Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,529
Profesa Haruna Ngunguri Lipumba,
Nakuandikia waraka huu wa kiuchungaji ilhali najua marafiki zangu wa CUF watacharuka na kudai naingiia mambo ya ndani.
Leo hii nimewaandikia Chadema, Nimewaandikia CCM na sasa nakuandikia wewe.
Kwa maoni yangu binafsi, nafikiri sasa ni wakti muafaka wa wewe kutafuta mtu mwingine wa kushika hatamu za kuongoza CUF. Kama vile nilivyomtaka Freeman Mbowe aachie manyanga ya Uenyekiti Chadema, naomba nitangulize mkono wangu wa shukrani na kukuomba sasa upumzike, tafuta damu mpya na yenye nguvu yenye uwezo wa kukijenga CUF upya na kwa ushirikiano wa wenzi kutoka Zanzibar.
Sijasema usigombee tena Urais, bali ujivue Uenyekiti wa CUF.
Chama chako kimejitahidi sana kupata viti vya kutosha kwenye TAMISEMI, lakini nafikiri ni wazi ili kuata majimbo mengi ya Ubunge hasa Tanzani aBara, kunahitajika sauti mpya ambayo itafnya kazi ya kuchuana na Msekwa na Makamba na hata pendekezo lango kuwa Sr. Slaa na Lwakatare wawe dynamic duo ya Chadema.
Je umeshawahi kukaa chini na kutafakari ni nani ndani ya Chama chako ambaye unamjenga na kumuandaa awe Mwenyekiti na kukiongoza chama?
Ukirudi kuangalia matokeo ya Ubunge, utabaini kuwa unahitaji mtu mwenye nguvu kubwa huku Bara, swa na Maalim kule Unguja ili kuweza kuongeza uwakilishi wa CUF katika kila mkoa. Njua Chama chako kimegombea Tonge na Chadema na wote mnataka kumpokonya CCM, lakini kwa mwendo huu wa kukosa nguvu nzuri kuongoza Chama kiutendaji kila siku, ni wazi 2015 matokeo yatakuwa yale yale, pamoja na matunda mazuri ya Muafaka kule Zanzibar.
Labda nikuulize, je CUF kuna CUF Zanibar na CUF Tanzania bara? Je Muafaka ni wa upande mmoja tuu wa Muungano?
Je kama Msomi n Mchumi aliyebobea, unapimaje matokeo ya Uongozi wako?
Mwaka 2015, tunahitaji ushndani mzuri, CUF imefanya vyema kujikita katika TAMISEMI na niliona juhudi zenu 2009 na hata mwaka huu. Lakini nafikiri Chama kinahitaji nguvu moya na sura mpya kukiongoza. Mara nyingine mabadiliko husaidia kuleta mwamko mpya na ndio maana kwako nakuomba utafute mpya na kule Chadema nawaambia wana mtu mwenye uwezo wa kukijenga upya Chama.
Miaka hii mitano inayokuja, inahitaji mtu achacharike kila siku kujenga Chama na kufika kila kona. Najua una majukumu makubwa sana ya kikazi ambayo si ya CUF kwa kutokana na umashuhuri wako kama Mchumi kufahamika duniani.
Basi fanya hima uachie mtu mwingine ashikilie usukani akusaidie kukijenga Chama na ikifika 2015, kazi yako iwe ni kuchukua fomu kugombea Urais.
Ni hayo tuu, kutoka kwa Mchungaji Kishoka.