Elections 2010 Lipumba atangaza kugombea urais 2010

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,138
Jamani inakera ndio maana naona huu upinzani wizi mtupu na thaman kwako ukiwa ndani ya hicho chama ..naona lipumba kwenye tv ya tbc anawahadaa watu kuna rais alianza kugombea toka 1975 amepata urais 2000 na sasa anaongoza na kuhaidi kuleta serikal ya mseto........
Hivi hakuna wengine kila siku hawa hawa tu jamani...mi nishachoka na sias za tanzania kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
CUF bado haijapitisha mgombea wao, Prof. Lipumba anahaki kugombea, na huenda akashindwa katika kura za ndani au akabadili mawazo baadae. Hata hivyo hakuna kitu cha kumshushia haki ya kugombea. Lipumba ni bora x1,000,000 ya Kikwete.
 
Pumzika kidogo
 
Kwani wewe umekatazwa kugombea?. Mbona kila mwaka tokea Uhuru CCM wanatawala kwani hakuna chama kingine? mbona hawa huwapigii kelele?

Kugombea ni haki ya kila mtanzania kikatiba bila kujali anatoka chama gani, sasa kama wewe umechoka siasa za Tanzania ya nini kuzifuatili?, achana nazo!!
 
Lipumba na Seif hawana jipya!
Kama wengi wa watanzania tulivyo!! Mambo tunayaona yanakwenda mrama hatuchukui hatua yoyote tunaishia kulalamika tu. Bora wanaojiandaa kugombea uongozi wa mwamko wa kimapinduzi, hata kushindwa ni sehemu ya mchakato kuliko sisi tulio pembeni na kazi yetu ni kukatisha tamaa wenzetu, aibu kwetu.
 
CUF bado haijapitisha mgombea wao, Prof. Lipumba anahaki kugombea, na huenda akashindwa katika kura za ndani au akabadili mawazo baadae. Hata hivyo hakuna kitu cha kumshushia haki ya kugombea. Lipumba ni bora x1,000,000 ya Kikwete.
.
Ni kweli Lipumba ni bora kuliko JK, tatizo amekaa mno juani mpaka kapauka kwa kiwango ambacho hauziki.

Upinzani wakikubali kuungana na kumsimamisha Dr. Slaa, Hamad Rashid Mgombea Mwenza, Lipumba apewe u-PM, CCM inang'oka!.
 
Lipumba na Seif hawana jipya!
Sijuwi jipya lipi unakusudia maana karibuni CUF imeweka njia ya Mapinduzi makubwa ya kidemokrasia katika siasa za Tanzania kwa vitendo, tayari Seif Shariff Hamad ameshatanguliza mguu mmoja ikulu...na si mda mrefu ndgu zetu Tanzania bara wataona utamu wa mabadiliko hayo, ambayo bila shaka, yatachochoea na wao kutaka hali kama hiyo kwao...waliokuwa hawana mpya ni CCM, tokea uhuru mpka leo nchi inanuka njaa na ziki.
 
Prof Lipumba achukua fomu kuwania urais

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba ametangaza rasmi azma yake ya kuchukua fomu ya kuwania kugombea nafasi ya Urais katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu.

Hii itakuwa ni mara yake ya nne kuwania nafasi hiyo kupitia chama chake kwa upande wa Tanzania Bara.

Profesa Lipumba alisema ameamua kuchukua fomu ya kuwania Urais ili kuhakikisha nchi inatoka katika tatizo la uongozi dhaifu pamoja na CCM iliyogawanyika.

Aliwaomba wanachama wa CUF pamoja na wananchi kumuunga mkono katika hatua yake hiyo.

"Wana CUF na wananchi wote mnatakiwa kuungana ili tuweze kufanya mabadiliko, hili CUF inaweza kufanya endapo itapewa ridhaa ya kupewa madaraka...Nawahakikishia kama tukiongoza nchi tutatembea juu ya maneno yetu na sio vinginevyo," alisema.

Akitangaza azma yake hiyo wakati akifungua kikao cha Baraza Kuu la chama hicho kilichofanyika makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam, Lipumba aliitupia serikali lawama kutokana na matatizo mengi yanayoikabili nchi.

Alisema hali ya nchi kwa sasa kuanzia kisiasa, kiuchumi na kijamii inatisha kutokana na Rais Kikwete kushindwa kuwajibika kiutendaji.

Lipumba alisema katika kujikomboa umefika wakati sasa kwa wananchi kuanza kazi ya kudai mabadiliko ya haraka ili nchi iondokane na hali duni iliyopo hivi sasa.

Alisema, wananchi wa kipato cha chini ndio wanaopata athari za kuyumba kwa uongozi baada ya bei za bidhaa mbalimbali kupanda mara nne ya bei ya huko nyuma pamoja na nafasi za ajira kupungua na kusababisha kundi la watu maskini kukua kwa kasi.

Mwenyekiti huyo wa CUF alisema, katika ripoti iliyotolewa na Benki ya Dunia imeonyesha kati ya Watanzania 100, watu 89 hawana ajira na hivyo inaonyesha dhahiri hata maelezo ya serikali inayosema watu wengi wamepata ajira kuwa ya uwongo.

Aliongeza kwamba katika kipindi chote cha CCM kuwepo madarakani hakuna sekta iliyoonyesha kuboreka na kutoa mfano wa huduma ya umeme, barabara, maji afya na elimu kuwa mbaya na hivyo kuhatarisha mwenendo wa ukuaji wa uchumi.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
 
mambo yanaanza kuiva, kwa upinzani hakuna ambae ameamua kutangaza nia ya kugombea ila lipumba, na yeye kasema atafanya na mazungumzo na wpinzani wenzake wamuunge mkono kwa urais na yy atawaunga mkono kwenye ubunge, ili kuwe na wabunge makini na rais makin i kisha wataunda serikali ya kitaifa
 
Anaingia tena profesa wa pumba! Unless kama Nipashe hawajamquote complete, sijaona mahala kagusia ufisadi -- jinsi gani atapigana na kansa hiyo.
 
kwanza naomba usahihishe heading, ametangaza adhma ya kuchukua fomu na sio keshachukua fomu.

kwa kweli uchaguzi wa 2010 tunategemea utakuwa wa aina yake, japokuwa naamini wananchi bado hawana imani na upinzani.

CCM watu wemechoka nayo ila pa kuelekea hawapaoni, pamezibwa

lkn tuangalie nn kitafuatia. LIPUMBA ni kiongozi mzuri ila mazingira hayoko condusive kwa sasa kuwa rais pamoja na CUF kuwa madarakani hasa kwa bara
 
20 yrs still fighting his desire to the state house! he must be joking
 
Kwa maneno mengine katika kipindi chake chote hicho akiwa kiongozi wa CUf ameshindwa kuwahamasisha wananchi wengi waikubali CUF kwa lengo la kuingia madarakani.
 
Shida ya CUF ni kwamba wanaibuka zaidi kwa sura za kimigogoro, kimiafaka, kimaandamano, etc.
Katika cool-environment ni kama vile wana'hibernate!
BTW, Lipumba kila la heri katika Azma yako!
 
Anaingia tena profesa wa pumba! Unless kama Nipashe hawajamquote complete, sijaona mahala kagusia ufisadi -- jinsi gani atapigana na kansa hiyo.

Huyu profesa alniichomoka tangu pale alipoungana na mama sofia Simba na Mkuchika kutetea hadharani wahutumiwa wa ufisadi -- mafisadi papa, waliotangazwa na Mzee Mengi. Alinisahangaza kweli kweli! Halafu akaja kutetea suala la ununuzi wa mitambo ya kufua umeme chakavu na ya kifisadi ya Dowans!!

Eti mtu huyu anataka urais tena!!!!
 
20 yrs still fighting his desire to the state house! he must be joking

Naona kugombea kwake kwa urais anafanya mradi wa kiuchumi. Watu wanabuni namna nyingi ya kuishi sustainably.

Naomba Malaria Sugu atufafanulie hapa -- asije na utumbo lakini!
 
Lipumba%2812%29.jpg

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba
 
Back
Top Bottom