Libya's NTC Flag removed at the Dar es Salaam Embassy

siwezi shangazwa na msimamo wa membe, kazeeka kisiasa sikuzi hakuna flag kuna INTERNATIONAL BUSINESS haya mabendera ni trade make, yakwamba wapi unaruhusiwa kupitisha rupia na kufanya biashara, sisi tubado tuko wakati wa FRELIMO, ZANOPF na ndio maana kiuchumi hatuna rafiki zaidi ya msauzi anayetukamua kila siku.

WATANZANIA tuchange mentality, kama membe ni kidume havunje ubalozi na QUATAR kwa kuleta ndege ya kivita nchi na kuiba wanyama, au wapigi barua kama alivyofanya kwa balozi wa libya

Kwa sasa NTC ni kama mtoto mchanga kwetu, lakini hawa jamaa wana over 70 trillion to spend, watakuwa wakubwa kesho tu na hiyo barua wanayo kwenye mafaili yao; tungechukua busara ya warussia ingekuwa bora
 
Ndugu yangu ni lini utakuwa na utashi na kuachana na ujinga huu? Wewe unadhani kilichofanyika kilikuwa ni kizuri? Kwa taarifa yako hii medani ya kidiplomasia kuna rules of the game na zinapokiukwa nchi ambayo ina ufahamu wa sheria za kidiplomasia kama ya kwetu haiwezi kulifumbia macho suala hili. Eti atatupatia matazizo? Brother kuwa na msimamo siyo kukimbilia kulaumu na kuruhusu watu ku-compromise na misingi ya sheria za kimataifa.

Watanzania tumerogwa wakati wenzetu wakigombania biashara na Libya sisi tunabishana juu ya bendera na kujifanya wanadiplomasia upumbavu mkubwa.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Ndugu yangu ni lini utakuwa na utashi na kuachana na ujinga huu? Wewe unadhani kilichofanyika kilikuwa ni kizuri? Kwa taarifa yako hii medani ya kidiplomasia kuna rules of the game na zinapokiukwa nchi ambayo ina ufahamu wa sheria za kidiplomasia kama ya kwetu haiwezi kulifumbia macho suala hili. Eti atatupatia matazizo? Brother kuwa na msimamo siyo kukimbilia kulaumu na kuruhusu watu ku-compromise na misingi ya sheria za kimataifa.

Mkuu sawa balozi kaweka bendera ya Gaddafi nje. Vipi kinachoendelea ndani ya ubalozi kitakuwa na uhusiano wowote na iliyokuwa serikali ya Gaddafi? Kutundika bendera ya Gaddafi nje ya ubalozi kutabadilisha balozi na mission nzima kubadili uamuzi wao wa kuitambua NTC? Au kwa vile bendera ya Gaddafi imerudishwa basi Membe ata judge the book by its cover? Au itambidi asome kitabu chote ili ajue content nzima?
 
Which laws of the lands? can Membe tell us what was the Tanzania' Law violated by that flag?

I think the word law of the land was misused there, rather than will of the politicians and Qadhaffi allies.
 
Mkuu sawa balozi kaweka bendera ya Gaddafi nje. Vipi kinachoendelea ndani ya ubalozi kitakuwa na uhusiano wowote na iliyokuwa serikali ya Gaddafi? Kutundika bendera ya Gaddafi nje ya ubalozi kutabadilisha balozi na mission nzima kubadili uamuzi wao wa kuitambua NTC? Au kwa vile bendera ya Gaddafi imerudishwa basi Membe ata judge the book by its cover? Au itambidi asome kitabu chote ili ajue content nzima?

Hawa watu wamechoka kufikiri, mtu hasiye fikiri kama membe hata sijui ali-penetrate vipi hadi akawa Waziri, nadhani ndio hizi system za kidhalimu, unafki na wizi!

Kama serikali yetu haiitambua NTC walipaswa kufunga barozi ya Libya siyo kuzuia bendera, maana hao wenye hiyo bendera ndio wanao tawala Libya, huwezi kuwachagulia bendera labda kama huwataki na uwatambui basi ubalozi ufungwe maana huo ni ubalozi wa watu wa Libya siyo ubalozi wa Qadhaffi na NTC ndio walioichua Libya.

Ni kwasababu tu tunaongozwa na watu wenye akili kama za huyo Qadhaffi za kudhani ukiwa kiongozi lolote linalokufurahisha wewe binafsi ndio lazima unao waongoza walitekeleze, hapa wanaongozwa na utashi binafsi siyo matakwa ya nchni.

Kama ingekuwa matakwa ya nchni Watanzania wangesha ambiwa tokea zamani kwanini Qadhaffi na sio NTC! na hata wangeambiwa siku nyingi ndoa ya watawala wetu na Qadhaffi, lakini hata walipo olewa na Qadhaffi hakuona umuhimu wa kuwaeleza wananchni maana wana amini kila linalo furahisha mioyo yao ndio matakwa ya nchni.
 
Hongera membe,
ila waasi watakuja elewa kwamba wamedanganywa
 
Kwanini OAU na US hawakuitambua serikali ya MPLA in 1976?.....naomba mtaalam ajibu hili swali,halafu aeleze tofauti ya AU kutoitambua serikali ta NTC leo hii.
 
Karibu dunia nzima wanaheshimu na kutambua baraza la mpito Libya kwa kuwa limetoka kwa wananchi wenyewe.! Unafiki wa serikali .
 
Karibu dunia nzima wanaheshimu na kutambua baraza la mpito Libya kwa kuwa limetoka kwa wananchi wenyewe.! Unafiki wa serikali .
Kwani uhuru walioupata wananchi wa Angola baada ya kuwatimua wareno, wakisaidiwa na Soviet Union na Cuba ulikuwa na tofauti gani na huu wa Libya?
 
Kwani uhuru walioupata wananchi wa Angola baada ya kuwatimua wareno, wakisaidiwa na Soviet Union na Cuba ulikuwa na tofauti gani na huu wa Libya?
Ndio unafiki wenyewe mkuu wangu siku zote tunatazama upande mmoja wa sarafu..
 
kwani uhuru walioupata wananchi wa angola baada ya kuwatimua wareno, wakisaidiwa na soviet union na cuba ulikuwa na tofauti gani na huu wa libya?
Kusaidiwa na mataifa ya nje kumuondoa mkoloni hiyo ni sawa na inakubalika, Wananchi wengi wa Libya wanampenda Ghadafi.

Kusaidiwa na mataifa ya nje ili kuitia nchi katika ukoloni, (kinachofanyika hivi sasa Libya) ni kuirudisha nchi katika ukoloni kupitia hawa puppet leaders wa NTC.

KUMLINGANISHA GHADAFI NA UKOLONI WA KIRENO NI MAMBO YASIYOENDANA KABISA, GHADAFI ALIKUWA MZALENDO MWANAMAPINDUZI ALIYEIPA HESHIMA LIBYA DUNIANI KWA KUSIMAMA KIDETE KULINDA RASILIMALI ZA NCHI, NA KUJITAHIDI KUJENGA TAIFA LENYE MAISHA BORA, WAKATI MRENO ALIKUWA NI MKOLONI MWENYE KUNYONYA WANANCHI WA ANGOLA.
 
Heri uishi maisha ya shida uwe huru, kuliko kuishi maisha ya raha nakuwa mtumwa wa fikra
 
Hiyo bendera itapandishwa tu, nadhani serikali inajaribu kukwapua yale mamilioni waliyotoa walibya na wakaweka masharti namna ya kuyatumia. Sasa wakiwatambua NTC ubalozi utaendelea kuwabana kuhusu pesa zile kwa kwa sasa hazina mwenyewe. Lakini Membe na Jk wanapaswa kutambua kuwa tunaihitaji Libya zaidi ya tunavyomuhitaji Daffi. Yaani, Daffi kwishney........! Hata leo hii waandishi wa habari walipokuwa wakitembezwa Bab Al aziziya chumbani kwa Ghadaffi kakutwa 'rebel' mmoja kajilaza kitandani kwa mkuu bijikoromea bila wasiwasi. viva NTC na tunasubiri mapinduzi ya Tz

View attachment 36379

Inasikitisha sana kuona Waafrika wa leo bado wana akili zile za kubadilisha dhahabu na "Shanga". Kuwatambua ' Wahuni wa Bengharz' ukiwa wewe unaitakia mema Afrika yenye umoja, amani, uhuru, na maendeleo ya kupigiwa mfano ni sawa kujidhihirisha kuwa uko tayari kupokea ushanga uliotengenezwa kwa mbegu za limao ili utoe kilo moja ya dhahabu. Hivi hamuoni kuwa uhuru wa Afrika kujiamulia mambo yake unavurugwa?
 
kwa unafiki wa waafirika ngozi nyeusi, Qaddafi is no more.

Ni mbaya sana kuwa nafikra kuwa Kuangushwa serikali ya Libya ni kumuangusha Comred Gaddaf pekee, ukiwaza hivyo ujue wewe sio mwafrika unayetaka umoja, uhuru na maendeleo ya Afrika na watu wake. hawa wanokazana kumuangusha C. Gaddaf watazame matendo yao ya sasa, kwanza wahuni (mliona kwenye luninga waliokuwa wakifanya walipo fika tripoli, wanatuhumiwa kubaka wanawake na watoto , wabaguzi wa rangi- wanaua waafria weusi), pili wapumbavu (wamevuruga ustawi wa Libya kwa kuwaalika wavurugaji wa Umoja wa Afrika huru-junzi mlisikia walichokubaliana na Sarkozy) na maovu mengi mengi kweli kweli.
 
Inasikitisha sana kuona Waafrika wa leo bado wana akili zile za kubadilisha dhahabu na "Shanga". Kuwatambua ' Wahuni wa Bengharz' ukiwa wewe unaitakia mema Afrika yenye umoja, amani, uhuru, na maendeleo ya kupigiwa mfano ni sawa kujidhihirisha kuwa uko tayari kupokea ushanga uliotengenezwa kwa mbegu za limao ili utoe kilo moja ya dhahabu. Hivi hamuoni kuwa uhuru wa Afrika kujiamulia mambo yake unavurugwa?
<br />
<br />
Nduguyangu hizi serekali za Africa zinazoongozwa na madicteta ambao rasilimali za nchizao zinanufaisha familia zao tu, si heri ya mkoloni?
 
Back
Top Bottom