Lipumba: Mimi bado ni Mwenyekiti wa CUF, sitambui kikao cha Zanzibar

Kwa kweli uwa nakuwa na wasiwasi na wasomi wetu,sasa mzee wangu lipumba anahoyafanya yanamshusha hadhi,kwa nini asimwangalie mwenzake dk slaa,kama anataka uenyekiti si angeenda hata a,c,t,kwanini afanye vurugu zote hizi licha ya yeye kutoziona fujo anazofanya,???? Elimu anayo haswa!!!sa ni nini anafanya huyu mzee?? Utu uzima dawa,!!!
 
Mtatiro kuingia ofisin najua anaogopa...na akithubutu kutia miguu pale makao makuu basi ndo siku ya kugawana na mbao
 
Jamani, ngoma sasa inogile. Prof. leo kakomaa hataki kabisa kuambiwa amesimamishwa uanachama.

Hii safi sana maana maalim anaendesha chama kama mali yake.
===========

Akihojiwa na mtangazaji Spencer Lamerk wa ITV usiku huu, Prof. Ibrahim Haruna Lipumba amesema kuwa yeye bado ni Mwenyekiti halali wa CUF.

Prof. Lipumba amesema kuwa kufuatia kutengua barua yake ya kujiuzulu Uenyekiti, aliandika barua kwa Katibu Mkuu wake kutaka kurejea kazini kama Mwenyekiti. Katibu Mkuu alimjibu kuwa anatafuta ushauri wa kisheria.

Kuhusu kikao cha Baraza Kuu la CUF kilichomsimamisha uanachama, Profesa Lipumba amesema kuwa kikao hicho hakikuwa halali kwakuwa hakukuwa na akidi ya Wajumbe wa kutoka Tanzania Bara. Amesema kuwa Katibu Mkuu hamshirikishi Naibu Katibu Mkuu Bara na kuonekana akiendesha chama kiimla.

Prof. Lipumba amesema kuwa Katibu Mkuu asipotaja tarehe ya yeye kurejea kazini kama Mwenyekiti, atasubiri barua ya Msajili wa Vyama ili aanze kazi tena kama Mwenyekiti wa taifa wa CUF.


Kwan lazma yy ndio awe mwenyekiti.
Duuuh Tanzania iko njia panda kila sehem kumechafuka.
 
Hivi hili konokono limetumwa?
Konokono limetengua kujiuzulu kwake. Kwa kujiuzulu kwake nafsi imemsuta.
Prof. Lipumba ni muujiza wa 8 wa dunia.
Ni kama vile prof. ameamka kutoka njozini na kusahau kabisa kwamba alikimbia mapambano na aliitelekeza marikebu ya kivita aliyokuwa anaiongoza mkondoni.

Mungu ampe hekima.
 
Akiongea na Itv (mubashara) jioni hii amedai yeye bado ni mwenyekiti halali wa CUF,na anasubiri go ahead kutoka kwa Msajili wa vyama vya siasa.anasema alimtaarifu katibu kua anarejea ofisini rasmi seif akadai asubiri mpk atakapo pata ushahidi wa kisheria.

kuhusu kusimamishwa uanachama anasema kikao hicho si halali na hakija hudhuriwa na wajumbe wote hivyo yeye na wenzake bado ni wanachama halali wa cuf.

binafsi nimemshangaa na nimeshindwa kumuelewa huyu profesa daah kichwa kinauma...
Kwa hiyo ameshakubaliana na msajili kwamba atamrejeshea uenyekiti alioutema kwa mbwembwe? Kama akili za maprofesa ziko type hii hakuna haja kuwa nao nchi hii
 
Lipumba amefanya kama alivyo fanya seif zanzibar. Seif alijitangazia ushindi na sasa Lipumba kajitangaza yeye ni mwenyekiti.


Hivi umeshiba ngebe ?? Kwani seif alikuwa Mwenyekiti wa chama cha Zanzibar akaandika barua ya kujiuzulu na sasa ametangaza kurudia tena??
 
Kiongozi wa aina hiyo akipewa majukumu makubwa kama kuongoza Nchi uongozi wake kwa alichokifanya ni wa kutiliwa mashaka sana
 
Back
Top Bottom