Elections 2010 Lipumba Amfagilia Dr. Slaa

Lukolo

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
5,143
3,196
Akizungumza wakati wa kutangaza majina ya wagombea wa nafasi ya ubunge na uwakilishi yaliyopitishwa na Baraza Kuu la Uongozi, Dar es Salaam jana, Profesa Lipumba alisema pamoja na umakini wa Dk. Slaa, lakini amechelewa kutangaza nia yake hiyo na kuwa yeye yuko tayari kupambana na wanaoitafuna nchi.

“Awali Slaa, (Freeman) Mbowe, Dk. (Sengodo) Mvungi, (Augustino) Mrema, wote waliweka bayana kuwa hawatagombea, na sisi kupitia mchakato wetu tukaamua kugombea tukijua kuwa kuna mambo mengi ambayo tunayadai bado hayajatekelezeka na watu wamechoka hususan vijijini ambako sisi ndio tutakwenda,” alisema Profesa Lipumba na kuongeza: “Slaa ana haki ya kufanya hivyo na Chadema kina haki kumsimamisha.

Slaa ni rafiki yangu, na ninajua kuwa ni mtu makini na aliyefanya mambo mengi mazuri hususan katika Bunge kwa kushirikiana na wabunge wa vyama vingine vya Upinzani, lakini amechelewa kutangaza nia yake.

Namtakia kila la heri. Ila mimi nitasimama kupambana na mapapa, sangara na nyangumi wa rushwa.”
Source: Habari Leo
Kwakweli kauli hii imetoka mdomoni kwa mtu makini anayeelewa ni nini anafanya kwa maslahi ya taifa. Kauli ya Lipumba inaashiria kwamba endapo Dr. Slaa angetangaza nia mapema, basi yeye Lipumba angeweza kujitoa ili kumpisha Slaa. Natamani akina MS KN na Tumain waseme lolote kuhusu hili.
 
Kwakweli kauli hii imetoka mdomoni kwa mtu makini anayeelewa ni nini anafanya kwa maslahi ya taifa. Kauli ya Lipumba inaashiria kwamba endapo Dr. Slaa angetangaza nia mapema, basi yeye Lipumba angeweza kujitoa ili kumpisha Slaa. Natamani akina MS KN na Tumain waseme lolote kuhusu hili.
Prof. Mapumba hajachelewa anaweza kujitoa sasa
 
kwa nini asijitoe slaa? Hapa ndo ninapowachoka wapinzani.....! Nyumba moja wanagombea fito!

for the reason that chadema wamejitoa znz , same reason cuf watajitoa kwa urais wa jamuhuri,
kama bado kuelewa ni kuwa you support the one who is more likely to win .
 
Kauli ya kusema Dr Slaa kachelewa haina mantiki kabisa katika siasa -- nawashangaa wote mnaoikweza! Suala la kuachiana ni mazungunmzo baina ya pande zote husika na kufikiwa makubaliano. Au yapo makubaliano hayo katika kam,bi ya upinzani -- ya kusema yule anayeanza kutangaza kugombea basi ndiyo anastahili kugombea?

Watanzania -- mbona mnakua hovyo hovyo tu namna hii katika kujenga hoja?
 
Lipumba asingeweza kumwachia Dkt Slaa kwa vile CUF wana deni la fadhila wanalopaswa kumlipa Fisadi Rostam.Sintashangaa huko mbele wakielekeza mashambulizi kwa Slaa badala ya JK.
 
AT THE END OF THE DAY WOTE WATAGOMBEA....NAMI NITASHINDWA KUIGAWANYA KURA YANGU KWA WATU WA UPANDE MMOJA......!guess where my single lot will go!!!!!
 
Ufisadi wa kutisha
• Trilioni 1.7/- zatafunwa serikalini

na Edward Kinabo


amka2.gif
SERIKALI ya Awamu ya Nne imeendelea kukumbwa na jinamizi la matumizi mabaya ya fedha za umma (ufisadi), baada ya kubainika kuwa imetumia sh trilioni 1.7 kwa kipindi cha mwaka 2008/2009 bila maelezo ya kina.
Uchambuzi huo ni ule uliotolewa na Shirika lisilo la kiserikali la ‘Agenda Participation 2000' juu ya ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) iliyotolewa hivi karibuni, umethibitisha kuwepo kwa ufisadi mkubwa wa fedha za walipa kodi.
Uchambuzi wa ripoti hiyo ya CAG kwa mwaka 2008/2009, umeonyesha ufisadi wa kutisha serikalini kwa kiasi cha sh trilioni 1.7 uliofanyika ndani ya mwaka huo.
"Jumla ya fedha za serikali ambazo ama zilitumiwa vibaya au wahusika wameshindwa kutoa maelezo ya kuridhisha jinsi fedha hizo zilivyotumiwa inafikia shilingi trilioni 1.7. Kwa kweli fedha hizi ni nyingi sana…", ilisema sehemu ya taarifa hiyo ya shirika hilo.
Kiasi hicho kilichofujwa ni sawa na fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya bajeti ya Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi na ile ya Miundombinu katika mwaka huo wa fedha.
Kiasi hicho pia ni sawa na mara mbili ya fedha zilizokuwa zimetengwa mwaka huo kwa ajili ya Wizara ya Afya ambayo ilipata sh bilioni 589 na mara nne ya kiasi kilichokuwa kimetengwa kwa ajili ya Wizara za Kilimo na Maji, ambazo zilitengewa shilingi bilioni 379 na shilingi bilioni 309 katika mwaka wa bajeti wa 2008/2009.
Kwa ujumla, ufisadi huo unahusisha makadirio ya fedha zilizotumiwa vibaya katika eneo la manunuzi yasiyo ya kawaida ya sh bilioni 12.8, masuala ambayo hayakushughulikiwa tangu kaguzi zilizopita sh bilioni 95.7 na misamaha ya kodi ya sh bilioni 752. 3.
Maeneo mengine ni udhaifu katika ulipaji wa mishahara uliofuja sh bilioni 3. 078, masuala yahusuyo malipo ya marupurupu sh milioni 395.8, ukiukwaji katika ununuzi wa magari wa sh bilioni 4. 018, pamoja na kiasi cha sh bilioni 203.2 zilizotumiwa vibaya au kupotea katika serikali za mitaa.
Katika ufisadi huo, Wizara ya Maliasili na Utalii ndiyo imetajwa kama mfano wa kusikitisha wa wizara zilizotumia vibaya fedha za umma.
Sehemu ya ufisadi uliofanyika ndani ya wizara hiyo inahusisha ubadhirifu wa sh milioni 12 zilizolipwa kama mishahara zaidi ya viwango halali vya mishahara ya wafanyakazi na sh milioni 53 zilizolipwa bila kutolewa viambatanisho vya kuhalalisha malipo hayo.
Sh milioni 445 pia zilitumika kulipa wastaafu, marehemu na wafanyakazi walioachishwa kazi, fedha ambazo walengwa hawakujitokeza kulipwa lakini hazikurudishwa hazina.
"Jambo jingine la kusikitisha ni kwamba Wizara ya Maliasili na Utalii ilishindwa kueleza yalipo mapato ya jumla ya shilingi bilioni 19.6," ilisema sehemu ya uchambuzi huo wa Agenda Participation ikirejea ripoti ya CAG.
Mbali na wizara hiyo ya Maliasili na Utalii, wizara, idara au taasisi nyingine za umma zilizopata taarifa mbaya za fedha kutoka kwa CAG ni Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Jeshi la Polisi na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Nayo Serikali ya Norway imeendelea kudai kurudishiwa sh bilioni 2.6 zilizotumiwa vibaya na Wizara ya Maliasili na Utalii.
Hata hivyo, katika taarifa ya bajeti ya wizara hiyo ya mwaka huu wa fedha, wizara hiyo ilisema kuwa ingeilipa Serikali ya Norway fedha hizo.
"Taarifa ya CAG pia inaonyesha utendaji usioridhisha katika nyanja ya mikopo iliyokuwa ikisimamiwa na taasisi za serikali kwa ajili ya wajasiriamali wadogo wadogo miongoni mwa wanawake na vijana nchini.
"Kwa mfano jumla ya sh milioni 355 zinazodaiwa kutolewa kwa wajasiriamali wanawake na vijana hazikuonyeshwa jinsi zilivyotumika. Taarifa za fedha kutoka halmashauri 41 hazikupatikana," ilieleza taarifa hiyo.
Mashirika ya umma na mamlaka kama vile Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Shirika la Bima la Taifa (NIC), Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Shirika la Taifa la Umeme (TANESCO), Mamlaka ya Bandari (TPA) na Mfuko wa Hifadhi wa Serikali za Mitaa (LAPF) ni maeneo mengine ya upotevu mkubwa wa fedha.
Kwa mfano, ilithibitishwa kuwa jumla ya sh bilioni 58 zilizokuwa zimetolewa kama mkopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu mwaka 2006, mpaka sasa hakuna uhakika wa kulipwa kwa fedha hizo ambazo zilitolewa dhamana na serikali.
"Kinachowasikitisha wengi ni kwanini serikali bado inashindwa kuziba mianya ya baadhi ya maofisa wake kuendelea kutafuna fedha za umma," umehitimisha muhtasari wa wachambuzi wa wanaharakati hao.

