Lipi hasa Jukumu la Makamu wa Rais?

Kazi yake nyingine ni kuzima Mwenge wa TANGANYIKA ingawa yeye si MTANGANYIKA.
 
Unataka kusema tuliomo humu JF hatuna majukumu?Watu wanatembelea JF kwa kuwa wanetegemea kubadilishana mawazo na Great Thinkers. Kumbe wengine mko humu kwa kukosa la maana la kufanya?

Waweza kulinganisha majukumu ya Rais na yako? Na kwamba tutakukuta,Siasa thread zote,MMU thread zote,Jamii intelligence thread zote aah...jaribu kuelewa maana bana..tena iwe kutwa kucha kama wenzetu humu ndani.. Sidhani..labda sijui awe Rais kama yupi..
 
Kuwa mkali hakutusaidii kuelewa. Wewe mwenzetu kama unajua majukumu ya Makamu wa Rais tueleweshe na kama anayatimiza tupe mifano. Mbona hawa wenzetu kwa upendo mkuuubwa wametueleza jinsi wao wanavyomuona SHABABI akiweka majiwe ya msingi 'byurifli' na wala hawajawa wakali?!

Ama kama Mh. Shababi anakuhusu, basi mtetee kwa hoja na sio kutulazimisha. Ombwe ndio nini kaka?

Hakuna kazi isiyo na majukumu. Kiufupi serikali inayoongozwa na Mkuu huyu wa kaya, ni kama haina ajenda wala dira! Ukitaka kubomoa majengo yaliyojengwa bila mpangilio,unaambiwa mtemi na bosi wako.Tena bora akuite ofisini,anakunanga mbele ya wananchi saa nyingine wapiga kura wako! Unasubiri Rais atue wakati makamu wake yupo!Unapiga simu,unapata majibu.Kesho asubuhi akina mama wanatandika khanga kumpokea uliyehangaika awajibishwe..unahisi umedharaulika.. Hayo na mengine ndiyo ombwe la uongozi! Vacuum! Nani hajui kuwa Riz One ana uwezo wa kiutawala wakati hana nafasi yoyote. Mtu anashindwa kutekeleza majukumu kwani hajui mkuu au prince wake wana interests ama hawana katika masuala ambayo akiyashughulikia,akagonga mwamba mbele ya safari, unaadhirika.. Na unahatarisha mahusiano yako na mkuu. Ni kama vile nchi inajiendesha yenyewe,dereva kalewa,kalala..anakurupuka akigonga miti.Au kuna wanaoiendesha kaya hii. Mkuu wa kaya ni kama sanamu la kutisha wanyama shambani!
 
Huyu makamu aliepo sasaa ni sawa na mkuu wake maana wote walitaka tu wafikie kile cheo kutokana na umaarufu wao si uwezo...sasa kila mmoja aka fight kivyake akafika ...kwisha wametimiza azma z*o na si vinginevyo!!!
 
Waweza kulinganisha majukumu ya Rais na yako? Na kwamba tutakukuta,Siasa thread zote,MMU thread zote,Jamii intelligence thread zote aah...jaribu kuelewa maana bana..tena iwe kutwa kucha kama wenzetu humu ndani.. Sidhani..labda sijui awe Rais kama yupi..

Nimerudia kusoma majibu yako mara mbili sijaelewa unachotaka kusema hata kidogo. Jaribu kupanga maneno upya huenda nikakuelewa. Samahani
 
Mimi nimeamua kukubali yeshe............jamaa ntaalamu wa mafumbo huyuuu
 
Wanajamvi


Ni kweli kwamba cheo cha Makamu wa Rais kipo Kikatiba, na ni kweli kwamba mantiki ya Kuwa na Makamu wa Rais ni kuwa Stand By (hasa kwa wakati huu tunapoona misafara ya marais wengi ikiambatana na ambulance) , Lakini kwa miongo kadhaa sasa nimekuwa nikifuatilia majukumu ya makamu wa Rais na kugundua kwamba mintaarafu ni aidha kufungua mkutano!! au kuzindua kitu!! au kumpokea Rais!!! (Unaweza kuongeza na kutembelea mbuga za wanyama etc) ......... zaidi (chichemi mbaya au nzuri) ni pale unapokuwa na makamu ambaye ana waambata wawili au zaidi kwa wale wasioonekana pichani kulia na kushoto(nadhani mmenielewa)

Je mmna maoni gani wenzangu? (sitaki kuwafilisi kwa kusema huu si mzigo kwa Taifa?- nisije funguliwa kesi ya uchochezi)

Kutumia pesa za walipa kodi inavyotakiwa ni kazi yake lakini kikubwa anasubiri dingi afe achukue mikoba. Khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee asipokufa imekula kwake.
 
Nimerudia kusoma majibu yako mara mbili sijaelewa unachotaka kusema hata kidogo. Jaribu kupanga maneno upya huenda nikakuelewa. Samahani

kifupi sijadharau muda wangu wala wa yeyote humu JF... Hata hivyo sidhani kama Makamu wa Rais anaweza kuwa na muda wa kutosha daily kuandaa na kupost thread,au kuchangia thread tangu asubuhi hadi usiku! Tena achangie kila forum walau thread 1 na afuatilie mijadala ajibu maswali kama mnavyoniuliza hapa.. Time hiyo atakuwa nayo Rais wa nchi gani? Labda Kim Jong Il [marehemu] ambaye inasemekana alikuwa na uwezo mkubwa kichwani mwake wa kuendesha mambo!
 
Hiki cheo ni cha kisiasa zaidi ni cheo cha kuwaficha wanaoonekana kuleta ukorofi ukitoka humo huna haja tena ya kutaka ulichodhamilia. Bilal alitaka urais wa zanzibar akafichwa mle kwa gharama ya wadanganyika sidhani kama akitoka mle atautaka tena urais.
 
Nikiwa Olever kwenye Civics niliambiwa kazi ya VP ni 1. Poverty eradication 2. Environment management
Basing on those matters, huyu jamaa ana kazi ngumu sana. Tatizo hatekelei majukumu yake ndo maana hata umuhimu wake hauonekani. Kwanza alitakiwa yeye ndo akae vijijini kuwasaidia wananchi kuondokana na umasikini uliokithiri but the funny thing is yeye ndo amekuwa masikini wa mawazo. Kazi ni kwetu wapiga kura
 
Nikiwa Olever kwenye Civics niliambiwa kazi ya VP ni 1. Poverty eradication 2. Environment management
Basing on those matters, huyu jamaa ana kazi ngumu sana. Tatizo hatekelei majukumu yake ndo maana hata umuhimu wake hauonekani. Kwanza alitakiwa yeye ndo akae vijijini kuwasaidia wananchi kuondokana na umasikini uliokithiri but the funny thing is yeye ndo amekuwa masikini wa mawazo. Kazi ni kwetu wapiga kura

Poverty haimo bosi wangu! Ni union affairs na environmental management,tena zina mawaziri wake! Vision yao ni TZ with strong UNION and safe,healthy and sustainable ENVIRONMENT! Hii nimequote kwenye awamu hii ya nne.Hiyo ya kwako hata sijui ya awamu ipi...
 
ana wake wawili huyu,atawasapoti vipi?,..jamaa ni phd holder lakini ana wake wawili,..imani bwana.
 
Hii post sioni umuhimu wake. Kimsingi raisi wa zanzibar ndiye alitakiwa kuwa makamu wa raisi kama enzi za marehemu karume.
 
Back
Top Bottom