Linganisha Picha Hizi: JK Nyerere vs. JM Kikwete

Mwl Nyerere akiwa na familia, pili akiwa analima ameinama hajawekewa jamvi ili asichafuke, yule anabembea, na katika kupanda mti anawekewa jamvi! Contrast ni dhahiri.

Wengi wanaomlaumu Nyerere kwa hali mbaya ya uchumi hawaangalii mfumo mzima wa wakati ule. Nyerere hakuwahi kuwekewa vikwazo rasmi, lakini ukweli vilikjuwepo. Nchi za magharibi hazikuwa na upendo naye kwa sababu ya ufadhili wake wa vyama vya ukombozi bara la afrika. Lakini hawakuthubutu kutokeza hadharani maana alikuwa na nguvu kubwa ya hoja, nakumbuka alivyokuwa anawatukana Reagan na Magreth Thatcher kule kwao (sio kwa vyombo vya hapa, hapana kule London Washington, tena akiwaita FOOLS,).

Wakati mwingine namsikitikia jinsi alivyojitahidi. Kama mnakumbuka ujenzi wa reli ya TAZARA ulipigwa mikwara na kila mtu, lakini Nyerere alisisitiza umuhimu wake na rafiki zake wachina wakaijenga. Leo hii mchango wa reli hii hauonekani sana kutokana na barabara kuu kuwepo. Lakini wkati ule waulizeni watu wa Kilombero, Iringa, Mbeya wakusimulie.
 
20th Century and 21st Century. The reality in change or advancement of technology and management traits.

Management by Follow Up (MFU) and Management By Walk Around (MBWA).

That's all Folks.
 
The pictures cannot be compared. They are at very two different parables. They can't match at any cost!!!!
 
Hawa ni watu wawili tofauti na hawalinganishiki kivyovyote, ila tu ni wa Tanzania, labda hii ni ulinganifu wao na wote ni wana CCM. Kiutendaji tofauti ni mbingu na nchi. RIP JK Nyerere (Mwenye heri mtarajiwa)
 
duh huyu mchizi kwete bonge la msaniii na nyerere bonge la serious worker
jk was the leader bt jm is only the manager:

Ni kweli kipindi cha nyerere uchumi wetu ulikuwa juu kuliko hata wa US na ulaya ila alipoondoka ndo tu tukawa miongoni mwa nchi masikini kabisa, AIBU! Please write a sense things
 
mimi naona ungemlinganisha nyerere na hitler hebu angalia hizo picha hapo chini .
wote walikuwa madictator,moustache zimelingana .tafauti ni moja tu mmoja ni picture-Julius-Nyerere-Tanzania.jpg mweusi mmoja ni mtu mweupe.! adolf_hitler1244032948.jpg
nyerere was the most over rated president of all time .he done shit
 
Nakubaliana na yote , ila tuangalie na wakati/Nyakati , kipindi cha jk Nyerere mambo mengi yalikua yakifanyika kwa mikono (Labour Intensive) kwa sasa mambo mengi hufanyika kwa mashine .. (Industrial revulution) , kikubwa hapa ni kulinganisha sera na uchu wa madaraka ambayo ni mambo ya kumpima mzalendo... Nyerere alikaa madarakani kwa kipindi kirefu na kulitumbukiza Taifa katika umaskini wa kupindikia , Nani anakumbuka mwa 1984 mahindi ya Yanga??? , ila pia Nyerere amejitaidi kutuunganisha watanzania... Kikwete naye ana sera zake.. Miundombinu ambayo anaichukualia kama ni mishipa ya damu ktk mwili wa binadamu , ni sera nzuri ambayo italisaidia taifa kupigana na adui umaskini.
 
tofauti ni mchana na usiku,,,,,,i wonder if we have the ,,,,,,,,,,,of state
 
Unalinganishaje mtu mwenye afya na mgonjwa mwenye HI....
 
Ni kweli kipindi cha nyerere uchumi wetu ulikuwa juu kuliko hata wa US na ulaya ila alipoondoka ndo tu tukawa miongoni mwa nchi masikini kabisa, AIBU! Please write a sense things

Unafurahisha kweli wewe hehehe
 
afya nayo inahusika wanaogopa anaweza kuanguka degedege bure akijitia kufanya kazi ngumu
 
Huu ni uchokozi wa wazi! Kumbuka hawa ni watu wawili tofauti na wemeishi katika enzi na mazingira na 'background' tofauti. Haitakuwa sahihi kutaka mmoja awe 'copy' ya mwingine. Tafuta namna nyingine ya kuwalinganisha ndugu!
 
RIP Moses!Nyerere is like mount kilimanjaro and the other one is like ....................................................................
 
Kuna watu wanahangaika kweli usiku na mchana kushusha hadhi ya Nyerere wanashindwa

Wanajaribu kuokoteza kila aina ya kosa alilolifanya wakati yupo madarakani lakini wapi!

Wanajaribu kutoa ile hadhi ya baba wa taifa na kumwita jina la kawaida au mwalimu wakijitahidi wanaita mzee wetu lakini hawafanikiwi!

Mbaya zaidi wamekuwa wakimfananisha Nyerere na watawala walio shindwa Tanzania ,Afrika,na dunia kwa ujumla wakidhani kwa kufanya hivyo wanamdhalilisha na lkn watanzania wameshagundua upuuzi wao

Kwa maoni yangu kujaribu kumfananisha baba wa taifa na vibaka walioko madarakani sasa na waliopita si tu kwamba tunamdhalilisha Nyerere tunaidhalilisha hata Tanzania ambayo Nyerere alitoa kila alichonacho kuiendeleza,kuikuza na kuifanya ifahamike duniani kote kama moja ya taifa imara na lakuogopwa ulimwenguni

Inawezekana ni kweli alikuwa na mapungufu yake kama mwanadamu, lakini sisi tuliopo leo tumefanya nini cha kumkosoa na kutembea kifua mbele tukionyesha mapungufu yake?

Umefika muda tumwache baba wa taifa akastarehe kwa amani na sisi tukaendeleza pale alipofikia huku tukizifanyia kazi changamoto zinazotukabili.
 
Ni kweli kipindi cha
nyerere uchumi wetu ulikuwa juu kuliko hata wa US na ulaya ila
alipoondoka ndo tu tukawa miongoni mwa nchi masikini kabisa, AIBU!
Please write a sense things

Na ndo mana tulikuwa tunakula dona pia kununua chumvi tu mpaka upate kibali.
 
Tofauti zao ni nyerere ameacha watoto malofa,na huyu wa sasa amejifunza baada ya kuwaona kina makongoro walivyo choka.
 
Tafadhali linganisheni picha hizi hapa zikimuonesha JK Nyerere na JM Kikwete na kisha tathmini mwenyewe
Kaka kulinganganisha mlima na kichuguu, Tembo na Sisimizi ni sawa na kumlinganisha Dr. Slaa na Emmanuel Nchimbi.......Utakuwa hujamtendea haki. Siku nyingine jaribu kulinganisha Nyerere na wazee wenzake kama Mandera, Kwame Nkuruma, S. Toure na wengineo siyo Ze Commedy na majembe ya kweli. Anyway wenye macho huona wenyewe.
Magamba nayaheshimu siyaogopi!!!!!!!
 
Rest in peace baba wa taifa. Hakuna wa kufananishwa na ww. Ulikuwa jembe. Tutakukumbuka daima
 
Mwalimu alikuwa ni mtu wa kazi zaidi tena kwa mifano.Nimeipenda ile picha mwalimu anapobeba toroi la concrete ,daah sidhani kama nchi hii kama tutakuja kumpata kiongozi shupavu na mwenye moyo wa uzalendo kama mwalimu jk.
huyu wa sasa urembo mwingi yaani kupanda mti mpaka kutandikiwa mkeka?daaaaah any way ndo hivo tu hakuna namna nyingine.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom