Lindi yetu na Sri Lanka

Mambo ambayo mleta mada(ambaye ni kiongozi) ameyaorodhesha kama ndiyo kikwazo,lakini kwa namna ambayo ni kama hana uhakika kwasababu ameyaorodhesha kama maswali.Nilitegemea hoja yake hii ingekuwa walau na mapendekezo mawili matatu given the fact that he's a leader.

Kama alivyofanya kwenye kutolea mfano wa ufisadi wa mbolea,ameuliza maswali,tena kuna hilo ambalo rafiki yake JK kalisema kuwa "watu hawapendi kuona maendeleo",nadhani akimaanisha wapinzani.Hilo la Zitto sijui kama alizungumzia individually ama as a society(kwamba hatupendi kuona maendeleo).Kwa namna nyingine,ni kama haamini moja kwa moja kuwa ufisadi ndo tatizo kuu.

Pamoja na kwamba ni kweli ufisadi unaweza kuwa pia ni tatizo la kimfumo,lakini hajatoa mapendekezo ama solutions.Makala hiyo ni nzuri tu lakini siyo yenye kuprovide solutions.Mleta hoja ametolea mifano ya mambo yanaoonyesha usawa ama mfanano kati ya mkoa/mikoa yetu wa/ya Lindi/mtwara vs Taifa la Sir Lanka,bila kuona kuwa mipango yetu kwa Lindi ni ya kimkoa na ile ya Sir Lanka ni ya kitaifa.Inawezekana kabisa kwamba Lindi ingekuwa Taifa basi lingekuwa mbali sana.

Sisi tatizo letu kubwa ni uongozi hilo siyo siri hata kidogo.Ni hatuwa walizozichukuwa viongozi wa mataifa hayo ndizo zilizowafikisha hapo walipo.Viongozi kulalamikia wananchi ndo tatizo lenyewe.Tunategemea solutions kutoka kwa viongozi na si malalamishi.Kiongozi akilalamika wananchi nao wafanyaje?Kiongozi asipokuwa na solution ya nini cha kuwafanyia wananchi,wananchi wanatakiwa wafanyeje?

We lack leadership,thats the fact,ngoja tusubiri kama kiongozi wetu atatoa na ushauri wa nini kifanyike,yeye si mmojawapo wa watunga sheria?Mbona China wananyonga mafisadi na ni ushahidi tosha kabisa kwamba hilo limesaidia taifa hilo kusonga mbele?

Kwanini asiseme yeye kama kiongozi,tufanye so and so kuutokomeza ufisadi kama ni kweli anaamini kuwa ni kikwazo cha maendeleo yetu?

kwa jinsi nilivyoona kiongozi kakataa utamaduni katumia mfumo.Ila huo mfumo ni wa siku nyingi sana na ni wa kitaifa ,kwa kihalisia ni utamaduni.Utamaduni si lazima uwe km DNA.kama anakubali ufisadi na wizi upo kila kijiji,na kila office na ni tabia iliyooota mizizi mikubwa there is no way mheshimiwa akataka usiitwe utamaduni.mwovu hafukuzwi na kushitakiwa bali huamishwa kituo.
 
Hiyo hapo chini ni quote kutoka kwenye ile thread ya "Maisha ya rais wa Iran",labda tu tuondoe hapo kwenye "shall remain poor",labda akimaanisha kumaliza uongozi ama utumishi wa umma bila kuitumia nafasi hiyo kujitayarisha.Hizo ni hatua za kiongozi makini,tena wa taifa lenye utajiri mkubwa wa mafuta na maendeleo wanayo.Lakini bado wanatambuwa umuhimu wa viongozi kutokujitajirisha kwa kutumia utumishi wa wa umma na kulifisadi taifa!Sasa hilo tu linaonyesha utofauti wa viongozi wetu.Tatizo la ufisadi inajulikana kila pahala kuwa ndo lenye kudumaza maendeleo.Lakini sisi wapi?
Under his authority whenever he appoints any minister to his post he gets a signed
document from him with many points particularly highlighting that he shall remain poor
and that his personal and his relatives accounts will be watched and the day he leaves
the ministry shall be with dignity, and therefore it is not lawful for him or his relatives to
take any advantage of his office. First of all he declared himself for all the 'Big' wealth
and the property he owned was a Peugeot 504 car, Model 1977, an old small house
inherited from his father 40-years ago in one of the poorest zones in Tehran . His
accounts with a zero balance and the only money comes in to his a/c was from his
salary from the university as a lecturer with an amount of US$ 250 only.
 
Chini ya uongozi wa? Tatizo la Watanzania hawajui kuwa huwezi kutarajia kuvuna maembe kutoka kwenye mvule! Mvule hauna matunda jamani. Na kama kwa miaka 50+ tumeambulia hapa tulipo, basi hiyo hamsini mingine haitakuwa tofauti. Dalili ya mauti ni Ukimwi!

Siyo rahisi kuendelea katika mfumo huu tulio nao.ufisadi ni mkubwa kupindukia.TANZANIA ni nchi ya kwanza afrika kupata misaada lakini fedha hizo zimishia kujenga barabara mbovu na zisizo na kiwango.dawa ni kupiga chini ccm leta CHADEMA.
 
Mipango ya Maendeleo ya ujumla ni utopia zaidi inafaaa sana siasa za kutowajibika kama za Tanzania na ndio maana hatuwezi kuendelea hata kidogo.

Ili tuendelee lazima tutumie competitive advantage ya kila mkoa. Mtoa mada well done Challenge kwao watu wa Magogoni JK et al msiogope kudhutubutu kufanya vitu nje ya mazoe yenu.
 
kwa vile mke wa jk anatoka lindi basi kila kitu lindi..i miss nyerere,hakupendelea butiama kama bagamoyo inavyopendelewa sasa hivi..
 
Mfuate aliko,mtoa mada ametolea mfano mkoa Lindi na jinsi unavyoweza kundokana na umaskini sasa mke wa rais anakuja vipi hapa?
 
Mdogo wangu Zitto Zuberi Kabwe, huwa ninapenda sana tafiti zako na the they way ambavyo huwa una apply kile ulicho tafiti, hakika wewe ni moja kati ya hazina kubwa katika nchi hii hasa katika eneo la uchumi, napataga sana shida ninapo mwona na kumsikiliza Mwigule Mchemba hasa siku ile mlipo kuwa na interview pamoja pale TBC, wewe ndo hakika Waziri wa Fedha wa nchi hii, pengine wengine wamesahau, wewe ndo mwasisi wa chanzo cha fedha za kuendesha hivi Vyuo vya VETA (rejea bajeti ya upinzani mwaka jana). Tunao watu ndani ya magamba wamesoma masomo ya uchumi kama wewe, tena wengine wanadai walifauru vizuri kulioko wewe, lakini ukweli hatuoni interpretation ya kile walicho jifunza katika utendaji wao, Aibu kubwa.

Mwaka jana uliwahi kuja na issue ya Mkonge Tanga, tena kupitia Channel 10 nilikusikia umeisha fanya utafiti hadi wa soko kwani ulijua kabisa matumizi mapya ya Mkonge duniani, ulipoliweka suala hilo Bungeni,Mmmm, hata Wabunge wa mkoa wa Tanga nao wakakuijia juu,AIBU kubwa, sitashangaa sana mwaka 2015 wakazi wa Tanga tena wakawarudisha Wabunge wale wale tena (shida ya dini nayo ni tatizo kubwa sana kwa wapiga kura wa mikoa ya Pwani, huu utafiti wangu binafsi, sio taasisis yeyote), umezungumza sana issue ya gas, nani akusikilize? Wenzio wameng'ang'ania eti we unatoka chama cha upinzani, tumekuwa tuna mjaji mtu na sio alicho kisema, AIBU kubwa mno katika nchi yetu.

Nini kaka cha kufanya, ukweli haya yote hata na hakika unayo mengine mengi mno ya maendeleo au solution za kuikomboa nvhi hi katika lindi kubwa la umasikini, ndani ya chama hiki kinachaofaidika na umasikini wa Watanzania yaani ccm, sioni kama itawezekana, umasikini wa Watanzania, ccm inafaika nao sana tu, nimeona ulicho kifanya kule kwenu Kalinzi, Mkabogo, Matizyazo, hakika dogo umeboresha sana maisha ya watu wa kule kwa kilimo cha Kahawa tu, baadhi ya vijana wenyeji wa huko sasa hivi wamerudi huko na kukomaa na kilimo cha Kahawa, sababu, kina lipa sasa hivi, utasikia magamba wako busy eti kukomboa jimbo hilo, wao muhimu kwao ni kutawala na sio kuondoa umasikini, AIBU kubwa, kumbe tukiwa na Viongozi wa type yako inawezekana kabisa kupingana na matusi tuliowahi kutukanwa na akina Peter Botha, mimi narudia, shida kubwa ya nchi hii if not nchi zetu hizi za Kiafrika, sio Elimu, tunao wasomi wengi mno wazuri tu, shida yetu kubwa ni kutafsiri kile mtu alicho soma shule katika vitendo tu basi, issue sio Elimu kabisa, nakataa, hiyo ilikuwa sababu kwa miaka ya 70 na 80 na kidogo mika ya 90 mwanzoni but sio karne hii ya 21. Hima Watanzania, tushirikiane kuitokomeza ccm, ndio chanzo cha umasikini wetu, hakuna kingine!
 
mheshimiwa si yupo aifanya hii thread more interactive kwa kujibu na kutoa maoni yake.
 
Nimeona na kusoma nchi nyingi za Asia raia wake wanajali sana utaifa kuliko ubinafsi, ndo maana nchi nyingi sana za Asia ambazo zote zilikuwa maskini sana wakati wa ww2 zilipopata mwanya kidogo tu zimepiga hatua za ajabu.
kuna kipindi nilisoma Post-War Japanese economy, wale wenzetu walifanikiwa kutoka kwa sababu ya uzalendo wa raia wao wakiongozwa na viongozi wao. walikuwa wanapelekwa nje ya nchi kusoma, walihakikisha wanasoma kwa manufaa ya taifa, wanarudi nyumbani na kuendeleza................ na strategies hizo hizo ndo zinatumiwa na mataifa mengine ya Asia.
sasa sisi, raia wabinafsi, wengi wetu wa SSA tukipata mwanya wa kukimbia nchi zetu wala hatujiulizi mara 2. mtu anaenda kusoma nje, anasoma hadi PhD anaona bora abaki huko huko aendeshe taxi kuliko kurudi nyumbani kusaidia hata kufundisha sekondari. mtu anawaza tumbo lake na jamaa zake, siyo taifa. tukija kwa viongozi wetu ndo yaani najisikia kulia tu, kila likitoka bomu moja linaingia jingine. kwa mtindo huu tusahau kabisa kukutana na wenzetu, tutaishia kwenda kujifunza kila siku na hatu-graduate.[/QUOTE ]Nchi nyingi za Asia na Mashariki ya mbali wanatumia mfumo wa serikali za majimbo, mfumo huu unawapa wananchi kuwa karibu zaidi na viongozi wao katika kupanga na kusimamia rasilimali za jimbo husika. kwa utaratibu huo maendeleo ya jimbo moja huleta impact kwa taifa. Vilevile mfumo wa majimbo huleta ushindani maendeleo wa jimbo moja na jingine. Mfumo tulionao sio rahisi kuendelea kwa kuwa kila kitu kinaamuliwa na wakubwa walioko Dar. Chukua mfano kulikuwa na maana gani kuagiza kila halmashauri ya wilaya kununua power tiller, je serikali yetu inaama kila mtanzania ni mkulima ? na kila halmashauri inaradhi bora ya kilimo cha kununua power tiller ?
 
Nchi nyingi za Asia na Mashariki ya mbali wanatumia mfumo wa serikali za majimbo, mfumo huu unawapa wananchi kuwa karibu zaidi na viongozi wao katika kupanga na kusimamia rasilimali za jimbo husika. kwa utaratibu huo maendeleo ya jimbo moja huleta impact kwa taifa. Vilevile mfumo wa majimbo huleta ushindani maendeleo wa jimbo moja na jingine. Mfumo tulionao sio rahisi kuendelea kwa kuwa kila kitu kinaamuliwa na wakubwa walioko Dar. Chukua mfano kulikuwa na maana gani kuagiza kila halmashauri ya wilaya kununua power tiller, je serikali yetu inaama kila mtanzania ni mkulima ? na kila halmashauri inaradhi bora ya kilimo cha kununua power tiller ?
 
Nchi nyingi za Asia na Mashariki ya mbali zinatumia mfumo wa serikali za majimbo, iwapo Tanzania tunataka kusongo mbele hatuna budi kuliweka jambo hili katika katiba. Mfumo wa majimbo unaweka wananchi karibu na viongozi wao na hivyo kupanga na kusimamia maendeleo kwa ukaribu zaidi. sisi mipango yetu imekuwa ni ya kitaifa bila kuangalia priorities za mikao. matokeo yake ni kuwa maamuzi yote hutolewa na viongozi wakuu wa kitaifa huku wa ngazi ya chini wakiwa ni watekelezaji tu. Majimbo yataleta umoja wa kitaifa na pia ushindani wa maendeleo kulingana na rasilimali zinazopatikana katika maeneo husika. Jiulieze kulikuwa na maana gani kuagiza kila halmashauri ya wilaya kununua power tiller ?, je inamaana kila mtanzania ni mkulima na je kila halmashauri ina ardhi inayofaa kwa kilimo cha power tiller, hii ni moja ya mipngo yetu mibovu ya kilimo. Katiba mpya tuweke mfumo wa mikoa au majimbo kuwa semi automous kwa maana viongozi wachanguliwe kwa kula za wananchi na wawe na mamlaka kamili ya kusimamia maendeleo
 
Yeah, I was there in SL in 2008 wakati huo vita vikiwa vimekolea sana, nakumbuka nilikatazwa kusafiri beyond mji mmoja unaitwa Kandy kuelekea Kaskazini. Kuhusu hiyo kama sh. 45,000 wanayopata madereva wa bajaj kwa siku, pengine ni chache sana kwani kule bajaj ndio taxi, na hata wenyewe wanaziita taxi na si rahisi kupata salon car for hire as a taxi, so ukitaka kulinganisha basi angalia dereva taxi wa Bongo anapata sh. ngapi kwa siku.

Wanaweza kusifiwa kwa kujikwamua kiuchumi kwa kasi, lakini kisiasa rais wao amefanya ubabe sana kwenye uchaguzi kwa kumnyanyasa mpinzani wake ambaye ndiye jenerali aliyeongoza vikosi kuwatimua Liberaration Tigers of Tamil Eelam aka Tamil Tigers. Tuige mfano wao kiuchumi, lakini nao waboreshe demokrasia! Nadhani watakuwa wameongeza viwanda, lakini hiyo 2008 walikuwa wanaimport sana kutoka India
 
Wakuu kumbe lindi nayo ina gesi nyingi hasa kilwa?

Lindi yaweza kuwa Sri Lanka ya Tanzania|Zitto Kabwe, Mb

Watanzania wengi tukisikiajina Sri Lanka jambo kubwa linalotujia kwa haraka ni ama Chai au Vita ya TamilTigers. Nakumbuka tulipokuwa darasa la sita Shule ya Msingi tulisoma ‘Chai SriLanka’ na kusoma miji kama Kolombo, Batikaloa na Trinkomalee (Colombo,Batticaloa, Trincomalee). Lakini tulipashwa sana habari kuhusu vita vya wenyewekwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka takribani thelathini. Juzi nilikuwa SriLanka. Vita imekwisha mwaka majuzi 2009. Chai ipo nyingi sana. Mwaka 2010 SriLanka iliuza nje jumla ya tani 314,000za chai yenye thamani ya dola za kimarekani 1.37 bilioni na hivyo kuongozaduniani kimapato ingawa Kenya ilisafirisha chai nyingi zaidi, tani 441,000.Hata hivyo kutokana na ubora wa zao hilo kuwa chini kidogo Kenya ilipata dolaza kimarekani 800 milioni tu. Mwaka huo Tanzania, yenye eneo kubwa zaidi lakulima nchi zote hizo iliuza nje tani 34,000 tu na kupata dola za kimarekani 61milioni hivi. Licha ya kwamba Tanzania ni nchi ya nne kwa kuzalisha Chai Afrikabaada ya Malawi, Uganda na Kenya, bado inaweza kuwa katika nafasi ya juuduniani iwapo tukiamua kuwa makini katika mambo tufanyayo na kupenda kufanyamambo makubwa.

Siku hizi napenda sanakujua historia za nchi katika kupambana na umasikini wa watu wao. Lengo nikuelewa juhudi za nchi mbalimbali katika kuleta maendeleo ya watu na kujifunzapale ambapo nchi zimefanikiwa. Ukitembea mitaa ya Jiji la Colombo unaona mjimzuri msafi uliopangwa vema na kila mtu anaonekana kushughulika. Njia nzuri yakujua ukweli wa maisha ya watu ni kuongea na watu wenyewe. Mara nyingi hutumiamadereva wa taxi au Bajaji kwa jiji kama la Colombo. Katika mazungumzo nabaadhi ya madereva wa Bajaji nilizokuwa natumia pale Colombo niliona mwelekeommoja wa. Kwamba katika kipindi cha miaka 10 iliyopita maisha yao yamebadilikasana. Wakisifia kuisha kwa vita dhidi ya Tamil Tigers na kuongezeka kwa mapatoyao kwa watu kutumia zaidi usafiri. Dereva wa Bajaji wa Jiji la Colomboanaingiza wastani wa rupia 4000 (shilingi45,000) kwa siku. Nikataka kujua nini kimepelekea mabadiliko haya ya kipatoambacho mpaka wenye Bajaji wanafaidika nayo. Takwimu zao zinaeleza mengi sana.Serikali iliamua kupambana na umasikini na hasa umasikini wa vijijini.

Mwaka 2002 asilimia 22.7ya wananchi wote wa Sri Lanka walikuwa wanaishi chini ya mstari wa umasikini.Ilipofika mwaka 2011 kiwango cha umasikini kilikuwa asilimia 6 tu. Umasikiniulishuka kwa kiwango kikubwa katika maeneo ya vijijini. Katika kipindi chamiaka mitatu kati ya mwaka 2007 mpaka 2010 umasikini wa wananchi wa Sri Lankawalio kwenye sekta ya Chai (Estate sector) ulishuka kutoka asilimia 32 yawaliokuwa wanaishi chini ya mstari wa umasikini mpaka asilimia 11.4 na wale wa vijijini nje ya sekta ya Chai umasikiniulishuka kutoka asilimia 24.7 mpaka asilimia 9.4 katika kipindi hicho. Nilipoulizazaidi kwa wanasiasa na viongozi wa Serikali nikaambiwa kuwa mabadiliko makubwayaliyotokea miaka ya karibuni yalitokana na Serikali kufanya maamuzi mahususiya kuelekeza fedha nyingi zilizokuwa zinakwenda vitani kwenye uwekezajivijijini. Wanasema walitumia fedha nyingi kwenye ruzuku ya mbolea kwa wakulima,kusambaza umeme vijijini na kujenga barabara za vijijini. Siku niliyofikaniliona kwenye moja ya magazeti yao lakila siku Rais wao akizindua Mtambo wa kuzalisha umeme katika mji waTrincomalee uliopo Mashariki ya nchi hiyo.

Nikajiuliza mbona na sisitunatekeleza MKUKUTA na tunasema kwamba tunawekeza fedha nyingi sana vijijini?Mbona na sisi tunatoa ruzuku ya Mbolea yenye thamani ya zaidi ya shilingibilioni 60 kwa mwaka? Inakuwaje wenzetu wafanikiwe sisi tusifanikiwe? Tanzaniaimeanza kutoa mbolea ya ruzuku katika msimu wa mwaka 2006/2007 kama ilivyo kwaSri Lanka. Wenzetu katika miaka 3 kiwango cha umasikini kimepungua kwa asilimia15 kwa wananchi walio katika sekta hiyo ya Kilimo na wanaoishi vijijini. Sisikatika kipindi cha muongo mmoja, 2001 mpaka 2011, umasikini umepungua kwaasilimia mbili tu. Moja ya sababu ya sisi kushindwa ni kwamba mfumo wa mboleaya ruzuku umegubikwa na ufisadi wa hali ya juu sana. Mfumo huu umedhihirishanamna ambavyo kazi ya kupambana na Ufisadi ni ya kimfumo zaidi maana kwa namnaviongozi wa vijiji wanavyoiba mbolea ya ruzuku unaweza kiurahisi kabisa kusemarushwa ni sehemu ya utamaduni wa Mtanzania. Siamini hivyo. Ninaamini kwambamfumo wetu unazalisha wala rushwa, walafi na watawala wenye tamaa nawasiotosheka kama nilivyoeleza katika makala zangu zilizotangulia. Je tukiondoaufisadi wa mbolea ya ruzuku tunaweza kupata mafanikio ambayo wenzetu wameyapata?Sina jibu wala jawabu la swali hili. Hata hivyo ninaamini kwamba kutofanikiwakwetu ni zaidi ya ufisadi. Ni kutofanya kazi kwa bidii? Ni kukosa umakini? Nikutofurahia mafanikio? Ni kukosa uongozi thabiti unaoweza kusimamia mchakato wamaendeleo kuanzia ngazi ya kijiji mpaka Taifa?

Hebu tutazame pamojatakwimu hizi. Sri Lanka ina ukubwa wa kilometa za mraba 65,000. Mkoa wa Lindiuna ukubwa wa kilometa za mraba 66,000. Sri Lanka ina Pato la Taifa la dola zakimarekani 60 bilioni mwaka 2011, Tanzania Pato lake la Taifa ni dola zakimarekani 24 bilioni. Sri Lanka ina jumla ya watu milioni 20, Tanzania inajumla ya watu milioni 45, Mkoa wa Lindi una jumla ya watu 750,000 hivi. SriLanka na Tanzania zote zina Bajeti ya dola za kimarekani bilioni Tisa hivi.Uchumi wa Sri Lanka unategemea sana zao la Chai na Utalii kwa fedha za kigeni.Mkoa wa Lindi una eneo kubwa zaidi la Kilimo kuliko Sri Lanka nzima hasaukizingatia katika hekta 5.2m zinazofaa kwa Kilimo ni hekta 500,000 tu ndiozinalimwa. Zao la Korosho laweza kuwa Chai ya Lindi. Kilometa za mraba 18,000za mkoa wa Lindi ni Selous Game Reserve, Kilwa ni kivutio tosha cha utalii wakila namna na Mkoa wa Lindi una fukwe ambazo hazijawahi kuguswa toka duniaiundwe na mola.

Sri Lanka hawana GesiAsilia. Lindi na hasa Wilaya ya Kilwa ndio mzalishaji mkubwa wa Gesi asiliahapa nchini. Pia sehemu kubwa ya Gesi iliyogunduliwa hapa nchini ipo katikamkoa wa Lindi inagwa wengi wetu hudhani kwamba ipo mkoa wa Mtwara. Lakini Lindina Mtwara sawa tu. Mtwara ina kilometa za mraba 16,000 (chini ya eneo la Lindilililopo Selous). Tufanye Lindi na Mtwara kwa pamoja ndio Sri Lanka yaTanzania. Tunaweza kujenga uchumi wa dola za kimarekani bilioni 60 kwa Lindi naMtwara? Tunaweza kufanya mikoa hii iwe na kiwango cha umasikini chini yaasilimia 3 ya wananchi wake? Tunaweza kuingiza watalii 800,000 kwa mwaka kwamikoa hii tu? Tunaweza kuuza nje Korosho yenye thamani ya dola za kimarekaniangalau 600 milioni? Tunaweza kutumia sehemu ya Mapato yatokanayo na Gesi asilikujenga miundombinu ya barabara, umeme, reli na maji kwenye wilaya zote za hiiSri Lanka yetu? Tunaweza kuwekeza kwenye Elimu kuhakikisha kila motto anapataelimu bora? Tunaweza kuhakikisha kuwa asilimia 97 ya wakazi hii Sri Lanka yetuwanapata huduma za Afya?

Majibu ya maswali yotehaya ni NDIO. Utashi. Utayari. Uthubutu. Hebu tuthubutu kuiweka Sri LankaTanzania. Lindi na Mtwara ni zaidi ya Sri Lanka. Nikipata fursa ya kuandikatena nitaandika kuhusu uwekezaji kwenye Elimu nchini Sri Lanka na kwamba Hakiya kupata Elimu mpaka Chuo Kikuu ni haki ya kikatiba yenye kuweza kudaiwamahakamani.
 
Back
Top Bottom