:love:
 
acha uongo hajasema hivyo,amesema anamrespect dk slaa kama mmoja wa watu anaowarespect
 
acha uongo hajasema hivyo,amesema anamrespect dk slaa kama mmoja wa watu anaowarespect
Kwa mtu yoyote mwenye akili timamu anajua kama umegombea uraisi zaidi ya mara mbili na ukashindwa mara ya tatu na nne kuna uwezekano mkubwa kupata kura chache zaidi ya ulizopata before, sembuse msomi wa Stanford university ashindwe kujua hilo.Sioni kitu chochote kilichomsukuma yeye kugombe zaidi ya kulipa fadhila.Haita nishangaza wakati wa kampeni mashambulizi yake yakiwa ni kwa Dr Slaa

Mkuu Wun...Malaria Sugu anachosema ndio Lipumba atakachosema huko mbeleni,hiyo ndio siasa yenyewe.Lipumba kama walivyo wanasiasa wengine anajua watanzania wepesi wa kusahau mambo,hawawezi kukumbuka mtafaruku uliotokea wakati wa kifo cha Chacha Wangwe kati ya Chadema, TLP na Cuf. Sasa hiyo heshima sijui imetoka wapi sasa hivi.
 
jana nilimsikia Prof lipumba kupitia star tv kwamba dk slaa kiherere kwani mwanzo yeye, mbowe na dk mvungi walitangaza nia ya ubunge lkn ghafla dk slaa akageuka na kuutaka urais .
alisema yeye kama lipumba anayonguvu ya kupambana na mafisadi na kumtaka dk slaa alikuwa agombanie ubunge .
sasa jee kama dk slaa amegeuka ghafla baada ya ubunge urais , hatuoni watz anaweza kuacha urais na kukimbilia UNO ambapo atasema anataka awakomboe walimwengu waliopo kwenye shida?

Wewe ni mwongo uliyetukuka. Ni sifa kuu ya wana CCM kuanzia katibu mkuu wao
 
Ukishaonja ndoana na MAFISADI wewe kyishnei....sasa prof. anaongea nini???? Kama anamweshimu Dr Slaa...Apishe njia tu
 
jana nilimsikia Prof lipumba kupitia star tv kwamba dk slaa kiherere kwani mwanzo yeye, mbowe na dk mvungi walitangaza nia ya ubunge lkn ghafla dk slaa akageuka na kuutaka urais .
alisema yeye kama lipumba anayonguvu ya kupambana na mafisadi na kumtaka dk slaa alikuwa agombanie ubunge .
sasa jee kama dk slaa amegeuka ghafla baada ya ubunge urais , hatuoni watz anaweza kuacha urais na kukimbilia UNO ambapo atasema anataka awakomboe walimwengu waliopo kwenye shida?

Wewe unayeokota makombo ya wanaokutuma ndiye mwenye kiherehere. Kauli wa Watu wengi ni .....
 
Lipumba ni mwongo, ana tamaa ya madaraka na kutaka kuwaharibia wenzake tu. Kama yeye amejaribu mara tatu bila mafanikio, na tena mwaka 200o aliungwa mkono na CHADEMA, ni nini jipya atakalofanya mwaka huu badala ya kujitoa ili kuongeza nguvu kwenye upepo wa mageuzi?
 
Ni wakati wa sisi wasomi na weledi na sio wakina ms na tumaini lakini kutumia media mbalimbali kuviunganisha vyama vya siasa haswa upinzani kuelekea uchaguzi mkuu ili kukingoa ccm,kwani chadema,cuf na watanzania wote adui yao ni ccm
 
Lipumba Mnafiki

Lipumba ni mchumia tumboni; anatunzwa na ruzuku ya wanaCUF toka visiwani wakati huku bara yeye hata ubunge hapati!! Anajua wazi kua mara zote CCM wamemgaragaza sasa kiherehere cha kusema Dr. Slaa amechelewa kinatoka wapi? Angekuwa mtu mzalendo halisi kama anavyotaka watu wamuone, angejitoa na kumuunga mkono Dr. Slaa mwenye nguvu zaidi ya kumuangusha mlinda mafisadi!!
 
Lipumba ni mchumia tumboni; anatunzwa na ruzuku ya wanaCUF toka visiwani wakati huku bara yeye hata ubunge hapati!! Anajua wazi kua mara zote CCM wamemgaragaza sasa kiherehere cha kusema Dr. Slaa amechelewa kinatoka wapi? Angekuwa mtu mzalendo halisi kama anavyotaka watu wamuone, angejitoa na kumuunga mkono Dr. Slaa mwenye nguvu zaidi ya kumuangusha mlinda mafisadi!!
Upo sahihi kabisa Bulesi. Kwa kuwa tayari ana kiri kwamba Slaa yupo vizuri, mimi ningemshauri afanye tu maridhiano na Slaa ili Slaa atakapopata Urais yeye apate japo uwaziri mkuu au hata uwaziri wowote hata kama ni ndani ya ofisi ya waziri mkuu. Kugombea kwake Urais na mwaka huu kunaweza kumfanya afe bila kuona cheo chochote cha serikali. Watu wake wa karibu mpeni ushauri huu wa bure.
 
Back
Top Bottom