Libya na gadafi tutaikumbuka milele.

KISOSORA

Member
Jan 14, 2011
34
0
Hivi wana JF kule Libya ni maandamano au waasi?maana kama ni maandamano wanapata wapi silaha?
 
Libya mngependa kuwa kama tanzania ambayo inajisifu kuwa na amani lkn haina uchumi mzuri?? Mngependa kuwa kama tanzania ambayo viongozi wanahubiri amani bila kueleza tafsiri ya amani ni kitu gani
 
Hivi wana JF kule Libya ni maandamano au waasi?maana kama ni maandamano wanapata wapi silaha?

Ndugu sijakusoma. Mbona kichwa cha somo haki-reflect content?

Anyway, kama ni kuikumbuka Libya/Qadaffi inategemea ni kundi gani la kijamii unalozumzia. Kwa baadhi yetu tutamkumbuka sana kwa kutusaidia kujenga majumba ya ibada na kufadhili dini yetu hata kutaka kuifanya dini yetu iwe ndio dini rasmi ya Africa kupitia muungano wao wa AU. Ila kama mtanzania nitamkumbuka sana kwa kuwa upande wa Nduli Idd Amin Dada dhidi ya Tanzania wakati wa vita ya Kagera. Akili kichwani mwako.
 
Hivi wana JF kule Libya ni maandamano au waasi?maana kama ni maandamano wanapata wapi silaha?


Ni waandamanaji waliolazimishwa kuwa wapiganaji na si waasi!

Hizo silaha zilikuwa za majeshi ya serikali, baada ya kuamuriwa kuwashambulia raia wanajeshi wengi waliasi na kujiunga na maandamano hivyo silaha za hivyo vikosi zikawa za hao waandamanaji!

Ikumbukwa hali Libya iko hivi kutokana na approach ya Gaddaf kwa waandamanaji na si kwasababu waandamanaji walikuwa na silaha....!

Kuhusu heading yako "Libya na gaddafi tutaikumbuka milele". Hapo hujasomeka; ni kukumbuka kama sisi watanzania au wana-ulimwengu?



 
Hivi wana JF kule Libya ni maandamano au waasi?maana kama ni maandamano wanapata wapi silaha?

Libya ina historia ndefu sana ya Kikabila. Hivi vikundi vinavyopigana na Gaddafi, ni vikundi ambavyo vinataka mabadiliko ambavyo havipo ktk kabila la Gaddafi. Yalianza Maandamano, sasa hivi Libya ipo ktk Civil War.
Kujibu heading yako kwamba tuaikumbuka Libya ya Gaddafi milele, I will say Yes.
Gaddafi kachangia sana ktk upatikanaji wa Uhuru ktk nchi za Afrika. Ni Rais pekee aliyebakia wenye mawazo kama ya Nyerere, Nkurumah, ya Africa kuwa States moja.
Ni Rais Pekee mwenye kutumia Nembo ktk Ndege, Nguo zake, zenye kutangaza Africa kabla ya Libya. Sema kuna mistakes nyingi ambazo kazifanya ambazo zitafanya watu washindwe kumkumbuka milele. Kawanyima haki raia wake, na haya mauaji anayofanya tayari yameshamuharibia kuheshimika kama kiongozi mkombozi wa Afrika.
 
Back
Top Bottom