Lindi wamjia juu mbunge wao kwa kuishi Dar

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,308
Mbunge wa Lindi Mjini, Salum Barwani (CUF) amewekwa kiti moto na baadhi ya wapiga kura aliokutana nao wakimtuhumu kukaa muda mrefu Dar es Salaam bila kwenda kuwaona. Pia Baraza la Utendaji la Wilaya la CUF lilimwita na kumweka kikao Jumamosi iliyopita na kumhoji sababu za kutumia muda mwingi Dar es Salaam na kutokwenda kuona wananchi baada ya Bunge la Bajeti. Kamati hiyo ilitaka kujua uhalali wa kukaa muda mrefu nje ya jimbo kwa kuwa vikao vya Bunge kwa mwaka hufanyika mara nne tu.

Katika kikao hicho, Barwani alijitetea kuwa licha ya vikao vya Bunge alivyokuwa akihudhuria Dar es Salaam, bado kuna kazi zingine za ufuatiliaji wa ahadi za Serikali kwenye ofisi za idara na wizara, baada ya kukamilika kwa vikao vya Bunge. Barwani aliendelea kujitetea kuwa yeye bado anasoma utendaji wa kazi za Bunge kwa hiyo anapaswa kufahamu zaidi kwa kuwa bungeni.

Mbunge wa CUF pia aliwashangaza baadhi wa watu pale aliposema kuwa anatekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010/15 kwa kuwa chama chake hakikushinda uchaguzi mkuu wa urais.
 
Aah huyo naye yupo ushahidi tu kama mbunge,vipi na Kafumu ameshakanyaga jimboni kwake tangu achaguliwe?
 
Hawa si ndiyo tunao wasema ni kawaida yao kuhama majimbo na wananchi walimjua wasilaumu wavumilie tu
 
Huku kwetu Mabwe Pande mbunge wetu Mdee tulimuona wakati wa kampeni tu na sasa ni mwaka umepita.
 
Huku kwetu Mabwe Pande mbunge wetu Mdee tulimuona wakati wa kampeni tu na sasa ni mwaka umepita.

we mbopo ni mjinga sana kwa sabaubu gani, mdee aliitisha mkutano wa wananchi hamkutokeza, kisa mlihongwa na ccm msihudhurie ili aonekane hapendwi njaa zitawamaliza
 
Back
Top Bottom