Linganisha-form four exam results

adobe

JF-Expert Member
May 6, 2009
2,776
1,877
Jamani matokeo ndo hayo,subirieni malalamiko_Ooh Ndelichako anapendelea.Hapo napo je?
 
mtaala ubadilishwe.....somo la elimu akhera liwekwe uone kama hawajafaulu wote!
 
mtaala ubadilishwe.....somo la elimu akhera liwekwe uone kama hawajafaulu wote!

Elimu ahera sio rahisi hivyo, kuna vichwa vya kiislamu vilikuwa Azania enzi hizo, vilikuwa na A's saba na kwenda juu, walikuwa wanasema mitihani ya dini inatungwa migumu mno halafu sylabus wanayo NECTA wenyewe hivyo unakuwa haujui hata usome wapi.
 
Jamani matokeo ndo hayo,subirieni malalamiko_Ooh Ndelichako anapendelea.Hapo napo je?

Mkuu mbona matokeo ni kichefuchefu. Habari zionaonyesha kwamba 60% wa watahiniwa wamepata daraja la sifuri (Division zero)!
 
Fimbo nzuri sana hii kwa Serikali isiyo sikivu,nchi hii haijawahi kuwa na matokeo mabaya kiasi hiki na hii inaonesha kuwa Walimu waliamua kuichapa bakora Serikali baada ya kupuuza madai yao.
Kwa mwendo huu hatutafika popote na tunatengeneza Taifa la vilaza ambao hawatakuwa na uwezo wa kuhimili ushindani katika maendeleo tunayotarajia kuwa nayo hapo baadae.
 
Afu Ndalichako amewapa haki yao bila kuwaangalia usoni hao waliojidai hawamtaki. Leo waje tena na story mpya
 
Mkuu Adobe

Acha kutumia computer ya NSSF HQ kupost JF jamaa wanaweza kukutafuta au edit docs before post
 
Mkuu mbona matokeo ni kichefuchefu. Habari zionaonyesha kwamba 60% wa watahiniwa wamepata daraja la sifuri (Division zero)!

60% ambao wamfikia level ya form 4, kusingekua na shule za kata hao 60% wote mngewata wameishia elimu ya msingi???

Muwe wepesi wakufikiri
 
Wakuu hata Islamic knowledge kwa haraka haraka...maksi za juu ni C. Elimu ni elimu tu....hata ya Imani inatakiwa mtu mwenye uwezo. Mimi nafikiri sasa tatizo linakuwa kubwa zaidi...unapojenga mazingira ya kutaka kusaidiwa badala ya kujisaidia mambo ndi yanakuwa hivi....Ndugu zangu wa Imani zote..tukae chini...tutafakari na kuchukua hatua...tatizo liko mahali fulani...mbona tunalifumbia macho?..........Tuseme kweli na kweli ituweke huru...tatizo ni CCM
 
60% ambao wamfikia level ya form 4, kusingekua na shule za kata hao 60% wote mngewata wameishia elimu ya msingi???

Muwe wepesi wakufikiri

Mkuu wangu hiyo 60% ambao wamefika form four lakini hawajui kusoma na kuandika kuna tofauti gani na ambaye hata hakufika darasa la kwanza? Si afadhali angefika la saba kisha akaenda chuo cha ufundi wa kupaka rangi.
 
Mkuu wangu hiyo 60% ambao wamefika form four lakini hawajui kusoma na kuandika kuna tofauti gani na ambaye hata hakufika darasa la kwanza? Si afadhali angefika la saba kisha akaenda chuo cha ufundi wa kupaka rangi.
Div 0 = Kutojua kusoma na kuandika?!!!! my world Hao waliofika form 4 si ndio hayo wanao wapeleka puta wanasiasa vilaza huko majimboni? miaka minne ya kuwepo shule kunakujengea ufhamu kuliko hao amabao hawakufika kwenye hizo shule kabisa
 
