Lipi la kujivunia miaka minne ya JK Ikulu?

Hana la kurekebisha aende msoga tu akale pesa za walipa kodi anazotafuna na kutuachia nchi yetu wenyewe. Hatukupigania uhuru kuwaachia akina sin bin Clair na RA na waarabu wake waliochukua mababu zake utumwa kutafuna rasilimali zetu. Wengine tuna jadi ati hatukukubali kuchukuliwa utumwa na kuwa ma-puppet wa waarabu.
 
mimi binafsi cha maana saana ninachoona huyu bwana kafanya ni:

1 ile hotuba ya kwanza bungen (ilikuwa nzuri)
2 kumlazimisha mahita astaafu mapema
3 kumwachisha kazi balozi mahalu na kusema ni mwizi
4............
5..........

mapungufu yake huyu bwana

1 amekuwa na fadhila sana
2 anakurupuka katika maamuzi
3 ni rahisi sana kudanganyika huyu bwana na kufaata ushauri wa mtu ambao ni uongo
4 amekuwa na safari nyingi sana
5 mpaka sasa amesimama huu ya mabega ya mkapa
6 usalama wa taifa unafanya kazi yake sana lakini mkulu hafanyii kazi majalida na riport anazopewa,
7 maendeleo mengi ni ya kinadhalia sana
8. anapenda kuwa na marafiki matajiri wakati yeye ni masikini
9. kuna hatari huyu bwana akaikwaza nchi hii kuliko hata mwenzake aliyepita.
10...........
11...........
12---------

huyu mimi bwana eti hanifani jamani sijui nyie wenzangu!
Well said!!
 
Hii mada ni nzuri sana kwa ajiri ya kusaidia watu kufanya decision ukichulia kuwa tunaelekea kwenye uchaguzi, let's be objective tusaidie watu wafanye maamuzi maana wengine hapa hawajui watampigia nani kura

Naungana na mchangiaji mmoja hapo juu aliyesema kuwa evaluation inategemea na manifesto (strategic plan) maana huwezi kuevaluate Rais kutoka hewani, kuna njia mbili tunaweza kumwangalia JK, moja ni kuangalia ahadi alizozitoa wakati wa uchaguzi, je ametimiza kwa percentage ngapi? Njia ya pili ni kumlinganisha na marais waliopita kwa kipindi kama hiki.

Kwa ahadi alizozitoa nafikiri even 10% hajafikisha, sijui inawezekana naelewa vibaya ilani ya CCM, kuna quantitative na qualitative promises hazija timizwa na uwezekano wa kuzitimiza haupo.

Je kwa marais waliotangulia, nafikiri kwa kipindi kama hiki the man still worse kwani hali ya maisha imepanda maradufu na ni bora waitumie slogan yao ya maisha bora kwa kila mtanzania tena. Kwa mtu ambaye hawezi kupata extra income hali ni mbaya sana na nina wasiwasi kama yeye analijua hili

Lakini hata hivyo kuna tangible achievement zinazoonekana kama dodoma university, barabara ya arusha singida, na mengineyo
 
Wakuu wana bodi,

Ni muda mrefu sijapost thread hapa,ila leo wakati tukiendelea kuisubiria Sikukua ya kuzaliwa kwa bwana Yesu Kristo nimeona ni vyema kuanza na thread hii.

Binafsi nampongeza mhe. Rais kwa kuweza kuliongoza taifa letu kwa miaka Minne,tumepitia mambo mengi ,msikusuko mingi na mambo kadha wa kadha.

Ila leo yakiwa yamepita masaa 48 ningependa tukumbushane ni yapi mazuri aliyofanya na yapi tunaona ni wa kati muafaka kumshauri mhe. Rais ayafanyie kazi kw akipindi cha mwaka mmoja ujao.

naomba tujadili..
gview.jpg

Btw the Line,I smell something fishy on ATCL.Stay tuned!

Mazuri ambayo yanatakiwa yaendelezwe:

1. Amesimamia ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma
2. Ametoa uhuru wa watu kutoa maoni yao hata yale ambayo yanampinga moja kwa moja. Mkapa alikuwa akiminya uhuru wa vyombo vya habari na alidiriki hata kuwakashfu Wakati wa mahojiano yake na Riz Khan wa CNN wakati huo.
3. Amewaruhusu wabunge wa CCM kuongea kwa uwazi zaidi bila ya vitisho - utakumbuka kuwa Rais mstaafu Mkapa aliwafunga midomo wabunge hawa wanaojiita wapiganaji wa ufisadi na walifyata mkia.
4. Ameruhusu baadhi ya mafisadi kufunguliwa kesi mahakamani - refer Mramba, Yona, Mgonja etc.
5. Alikuwa radhi Baraza lake la mawaziri na hasa waziri mkuu ajiuzuru baada ya kashfa ya Richmond
6. Ameipa meno zaidi ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa serikali (CAG) ambayo imekuwa chanzo cha kugundulika kwa kashfa nyingi tunazozijua hivi leo.
7. Ameendeleza uhusiano mwema wa Tanzania na majirani zetu na aliweza kuwa kiungo muhimu wakati wa mgogoro wa Kenya tofauti na Rais wa Uganda Yoweri Museveni ambaye pamoja aliamua kuegemea upande mmoja.

Mapungufu ambayo yanahitaji marekebisho

1. Vita dhidi ya ufisadi ambayo kwa sasa Serikali imekuwa legelege has katika kuchunguza na kuwafungulia mashitaka watuhumiwa. Serikali imekuwa ikilalamika zaidi ya kuchukua hatua.
2. Safari nyingi za nje na ndani ya nchi ambazo tija yake ni vigumu kuitathmini.
3. Kushindwa kukamilisha kwa wakati miradi mikubwa ya barabara ambayo aliirithi toka kwa mkapa ikiwepo barabara ya kati ya Manyoni na Singida na barabara ya kusini.
4. Kuendesha nchi kwa kauli mbiu ambazo hazina mipango kamili ya utekelezaji wala usimamizi - Kilimo Kwanza, Nguvu mpya ari mpya na kasi mpya ni baadhi ya kauli mbiu hizo.
5. Kuendeleza matumizi mabaya ya fedha za umma kwa ugawa fedha kiholela bila kuwa na utaratibu unaoeleweka wa kizisimamia na kujua impact yake kwenye jamii - refer Mabilioni ya Kikwete (Tshs 21 billion)
6. Kutoa matamshi ambayo yanatiashaka na umakini wa Serikali katika kusimamia sheria za nchi - mf. madai kuwa ana majina ya wala rushwa, majambazi na wakwepa kodi kuwa anawapa muda wajirekebishe.
7. Kutotekeleza ahadi za wakati na baada ya kampeni - mfano ni ile ya kurudisha nyumba za Serikali hasa zilizo katika maeneo yenye taasisi nyeti zilizoporwa na Mkapa, Magufuli na mafisadi wengine wa awamu ya tatu.
8. Kuendeleza sera potofu za awamu ya tatu za kukumbatia wageni - waliobatizwa kuwa wawekezaji - na kuwakandamizi wananchi wa hali ya chini. Refer wananchi wa Babati wanaohamishwa kwenye maeneo yao kupisha mwekezaji.

Naamini kuwa mapungufu haya yanarekebishika ikiwa Rais ataamua kwa dhati ku
 
Tata said:

Tata,

..asante kwa uchambuzi wako mzuri.

..the negatives outweighs the positives.

..tukimchagua tena JK ujue imekula kwetu wananchi.

..kama Raisi ameharibu kazi ktk 1st term usitegemee atakuja kujirekebisha on the 2nd term.

..
 
How do you come to such conclusion. Umepima kwa kutumia nini?
 
bnhai,

..soma posting ya Tata niliyo-quote.

..I didnt go outside what Tata had written to come up with my conclusion.

..naamini ukilinganisha mazuri vs mapungufu kama alivyotusaidia Tata uta-conclude kwamba JK kazi imemshinda.
 
Anafaa kupongezewa kwa
1. kui-structure polisi operation system ya Tanzania before 2005 enzi za Mahita na Mkapa polisi walikuwa mungu watu lakini at least enzi hizi polisi wameanza kufahamu utu na kwamba wameajiriwa na wananchi bravo kamanda Wema na Kikwete

2. Kuanzishwa kwa mpango wa ujenzi wa dispensary kila kata unafaa kupongezewa japo upungufu wa wataalamu na madawa unahitajiwa kushughulikiwa bravo JK kwa kuanzisha huduma hii ya msingi kwa binadamu fanya bidii zaidi..

3. Uhuru wa uandishi, kutoa mawazo na kuongea bila hofu ya kunyanyaswa, kufuatwa na vyombo vya dola ni hatua ya kupongeza japo kuna watu wanafikiri ni kuwa mdhaifu kwangu mimi naona anajenga utamaduni mzuri unafaa uachwe ukomae mpaka wananchi wazoea kuchambua pumba na mchele ni upi katika kelele nyingi kutoka kwa watu wengi..tumepata fursa ya kufahamu aina viongozi wa kidini na kisiasa tulionao baada ya kuruhusiwa kupayuka bravo Kikwete endelea kuwa mvumilivu na mstaarabu.

4. Kuanzishwa kwa chuo kikuu cha Dodoma ni jambo kubwa linalotokana na juhudi zake binafsi linafaa kupongezwa japo nafikiri ni wakati muafaka kwa kila mkoa kuwa na state university mfano:- Rukwa state university, Mbeya state university, manyara state university nk...sioni sababu ya mkoa mzima kukosa university ni aibu kwa karne hii

5. Kuwapeleka mawaziri na makatibu wakuu kwenye mkono wa sheria ni hatua inayofaa kupongezewa kwakuwa kwanza ilikuwa kama ajabu kwetu sisi ah haiwezekani waziri? lakini imesaidia ma-oficcer wengi serikali kuwa makini na maamuzi yao..ni kweli usiopingika kuwa hatua hii imesaidia taifa kuokoa mipesa mingi kwakuwa sasa kuna uwoga katika kuchukua uamuzi wa kijinga..japo wanasheria wa serikali wamekosa kabisa uzalendo kabisa kwa kupeleka kesi za kijinga ili washtakiwa washinde..sic bravo kikwete kwa kuonyesha mfano...

6. Uamuzi wa kukataa east african fast tracking na kulinda ardhi yetu ni wa kupongezwa kwa kuwa wananchi wengi bado wanahofia kuwa EAC haina maslahi kwa wa Tanzania ni hatua nzuri kwakuwa amekuwa mzalendo...ingekuwa mkapa hapa hata poilsi wangetumika kama alivyoingiza net group solution tanesco...bravo JK

Nawakilisha
 
Pamoja na mafanikio mengine, Kikwete kwa miaka minne ya uongozi wake amefanikiwa kufanya yafuatayo:

1. Kumteua Mh. Makamba kuwa Katibu Mkuu wa Chama Chetu. Mh. Makamba anaweza kusema chochote kwa haraka bila kufikiri sana ili kukitetea chama na Mwenyekiti wetu.
2. Amefanya maamuzi magumu ya kutowaondoa katika uongozi wa Chama watuhumiwa wa Richmond na EPA ambao ni wajumbe wa H/Kuu na Kamati Kuu.
3. Amejitahida sana kuhakikisha kuwa anatunza siri za Meremeta.
4. Ameonyesha ujasiri wa kutotekeleza maagizo ya Bunge yaliyoitaka Serikali kushughulikia mafisadi. Hapa ameonyesha kuwa ni kiongozi mwenye msimamo na asiyependa kusukumwasukukmwa.
5. Ameonyesha msimamo wa kutoyumbishwa kwa kukaa kimya bila kuwachukulia hatua viongozi walioghushi vyeti vya Elimu.
6. Ameonyesha uwezo mkubwa wa kutotimiza ahadi kama vile ya kushughulikia orodha ya wauza madawa ya kulevya aliyokiri kukabidhiwa.
7. Kwa kiasi kikubwa amefanikiwa kutimiza ahadi ya kuunda serikali ya wana mtandao.
8. Ameweza kuwa na Serikali kubwa yenye mawaziri wengi wasio na uwezo.

Kwa hakika mafanikio ya Mhe. Kikwete ni mengi kiasi kwamba siwezi kuyaorodhesha yote. Haya ni ni baadhi tu ya hayo mengi.
 
How do you come to such conclusion. Umepima kwa kutumia nini?

Premise ni kuwa mgombea wa urais, hutumia ilani yake kwa ahadi ya kuwa ataisimia utekelezwe! akichaguliwa athakikisha aliyoahidi kwa sehemu kubwa yametekelezwa ili aweze kuomba ridhaa kwa mara ya pili na wananchi mmwamini. Kipindi cha pili Raisi anatekeleza ilani kwa lengo la kulinda chama kiaminike tena. Muungwana however, has failed the party and himself, given the fact that miaka minne aliyofanya kazi hayaonyeshi chochote sanasana kutufanya sisi wadau ndo punguani kwani leo watu ndo wanajua kuwa hawakuwa na kigezo cha maana kumpa Urais. alijua kuwa atasimama kuuomba ridhaa na kulikuwa na kila sababu ya kufanya vema japo kwa kuzuga ili apewe kipindi cha pili, hajaweza. Je nini kitamfanya afanye vema akipewa awamu ya pili? kumbuka huyu ni rais pekee tz aliyejiandaa kwenda ikulu kuliko marais wetu 3 waliotangulia. alijipanga kuongoza nji tangia 1995, senksi to Nyerere, that would have been the end of TZ, he was the wrong person to take over a rip country from Mwinyi. kama ziara zake akiwa waziri wa mambo ya nje hazikumsaidia hizi za sasa ndo zitampteza tu!

huyu kwa majungu na kuendekeza waganga, anatutumbukiza kwenye hatari, na shekhe wake katutishia basi sijui itakuwaje.

i am lost btn the translation, but mesji is sent
 
Back
Top Bottom