Lift za PPF Tower msitumie jamani....

Boflo

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
4,384
4,409
Jana nilienda ppf tower, wakati nasubiri kupanda lift nilikuwa na wamama kadhaa na mkaka mmoja,

tukapanda, nilikuwa nashuka floor ya tano pamoja na wengine 2 , waliobaki walikuwa wanashuka floor za juu

zaidi... wakati Lift inakaribia kufika foor ya 5 ikawa inashuka chini kwa kasi sana, halafu inarudi tena kama

mara 3, wamama walikuwa wanaogopa sana, yule mkaka akatutoa wasiwasi akasema ndio kawaida ya ile lift

na inatakiwa kufanyiwa marekebisho....nilitamani nifungue mlango wa lift nitumie ngazi...lakini hakuna hiyo

option mpaka ufike floor unayotaka....Kuna siku hii lift italeta madhara makubwa, Watz naona hawathamini kabisa

maisha yao...

ppf 2.JPG
 
kuna siku nilipanda lifti hapo, nikapress floor niliyokuwa naenda, baada ya mlango kujifunga ikagoma kupanda wala kushuka, nilitamani nizimie baada ya kama dakika kidogo mlango ukajifungua, spidi niliyotoka nayo si ya kawaida
 
lift zina mambo mengi...mfano ni katika movie ya "Devil"
 
Hivi system ya tz itaacha lini kufanya kazi kwa feedback. yaani unyeshewe na mvua ndipo uchukue mwamvuli
 
Mimi haya ndio makazi yangu ya pili baada ya nyumbani kwangu...to be honest PPF Tower imefulia kama management au wahusika wengine wowote wa PPF wapo huku JF basi wasikie... sio lift tu vyoo ni vichafu na vibovu, umeme ni wa tabu, AC hamna, system ya maji ndio usiseme....wadau msione vioo kwa nje vinapendeza ndani ni balaaa.....
 
niliposkia voda wamehama pale, basi nikajua jengo ndo limekwisha chakaa,
pole kwa wapangaji wa jengo hilo
 
Mie nilikwama kwenye lifti hiyo 2008 kwa dk kumi. Actually hakuna mpangaji wa jengo lile ambaye hajawahi kukwama. Ni tatizo sugu kama la rushwa vile......
Kitu kinaitwa maintanace kwa watanzania ni tatizo!
 
yote tisa kumi ni hap[o KITEGA UCHUMI.. lile jengo ni kama nyumba ya udongo..lift zake ku stuck ni kitu cha kawaida sana wengine mbaka walizimia..
 
ZIle lift zinamatatizo sana, service inafanyika kila mara lakini hakuna matokeo mazuri, cjui wale technicians wababaishaji au labda wadau hawataki kutumia pesa za kutosha kufanyia services
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom