Elections 2010 Lipumba atangaza kugombea urais 2010

"Naamini kwa uwezo nilionao, ninaweza kutatua matatizo ya nchi hii, na nina hakika ya kupata tuzo ya utawala bora." Profesa Nguyuru Haruna Ibrahim Lipumba

Picha hiyo inatisha...anaonekana kuongezeka uso!

Lipumba, acha siasa za kushindania u-rai! Afadhali kwanza uwe m-Bunge tukusikie huko Bungeni!
 
Naongezea...

Lipumba usiwe na uchu wa fisi wa pesa za Dr. Mohamed "Mo" Ibrahim...eti, "tuzo ya utawala bora."
 
Lipumba anasema ataunda serikali ya umoja wa kitaifa kwa misingi gani? Sikujua kuna mpasuko wa kisiasa Tanzania bara kama ilivyo Zanzibar. Angetuhakikishia kuwa CUF ina uwezo wa kutawala nchi ningefarijika zaidi.
 
Nchi Tanzania imeshapasuka,imegawanywa katika misingi ya DINI,Mbaya zaidi hakuna ana/aliyeweza ku address hii ISSUE kwa uzuri wake na kuweka bayana namna ya kupata ya suluhu kabla halijakuchwa na kuingia kiza kinene.

Obama aliweza ku address issue ya ubaguzi wa rangi akaeleweka pamoja na kwamba alieleza ukweli unaouma kwa baadhi ya watu,lakini walikubali uhalisia na kusonga mbele,na ndio utaona sasa hivi racial melting point in US imekuwa high,ingawa still kuna vijimambo vya hapa na pale but the issue was well addressed.

Akiwa Rais Muislam kama ilivyo sasa hivi,waislam wanapunguza kelele dhidi ya CCM na kuona si tatizo sana. Kinyume chake,wakristo wanapiga kelele na kufanya mikakati kadha wa kadha ili kulinda kile kinachoonekana ni maslahi yao.

Akiwa Rais ni Mkristo,the same applies,kelele zinapungua kabisa,na inakuwa ni zamu ya Waislam kulalamikia serikali na CCM kwamba ina sura ya ubaguzi na kutafuta mikakati ya kutetea kile wanachodai ni haki zao.

Kumekuwa hakuna kuaminiana kabisa kutokana na kutofautiana katika itikadi ya dini,na hii hali inaelekea kubaya,kama hatua madhubuti ambazo zina balance pande zote hazitachukuliwa,basi kuna dark future.

Tupo tayari kutothamini potential figures kwa sababu ya dini zetu,tupo tayari kutetea maovu kwa sababu dini yetu inapata maslahi nayo.
 
Tatizo ni chama chake? we need a liberal party na si chama chenye mwonekano wa kidini kama CUF. Mikutano yao ni kama forum ya walimu na wanafunzi wa madrassa. Na ndiyo sababu ccm inashinda maana watu wanaona ni bora jini ulijualo kuliko usilolijua.

Hakuna kiongozi yeyote wa upinzani anayeweza kukubali kuiunga mkono CUF kwa sababu ya mwonekano wa Udini ilionao.

You are absolutely right. Hakuna shaka kwamba CUF kina mwelekeo wa kuwa chama cha kidini. Hata kampeni zao wanapigia zaidi misikitini.

CUF kinaweza kutoa Rais wa Zanzibar lakini hakiwezi kutoa Rais wa Tanzania. Lipumba agombee ubunge. Hatakaa awe Rais wa Tanzania.
 
Kweli anaweza kushindana na siyo kushinda sisi tunataka mshindi. Hii itakuwa ni mara ya ngapi vile?

hakuna njia ya haki ambayo wananchi wanaweza kuhusishwa kumchagua mgombea wanae mtaka kutoka upinzani kuliko Lipumba kujipigia pande mwenyewe kwamba yeye ndio anafaa?

UDINI! UDINI! UDINI! Chama chake kimejaa udini na hii nchi haina dini, we unazani itakuaje? aendelee kupiga makelele jukwaani na kuikosoa serikali ili siku ziende lakini si yeye wala chama chake cha kuitawala nchi. afu mi nashangaa kama vile hawaoni wajirekebishe..
Hakuna Udini wala ukabila katika Uchaguzi mkuu Sisi tunachotaka kwamba Apatikane Kiongozi atakaye weza Kushindana Na Mzee J.Kikwete. wewe Unafikiri Mtu kama Mzee Mrema,Mtikila, na viongozi wengine ukimtowa Proffesor Lipumba kuna Mtu yoyote anayeweza kusimama na Mzee Kikwete na akamshinda katika Uchaguzi Mkuu? Tutakuwa kila siku Washindikizaji wa CCM, na hiyo CCM kila ukifanyika uchaguzi watakuwa wao ndio Washindi wakuu. Kwa Ushauri wangu mimi vyama vyote vya upinzani vimuunge Mkono Proffesor Lipumba kwanza na jambo la pili vyama vya Upinzani kama vitaungana kuwa kitu kimoja basi vinaweza kushinda katika Uchaguzi Mkuu. Asanteni sana.
 
Jamaa ili linaweza ila shida yangu ni kuwa kwenye mikutano ya siasa ya CUF baraghashea na ijabu ni nyingi sana!!!

baraghashea na ijabu ni nyingi isikuumize kichwa hivyo ni mapambo tu ya hao Waislam. Tunataka Mtu ambaye atakuwa yupo mwenye nguvu kumshinda Mzee J.Kikwete katika Uchaguzi Mkuu ujao,ondosha wasiwasi mkuu Mwanamayu.
 
Ingawa I am not supporting any political arrangement let alone 'party', IMO Prof. Ibrahim Haruna Lipumba is most qualified candidate kutoka ktk batch tuliyonayo. Huo ndio ukweli.
 
Ni kweli Por lipumba ni candidate wa hiyo post. hawezi kupata postive repsonse kutoka vyaa vingine sababu inabidi kuwe na makubaliano fulani ili ilo liwezekane.

Mfano CUF kukubali kusurender kutosimamshia wagombea wagombea kwenye baadhi ya majimbo wasyokuwa na nguvu. Najua CUF wanaweza kusema haya Arusha Moshi tarime mwanza wanawaachia NCCR na Chadema. Hili ni gumu vile vile sababu kuna wana CUF wanataka japo kugombea kwenye majimbo haya.

Tuje Majimbo mfano ya Dar nani yuko tayari kumuacia mwenzake ubungo, kinondoni.

Kifupi CUF wont get the support if they wont give the support. hata kama lipumba anatamani nguvu za ndani ya chama cake zitamshinda.
 
Mi nakubaliana na hili la kumsimamisha mgombea mmoja wa upinzani nafasi ya urais naikiwezekana waachiane hata ubunge,hii italeta ushindani na kuna uwezekano hata wakikosa urais wakaongeza wabunge.Lipumba ni mtu makini na atatuongoza vizuri tukiacha zile njaa zetu za pilau/kanga/fulana/elfu 10.
 
Alisema anakusudia kuwasilisha maombi hayo kwa vile haoni kama kuna mtu katika vyama hivyo mwenye uwezo wa kukabiliana na mgombea wa kiti hicho kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, kulingana na hali ya kisiasa ilivyo nchini.

Ndiyo maana huyu mheshimiwa hafanikiwii. Hana hulka ya kisiasa wala maneno ya kidoplomasia. Utaombaje vyama vingine visi simamishe wagombea na kuunga mkono chama chako kwa kusema kuwa vyama vyao hawana watu wenye uwezo? Ana fikiri kuna chama kita kacho kubali kuambiwa kuwa hamna mgombea mwenye uwezo tokea chama chao?
 
Ndiyo maana huyu mheshimiwa hafanikiwii. Hana hulka ya kisiasa wala maneno ya kidoplomasia. Utaombaje vyama vingine visi simamishe wagombea na kuunga mkono chama chako kwa kusema kuwa vyama vyao hawana watu wenye uwezo? Ana fikiri kuna chama kita kacho kubali kuambiwa kuwa hamna mgombea mwenye uwezo tokea chama chao?


I am not sure if the quote is genuine sana kivile...kwani imeandikwa na nani?
 
Msimamo wa CUF au ilani ya uchaguzi inasema vipi kuhusu Mahakama ya Kadhi na OIC?
Tafadhali ninaomba kueleweshwa.
 
You are absolutely right. Hakuna shaka kwamba CUF kina mwelekeo wa kuwa chama cha kidini. Hata kampeni zao wanapigia zaidi misikitini.

CUF kinaweza kutoa Rais wa Zanzibar lakini hakiwezi kutoa Rais wa Tanzania. Lipumba agombee ubunge. Hatakaa awe Rais wa Tanzania.

CCM wanakampeni kuwa CUF ni chama cha kidini, na CHADEMA cha wachaga, kwa hili wamewashinda wengi. Na wengine wanaingia katika mkumbo ule ule wakiwa katika jahazi la kuiondoa CCM madarakani, wanaanza kuimba propaganda zilezile za CCM na kunyoosheana vidole.

Kwa jinsi hii kuja kuitoa CCM madarakani itakuwa miujiza.
 
You are absolutely right. Hakuna shaka kwamba CUF kina mwelekeo wa kuwa chama cha kidini. Hata kampeni zao wanapigia zaidi misikitini.

CUF kinaweza kutoa Rais wa Zanzibar lakini hakiwezi kutoa Rais wa Tanzania. Lipumba agombee ubunge. Hatakaa awe Rais wa Tanzania.

Ubunge wapi, ilhali Ilungangulu, kijijini kwao hata ujumbe wa nyumba kumi hawezi kupata? atafute chuo afundishe tu. He is good for nothing.
 
mi siwezi kumpigia kura lipumba hata siku moja kwasababu simwamini kama atakuwa na religious tolerance yoyote. anatakiwa kututhibitishia watz hicho kwanza ndo atapata kura. bora aje mtu mwingine haijalishi kama ni mkristo au mwislam...ninachotaka ni kuwa na imani na mtu juu ya hili, na lipumba kwangu mimi amefeli mtihani huu.
 
Back
Top Bottom