Lini tutasikia tamko la JWTZ kuhusu mgogoro wa Malawi na Tanzania?

Status
Not open for further replies.

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,052
28,242
wakati wa uchaguzi mwaka 2010 tulishudia mnadhimu wa jeshi-Shimbo akitahadharisha juu ya tishio la amani nchini.je ni lini tutamsikia tena akiongelea juu ya tishio la usalama wa mpaka wetu na malawi?

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
Wanajeshi hawawezi kuanza kutoa matamko tamko tu wakati jitihada za kidiplomasia zinaendelea. Hilo litakuwa jeshi la kitoto.

Subiri diplomasia ichukue mkondo wake kwanza. Wanajeshi wakianza kusema sasa wanaweza hata kuharibu mazungumzo.

Halafu watu wanaoshabikia vita ndio hao hao hata wakiona mjusi tu wanakimbia.
 
Jeshi letu limegeuka nepi ya kisiasa kwa chama cha mafisadi. Usishangae ukakuta wakuu wa majeshi yote wana kadi za CCM kuthitisha walivyo hovyo na wasaka ngawira na wachumia tumbo. Anayebishia hili ajiulize mantiki ya aliyekuwa mkuu wa majeshi Robert Mboma kugombea ubunge. Namshukuru Mungu alichemsha. Jeshi lenye kuongozwa na wakereketwa wa chama tawala haliwezi kuwapo pale kulinda usalama wa bali maslahi ya wanasiasa kama ilivyo kwa jeshi la wanasiasa wa Tanzania (JWTZ).
 
Wanajeshi hawawezi kuanza kutoa matamko tamko tu wakati jitihada za kidiplomasia zinaendelea. Hilo litakuwa jeshi la kitoto.

Subiri diplomasia ichukue mkondo wake kwanza. Wanajeshi wakianza kusema sasa wanaweza hata kuharibu mazungumzo.

Halafu watu wanaoshabikia vita ndio hao hao hata wakiona mjusi tu wanakimbia.

nini kilichowafanya watoe tamko wakati wa uchaguzi?

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
wakati wa uchaguzi mwaka 2010 tulishudia mnadhimu wa jeshi Davis Mwamunyange akitahadharisha juu ya tishio la amani nchini.je ni lini tutamsikia tena akiongelea juu ya tishio la usalama wa mpaka wetu na malawi?

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA

Mnadhimu Mkuu wa JWTZ ni Luteni Jenerali A. Shimbo. Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ni Jenerali Davis Mwamunyange.
 
nini kilichowafanya watoe tamko wakati wa uchaguzi?

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA

Usilinganishe machungwa na matufaa.

Wakati wa uchaguzi hakukuwa na open confrontation iliyoweza kuwa escalated na tamko lao, na kwa kutoa tamko walikuwa wanathibitishia umma kwamba nchi ina usalama, tamko hili lilikuwa justified kwa minajili ya kuongeza usalama kwamba kama kuna mtu anataka fyokofyoko afikirie mara mbili maana asije kuivaa wrath ya jeshi.

Sasa mara hii tuna confrontation na nchi jirani, kuna wananchi dakika kumi na tano mbele washaanza kushabikia vita, huko kwa Wamalawi kuna watu wako gung-ho tayari, kwa hiyo tamko la jeshi ni rahisi sana kuwa counterproductive. Badala ya kutuliza hali, likazidisha escalation mambo yaende kuelekea vita hata pale ambapo mazungumzo yangeweza kumaliza matatizo.

Ndiyo maana nasema muda wa wanajeshi kusema haujafika.Kwanza Wanajeshi hawatakiwi kuwa watu wa kusema sema ovyo, hiyo ni kazi ya wanasiasa.Wanajeshi wao wanapewa amri, wanakwenda kufanya kazi tu.
 
Nimemsikia Lowasa tbc anasema amehakikishiwa na jeshi kwamba wapo makini na wamejiandaa vya kutosha kulinda mipaka yetu.
 
Usilinganishe machungwa na matufaa.

Wakati wa uchaguzi hakukuwa na open confrontation iliyoweza kuwa escalated na tamko lao, na kwa kutoa tamko walikuwa wanathibitishia umma kwamba nchi ina usalama, tamko hili lilikuwa justified kwa minajili ya kuongeza usalama kwamba kama kuna mtu anataka fyokofyoko afikirie mara mbili maana asije kuivaa wrath ya jeshi.

Sasa mara hii tuna confrontation na nchi jirani, kuna wananchi dakika kumi na tano mbele washaanza kushabikia vita, huko kwa Wamalawi kuna watu wako gung-ho tayari, kwa hiyo tamko la jeshi ni rahisi sana kuwa counterproductive. Badala ya kutuliza hali, likazidisha escalation mambo yaende kuelekea vita hata pale ambapo mazungumzo yangeweza kumaliza matatizo.

Ndiyo maana nasema muda wa wanajeshi kusema haujafika.Kwanza Wanajeshi hawatakiwi kuwa watu wa kusema sema ovyo, hiyo ni kazi ya wanasiasa.Wanajeshi wao wanapewa amri, wanakwenda kufanya kazi tu.
kwa nini Shimbo asijitokeze sasa na kutuliza wananchi kwamba mipaka yetu ipo salama?acha uwoga wa vita.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
wakati wa uchaguzi mwaka 2010 tulishudia mnadhimu wa jeshi-Shimbo akitahadharisha juu ya tishio la amani nchini.je ni lini tutamsikia tena akiongelea juu ya tishio la usalama wa mpaka wetu na malawi?

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA

wanajeshi hawatoi tamko. Jeshi linapewa amri na wanatekeleza. Mfano wakiamriwa wakawaue wanachadema lazima watekeleze amri. Wakiamriwa kuingiza powertillers nchini inatekelezwa
 
Shimbo aliambiwa atulie ule ni upepo si unaona umepita?anajilia vyake tu alivyodhulumu kwa wanajeshi wake!!sasa afanye nini maana analipwa fadhila kumsaidia JK miaka ile kule Monduli!!acha ale fadhila zake!4Tril sio nnyingi ni vijichenji tu!
 
wanajeshi hawatoi tamko. Jeshi linapewa amri na wanatekeleza. Mfano wakiamriwa wakawaue wanachadema lazima watekeleze amri. Wakiamriwa kuingiza powertillers nchini inatekelezwa
2010 wanajeshi walitoa tamko!

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
Utanyongwa kwa maneno yako mwenyewe,
Jeshi halisimamii usalama ndani ya nchi bali wa mipaka.
Lile tamko la mnadhimu wa jeshi lilikuwa la kisiasa,
na ni ukweli usiopingika kwamba aliingilia kazi ya POLISI.

Malawi wametamka wazi wanamiliki ziwa lote,
pia ndege zao zimetua ndani ya ardhi ya Tanzania,
Tamko la fyokofyoko wapi?Wakati hiyo ndo kazi yao asilia?
Jeshi halikutakiwa kutoa tamko,
lilitakiwa kukamata ndege zile,
mara zilipotua.
Najiuliza,
Ni kweli JWTZ wanalinda mipaka ya Tanzania?
Au wanalinda mipaka ya mikoa na wilaya?
au wanalinda masllahi yao CCM?

Usilinganishe machungwa na matufaa.

Wakati wa uchaguzi hakukuwa na open confrontation iliyoweza kuwa escalated na tamko lao, na kwa kutoa tamko walikuwa wanathibitishia umma kwamba nchi ina usalama, tamko hili lilikuwa justified kwa minajili ya kuongeza usalama kwamba kama kuna mtu anataka fyokofyoko afikirie mara mbili maana asije kuivaa wrath ya jeshi.

Sasa mara hii tuna confrontation na nchi jirani, kuna wananchi dakika kumi na tano mbele washaanza kushabikia vita, huko kwa Wamalawi kuna watu wako gung-ho tayari, kwa hiyo tamko la jeshi ni rahisi sana kuwa counterproductive. Badala ya kutuliza hali, likazidisha escalation mambo yaende kuelekea vita hata pale ambapo mazungumzo yangeweza kumaliza matatizo.

Ndiyo maana nasema muda wa wanajeshi kusema haujafika.Kwanza Wanajeshi hawatakiwi kuwa watu wa kusema sema ovyo, hiyo ni kazi ya wanasiasa.Wanajeshi wao wanapewa amri, wanakwenda kufanya kazi tu.
Nani aliwapa AMRI ya kusema WAPINZANI NI LAZIMA WAKUBALI MATOKEO?
Hawahitaji kusema walitakiwa wawe macho siku zote inaelekea wamelala kitanda kimoja na CCM, uvamizi wa Malawi ni news kwao.
 
kwa nini Shimbo asijitokeze sasa na kutuliza wananchi kwamba mipaka yetu ipo salama?acha uwoga wa vita.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA

Bila shaka JWTZ wanapaswa kujitokeza hadharani kuwahakikishia usalama wa mipka ya nchi hasa huko ziwa nyasa.
Kwa hali hii ambapo hata waziri wa ulinzi hajatembelea eneo lenye chokochoko na hajatoa tamko lolote kuwahakikishia ulinzi ni lazima wananchi wawe na wasiwasi wa mipaka ya nchi na usalama wa nchi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom