Luteni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 2,274
- 301
MWENYEKITI wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amewapuuza wanasiasa wanaobeza hatua yake ya kutangaza nia ya kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu ujao, akiwemo Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusufu Makamba.
Akizungumzia kauli iliyotolewa na Bw. Yusufu Makamba dhidi yake kuwa kusimama kwake kugombea kazi itakuwa ni rahisi kwa CCM, Prof. Lipumba alisema kuwa tangu Bw. Makamba achaguliwe kuwa Katibu Mkuu amekuwa akiwasaidia (wapinzani) kukisambaratisha chama tawala.
"Katika kazi ambayo anatusaidia Bw. Makamba ni kukisambaratisha chama chake, karibu viongozi wote wa CCM ukiwauliza Makamba ana kazi gani kwenye chama wanakwambia kabisa kwamba hana lolote, wanashindwa tu kuwa wawazi na kusema ukweli, lakini Makamba hatakiwi CCM.
"Tangu alipochaguliwa kuwa Katibu Mkuu chama kimekuwa katika hali ya mapandemapande, amechangia kwa kiasi kikubwa kukisambaratisha," alisema.
Alisema kuwa Rais Kikwete asipokuwa makini na Bw. Makamba na kuendeleza usanii wake utasambaratisha nchi nzima.
Mwishoni mwa wiki hii, Prof. Lipumba alitangaza nia yake ya kuwania tena urais, lakini baadhi ya watu wakiemo viongozi na wanasiasa walimkejeli kwa uamuzi huo.
Chanzo: Majira