Duh!haya matokeo hadi yanatia kinyaaa kuyangalia.Watu wamepata mshituko sana kwa ha ya matokeo na kuanza kujiuliza tatizo ni nini?wengi wameenda moja kwa moja kwa kutaja tatizo ni upungufu wa walimu na vifaa.
Lakini mimi naona pamoja na hayo kuna matatizo mengine.kwa sababu shule la private zina walimu na vifaa vya kutosha lakini nako hali ni mbaya pia kuna shule za serikali zinavifaa vya kutosha na zimepewa majina ya shule za wanafunzi wenye vipaji maalum lakini nako mambo mabaya.
Hicho ndicho kinafanya niwe na mawazo tofauti kutokana na matokeo mabaya ya mtihani wa kidato cha nne.
1.Je,mitaala ya elimu inakizi mahitaji ya walimu na wanafunzi?
Hapa unaweza ukaangalia na kujiuliza tuna mitaala ya elimu je inawaweze wanafunzi kuendana mazingira ya sasa.kwamba inawawesha wanafunzi kusoma ili wajikomboe yaanii elimu yao iwasaidie kufanya kazi popote na si kutegemea ajira toka serikalini!?.Pia mitaala hii walimu wanaifahamu?utashangaa mwalimu yuko kazini muda mtaala unabadilishwa mwalimu hajapewa elimu yeyote kuhusiana na huo mtaala unategemea nini?Ningeomba hili jambo lifanyiwe uchunguzi.
2.Walimu tulionao ni walimu kutoa elimu kwa wanafunzi,au ni jina tu ni walimu.??hapa napo paangaliwe kuna baadhi ya walimu watu hawana wito wa kuwa walimu na kazi ya ualimu ni wito.Utakuta walimu wengi wamekimbilia ualimu ili tu wapate ajira na si walimu wenye moyo wa dhati wa kutoa elimu bora hao wanaitwa walimu mshahara.Ukimkuta darasani anafundisha unawaweza kutoa machozi hakuna anachofundisha wanafunzi wakaelewa zaidi ya kuwapigia kelele watoto na kuwapotasha kabisa mwanafunzi akimwambia mwalimu hapo sio.Atamtukana na kumwambie utabishana na mwalimu wewe!!!!!!duh kwa staili hiyo unategemea nini?Au mheshimiwa mwalimu anaingia darasani kanywa pombe kupindukia au katoka kuvuta bangi unategemea atafundisha nini?Kingine cha kuchekesha mwalimu ana Shahada ya elimu hajui hata jinsi ya kuandaa andalio la somo na Azimio.Lazima huko jikoni wanakopigwa walimu kuangaliwe vizuri.maana hawa hawa walifanya vibaya mwaka huu ndio mwakani utawakuta wako mashuleni wanafundisha.Hapo lazima tu wanafunzi waambulie patupu.
3.Mazingira wanaishi walimu yanaridhisha?Mwalimu anakaa nyumba ya kupanga tena kwa gharama kubwa na aliko panga ni mbali na shule unategemea mwalimu kama huyo atafanyeji?kwanza atakuwa na uchovu kabla hajaanza kufundisha nyumbani nako kuliko inashindikana hata kuweza kuanda mada yakwenda kufundisha somo husika.nini kinafuata hapo?Ni zima moto na bra bra za kutosha.Hapa utaishangaa hii nchi yetu imekuwa nchi yakujipendekeza kwa wageni(wahindi) na matajili.kwa nini nasema hivyo kuna shirika la nyumba la taifa kuna nyumba nyingi sana wamejenga na ni bei chee sana kwa kodi yake ya nyumba.Cha kushangaza zimekuwa za wahindi na watu wenye nazo.Wakati mwalimu anahangaika kukaa kwenye nyumba duni!!!!je mwalimu anashindwa kulipa elfu 30000/=per month.kwanini wafanyakazi wa serikali wasipangishwe,tuna POLISI,Tuna WANAJESHI,Tuna mabwana shamba.kwa nini wasipewe hizi nyumba?
4.Motisha.walimu hawana motisha.
5.Je,wanafunzi wako tayari kupa elimu?Hili nalo ni swali ambalo linatakiwa kuangaliwa vizuri na kupata ufumbuzi.mwanafunzi anaenda shule bila daftali anachukua mpira na vitabu vya hadithi na mapenzi.unategemea nini?mwanafunzi haendi shule unategemea nini?
6.jamii iko tayari watoto wao wasome na wanafanya nini ili watoto wao wasome?Huko nako kuna tatizo mzazi tokea mtoto wake afungue shule hajawahi kukagua madaftali wala report ya mwanae.je,huyu mzazi yuko tayari kweli mwanae asome?Au mzazi mwanae akichapwa fimbo hata moja bila hata kuangalia kosa nini huyo mbio shuleni na panga mkononi na kuanza kumtukana mwalimu hivi utafikiri mwalimu atakuwa na Ari ya kufundisha tena.
Mwisho serikali ipo kweli?kama ipo kwanini haya yapo ndo kusema hawayaoni.?Au ndio hiyo mtu anasoma makaratasi tu bila kujua hali halisi ilivyo?Duh!Hii ndio Tanzania bwana!!!!!!!!!!!!!
 
Div 0 = Kutojua kusoma na kuandika?!!!! my world Hao waliofika form 4 si ndio hayo wanao wapeleka puta wanasiasa vilaza huko majimboni? miaka minne ya kuwepo shule kunakujengea ufhamu kuliko hao amabao hawakufika kwenye hizo shule kabisa

Hakuna ufahamu wowote hapo! Division zero haina ufahamu wowote zaidi ya shida tu na kupoteza muda
 
60% ambao wamfikia level ya form 4, kusingekua na shule za kata hao 60% wote mngewata wameishia elimu ya msingi???

Muwe wepesi wakufikiri

Sasa kuna maana gani kufika form four alafu cheti hupati?
 
Back
Top Bottom