Ligi kuu ya Tanzania na maendeleo yake

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671
kila siku nikifungua katika sehemu hii nipate kujua msimamo wa ligi yetu ya tanzania sioni thread inayozungumzia.

utaona mambo ya ligi za ulaya na hasa uingereza

naomba tutumie thread hii kuhabarishana habari ya ligi yetu

kwa kuanzia Maji maji na Azam matokeo ni ( Maji x 2)1 - (Azam) 0
 
Mbona website ya Azam inaonyesha mechi hii(tarehe 2/9/2010) Azam 1 Maji Maji 0?, Matokeo hayo hapo juu umeyatoa wapi?
Ligi ilisimama kupisha michuano ya Kimataifa.
 
Mkuu ligi inaendelea vizuri tu,ila tatizo inatawaliwa sana na vimbwanga ambavyo hata kujadili ni udhia mtupu:- Mara maiti imeibwa mortuary ili kulogea mechi,...ooo mara waganga 30 wamekwenda kuloga mechi Mwanza ..... sijui Ulimboka kaenda kumlipa deni Kado wakati kuna mechi inamkabili mbele na wadau kuhusisha na hongo,.... mara nyimbo za Taifa zimegoma kwenye cd.....blabla .... ooo Kaijage kasimamishwa kazi kumbe mkataba ulikwisha siku nyingi........ mara tenda ya tiketi za mechi bado kutangazwa huku ligi inaendelea na watu tunanunua tikets,....utakuta wenye uwezo wa kulipa viingilio ndo wanaoingia viwanjani bure kwa kisingizio eti ni wadau. Hapo utakuwa na hamu kweli ya kufuatilia ligi! Tunafuatilia kiugumu ugumu tukiamini kuwa haya yote yatakwisha.
 
Back
Top Bottom