Link ya kipindi cha njianpanda kuhusu shuhuda za Loliondo

Shetani anawapa watu matumaini ya uongo kuwa wamepona kumbe bado ni wagonjwa. Hii ni wazi kwani shetani kazi yake ni kuua na sio kuponyesha (Yohana 10:10). Watanzania amkeni mjue kuwa kinachofanyika Loliondo ni kazi za shetani tu
 
Ahsante Miss Judith lakini watu ni wagumu kuelewa na kukubali ukweli. Mungu akubariki kwa kujaribu kuwafungua watu macho.
 
mi naona huyu alienda loliondo kupma dawa ya babu kma inapnesha sasa inamuumbua kwa nn wngine wapone afu huyu pekee ndo ajfanye ajapona... chkua uamuz na fikiria
 
Nakuonea huruma we mama unavyohangaika na Loliondo. Una kanisa lililokimbiwa na wateja nini? POLE, Loliondo tutaenda tu hata ufanye nini.
 
Hivi kweli hakuna hata mwana jf mmoja ambaye ambaye ameisha tumia hiyo dawa hatuthibitishie ukweli halafu awe na uthibitisho wa kitaalamu tuache uthibitisho wa kiimani
 
mtasema yote mtamuumbua sana babu mara ni mchawi nk kwani wizara ya afya wangeshindwa kujua hiyo dawa ina masalia ya miili ya watu?? ushahidi wa waliopona ni mwingi akiwemo baba yangu mzazi ameumwa siku nyingi ametibiwa hospitali nyingi ametumia kikombe cha babu kapona vema huu ni mwezi wa nne hajatumia dawa yoyote anachapa kazi kwenda mbele na daktari wake amempina anashangaa.sasa kama hamna imani msiende huko na pole kwa makanisa ya kinafiki yanayoigiza babu ni mchawi kisa wamekosa waumini na watakosa kabisa watafunga tv zao na benk watakosa hela za kuhudumia,warudi Nigeria kujipanga upya kujiongezea nguvu.Hivi huko kwa matapeli mnafuata nini? nendeni kwenye makanisa yanayouhubiri wokovu wa akweli na sii kujigamba kuponyesha,kuwapa watu mali,hata yesu aliteseka nasi tunapaswa kuteseka pamoja nae ili tufike mbinguni na sii kufuata utajiri au mijihela kwani yesu alishawahi kutangaza hata siku moja leo ntapita mtaa fulani kuwaponya au kuwatoa umaskini> nauliza tena alishawahi?????? kweli tumesoma lakini tunaangamia kwa kukosa maarifa kiduchu tu.
 
Babu ni mwana imani wa kweli,anaponya na bila imani hata mbinguni hamtaingia....chungeni sana mnaomtukuza shetani!
 
Hapa shy town kuna mzee anaitwa fundi urasa alienda loliondo anaumwa kisukari baada ya kurudi akaamini kapona akaanza kunywa soda na vitu vyengine last week ilimpanda na kuambiwa aache kula sukari na pia hajapona kisukari kwa yeyote aso amini aje aulizie fundi urasa maeneo ya stand ya mabasi ya mikoani apate ushuhuda kw KKKT wanatapeli watu wakishirikiana na babu tafadhali OCAMPO wa ICC njoo utusaidie
 
Wajinga ndio waliwao.
 
Watu wengi wanapenda sana kudanganywa, tena wengine ufanya juu chini ili wadanganywe, ili wapate kudanganyika...!

Na kama hawakupata watu wa kuwadanganya, wanaugua na hata kupata matatizo ya akili.
 
Shetani anawapa watu matumaini ya uongo kuwa wamepona kumbe bado ni wagonjwa. Hii ni wazi kwani shetani kazi yake ni kuua na sio kuponyesha (Yohana 10:10). Watanzania amkeni mjue kuwa kinachofanyika Loliondo ni kazi za shetani tu

Mkuu kwani Mungu ana kanuni ya uponyaji?
 
Back
Top Bottom