Lipi hasa Jukumu la Makamu wa Rais?

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,141
13,215
Wanajamvi


Ni kweli kwamba cheo cha Makamu wa Rais kipo Kikatiba, na ni kweli kwamba mantiki ya Kuwa na Makamu wa Rais ni kuwa Stand By (hasa kwa wakati huu tunapoona misafara ya marais wengi ikiambatana na ambulance) , Lakini kwa miongo kadhaa sasa nimekuwa nikifuatilia majukumu ya makamu wa Rais na kugundua kwamba mintaarafu ni aidha kufungua mkutano!! au kuzindua kitu!! au kumpokea Rais!!! (Unaweza kuongeza na kutembelea mbuga za wanyama etc) ......... zaidi (chichemi mbaya au nzuri) ni pale unapokuwa na makamu ambaye ana waambata wawili au zaidi kwa wale wasioonekana pichani kulia na kushoto(nadhani mmenielewa)

Je mmna maoni gani wenzangu? (sitaki kuwafilisi kwa kusema huu si mzigo kwa Taifa?- nisije funguliwa kesi ya uchochezi)
 
'nilimpigia cm mh Rais akasema nisubiri atue chini manake alikuwa anakwenda Africa ya kusini',ingekuwa amri yangu ningemfukuza kazi' mh. WAZIRI MKUU NA SAKATA LA JAIRO.
 
kazi zipo nyingi za kufanya hasa ktk nchi maskini kama Tz (no nchi yenye watu maskini) ndiyo maana ktk ofisi yake kuna mawaziri wa kumsaidia labda tatizo ni aina ya Makuamu wa Rais tunaye kuwa naye kwamba si muwajibikaji hadi inafikia kipindi tunasahau kama yupo au lah. Kidogo Dr Omari alikuwa anajitahidi
 
kazi zipo nyingi za kufanya hasa ktk nchi maskini kama Tz (no nchi yenye watu maskini) ndiyo maana ktk ofisi yake kuna mawaziri wa kumsaidia labda tatizo ni aina ya Makuamu wa Rais tunaye kuwa naye kwamba si muwajibikaji hadi inafikia kipindi tunasahau kama yupo au lah. Kidogo Dr Omari alikuwa anajitahidi

humjui Dr. Bilal vizuri wewe! Yule ni zaidi ya greda! We unajua chanzo cha PM kulialia hovyo kwenye issues? Hujaona Magufuli na Tibaijuka wanavyoshindwa kutimiza majukumu yao? Ama hujajua tatizo bado? Je unajua maana ya ombwe?? Tafakari,utaelewa..
 
Hii yote ni unnecessary mizigo tunayobebeshwa sisi walalahoi walipa kodi. Huwezi kuwa na system
ambayo tuna RAIS, VP, PM na wakati mwingine Second VP. Ndiyo maana kwa mtiririko huu wa
kurudikiana vyeo VP amebaki kutembea na mikasi tu mifukoni, ndiyo hana kazi!

Kama tunafuata system US basi RAIS na VP wanatosha hakuna haja ya kuwa na PM. Kama tunafuata
system ya UK basi tuwe za PM mtendaji (kama India) vyeo vya RAIS, VP tuondoe.

Lakini kwa kuwa mi-afrika (inluding me) tumelaaniwa tunaona sahihi watawala hawa weusi kujirundikia
vyeo eti tunasema wameula! Ona sasa kule ZNZ eti RAIS, First VP, Second VP, ka nchi kenyewe sawa
na mkoa wa Tangayika, sijui huo mlolongo wote wa viongozi wa Kitaifa wanafanya nini? kuwakamua tu
masikini walipa kodi.
 
ha ha ha ha haaa..... Umesahau na mazingira kipindi kile,kipindi hiki hawakuandaa kazi ya kumpa. Unaweza kuta tumo naye JF kwa kukosa majukumu!
Unataka kusema tuliomo humu JF hatuna majukumu?Watu wanatembelea JF kwa kuwa wanetegemea kubadilishana mawazo na Great Thinkers. Kumbe wengine mko humu kwa kukosa la maana la kufanya?
 
humjui Dr. Bilal vizuri wewe! Yule ni zaidi ya greda! We unajua chanzo cha PM kulialia hovyo kwenye issues? Hujaona Magufuli na Tibaijuka wanavyoshindwa kutimiza majukumu yao? Ama hujajua tatizo bado? Je unajua maana ya ombwe?? Tafakari,utaelewa..

Kuwa mkali hakutusaidii kuelewa. Wewe mwenzetu kama unajua majukumu ya Makamu wa Rais tueleweshe na kama anayatimiza tupe mifano. Mbona hawa wenzetu kwa upendo mkuuubwa wametueleza jinsi wao wanavyomuona SHABABI akiweka majiwe ya msingi 'byurifli' na wala hawajawa wakali?!

Ama kama Mh. Shababi anakuhusu, basi mtetee kwa hoja na sio kutulazimisha. Ombwe ndio nini kaka?
 
ni mtu mwenyewe tu,hata pm wa sasa na aliepita tofauti,waziri wa uvuvi alepita na wa sasa tofauti,rc dar hakuwepo mwaka mzima na hakuna noma lkn huko nyuma walikuwepo wachapakazi,
tetesi kikwete alimtaka mama flani awe vp lkn kuondoa nogwa ya siasa znz ilibidi hy awepo
 
aa mimi huwa ananiogopesha akiongea utafikiri yupo icu anaongea taratibu kama mgonjwa vile ,hivi huwa ana ugonjwa gani ,msafara wake anatembea na ambulance au haamini hospital zetu?
 
Aliyekuwepo zamani marehem Omar Ally Juma anagalau yeye alikua anazunguka kuangalia Mazingira na kufunga viwanda vichafu..hawa waliofuata baada ya kifo chake sioni kabisa umuhimu wao,...kwa kweli hiki cheo bora kifutwe mana kinaongeza gharama tu...ama hiki ama PM kimoja kifutwe...
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom