweli cdm wanakubalika licha ya shutma zinaenezwa na ccm na washirika wake. Cha ajabu TBC wameripoti mkutano huo lkn hawakuripoti hata ck moja mikutano ya cdm kanda ya ziwa. Ama kweli hii ni TBCCM, cdm songa mbele
TBC kutotoa habari za CDM na kuonyesha mikutano ya vyama vingine ndivyo wanavyofanya watu wapate hamu ya kuhudhuria mikutano ya CDM.
 
Unafiki umewajaa, tamaa ya kupata mafanikio bila ya kuwekeza kwa wananchi ni donda ndugu kwa vyama dada na shangazi kwa ccm!
 
Lipumba na Mbatia tayari ni mufilisi wa kisiasa ambao wameamua kujitambulisha kuwa ni watoto wa CCM-si warudi CCM- nguvu ya umma itawazoa kama ile tsunami ya Japan !!!!!!!!!!!!!!!!
Kujikomba kwa CCM ni kukosa dira ya kisiasa-hapa si suala la kuwa na kutegemea nguvu za wingi wa kura bungeni ili kuidhibiti CDM, bali awareness ya umma iliyo nyuma ya CDM; it is too late for CCM hata wakijaribu kupiga propaganda (uwongo) kujaribu kugeuza waTz mawazo kwamba agenda ya CDM ni kuleta vurugu, bali kwa sisi tunaoumizwa na serikali ya kifisadi ya CCM haina budi kuondolewa na nguvu za umma!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Mbatia alikuwa anaongea kwa konfidensi kama Makamba vile
 
Ni vyema tukajaribu kutafuta na kuujua ukweli. Cuf na NCCR ni wazi wanasubiria serikali ya umoja wa kitaifa.

Ni imani yao kwamba serikali ya umoja wa kitaifa ni jambo la lazima na ni suala la muda. Wao hawaamini kwamba inawezekana CCM kuondoka madarakani ila ni rahisi kuungana nao.

Nasikitika sana. Inatia huzuni kwamba hawa ndio watu ambao watanzania wanatakiwa kuwategemea na kuwaona ni wakombozi.

Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki CHADEMA.
 
Tbc walionesha mkutano wa CDM wa mwanza. Cuf na nccr hawana impact yoyote kwa chadema.
 
Mpango maalum huo, wakaanza na Tido maana yaonekana alikuwa anatoa fursa angalau na kwa CDM.
 
Hawa ni watu wawili waliokosa mwelekeo na walioamua kupoteza muda katika kuwagawa watanzania kwa siasa zao za maji taka. Huu nao ni uhuni!

Wangefanya mambo mengine ya msingi na siyo kuwayumbisha watanzania. They lack Legacy at all!
 
cheap politics are results of cheap politicians.

ukiwaangalia wenyeviti wa hivi vyama ni njaa tupu ndio zinazowasumbua.

Tuwaombee raia wa tz wapate uwezo zaidi wa kuchambua pumba na kichele.
 
mbatia na Lipumba wanajiaibisha kukubali kula pesa za CCM ili kupiga kampeni dhidi ya CHADEMA...sIJUI ni njaa au wivu!!!
 
Msando,

Kwa nini unasema kwamba CUF na NCCR ni ''wazi wanasubiria serikali ya umoja wa kitaifa''?

Well, in any case serikali ya ''umoja wa kitaifa'' kwa nchi zetu za Africa imeprove failure. Kiukweli ni kwamba kiongozi/chama kilichoshindwa au kinachoelekea kushindwa kimekuwa kikivihadaa vyama pinzani ili waungane na kuunda serikali ila kimsingi lengo lao ni kuendelea kubaki madarakani na baada ya kushika dola, life goes on as usual.

Mifano ipo hai - Zimbabwe (mvutano wa Mugabe na Tsvangirai), Kenya (vurugu kati ya Odinga na Kibaki) na najua hata Zanzibar Seif Shariff yupo yupo tu na hana say pale.
 
Yangu macho Nili mshauri sana Matatiro CUF hakumfai aondoke kabla wananchi hawaja mkatia tamaa hasikii ...................Mtatiro chakula ipo CDM huko uliko njaa itakuua mwachie lipumba kibalaka wa zench aendelee na hilo boya ambalo nusu limesha zama majini
 
consultant,

Nimemsikia Prof Lipumba akihutubia Kigoma. Anasema serikali ya kitaifa Zanzibar iheshimiwe na imeleta amani na manufaa kwa wazanzibari. James Mbatia akasupport na kusema hayo hayo.

Kimsingi wanasema inawezekana kufanya kazi na CCM na itakuwa kwa manufaa ya wananchi. Wanataka kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuleta maendeleo.

Wao CCM sio wabaya wana mapungufu tu ya kibinadamu. Hivyo kwa kuunganisha nguvu wanaamini maendeleo yatapatikana.

Hiyo ndio sababu nalazimika kujiuliza hawa ni kwamba wanasubiri kuundiwa serikali ya umoja wa kitaifa lengo ikiwa na wao wawe watawala!
 
Back
Top Bottom