LHRC yaitisha Maandamano nchi nzima kupinga malipo ya DOWANS

Big Up mkuu kwa maelekezo mazuri hapo chini!!!!!!!!!!!!!!

Lakini, kwa hili la kusubiri maelekezo; sote tuwe sehemu na chachu wa mabadiliko tukiwa katika nafasi ya kushika ushukani wenyewe nala kusionekane wengine ni abiria tu kwenye jahazi la kushinikiza kutokee mabadiliko ya aina yoyote ile.

Tafadhali sana hakikisha unatoka na chupa ya maji zile kubwa za lita 1.5 na kitaulo kidogo mkononi.

Wakati wote wa maandamano mnapoona askari wanasogelea lowesha kitaulo chako kabisa kiwe na maji, utakaposikia bomu limerushwa funika macho yako na hicho kitaulo halafu chuchumaa hapo ulipo kwa muda, kuwa muangalifu wakati wa kuchuchumaa watu wasije wakakukanyaga maana hicho ndicho kinachosababisha watu wengi kupoteza maisha.

Tunaomba watu wa LHRC watueleze utaratibu wa kufahamiana ili tunapokamatwa na kuwekwa ndani waweze ku take stock, tukiwa wengi zaidi hawataweza kutukamata maana magereza yatakua madogo hebu tutoke tukomboe nchi yetu, tunaomba sana media watu support, hebu wasome experience ya wa pakistan wakati wa maandamano ya wanasheria vijana, kwenye ukombozi unaojulikana leo kama the black coat movement ukibeba vazi la mawakili, media ili play a very significant role kwa kuwaonyesha walioko majumbani kinachoendelea nao wakaweza kutoa uoga na kujiunga na wenzao.

Tuko pamoja tunasubiri maelekezo ya wanaharakati
 
Je ni maandamano ya kupinga malipo ya Dowans ndio hivi sasa yanamfanya Dr Dr Dr Dr (kwenye mchakato bado UDSM) Kikwete kuanza kufunga njia mbalimbali jijini Dar es Salaam na kusemekana kujiandaa kutangaza HALI YA HATARI nchini kweli???????????
 


Madaraka ya kutangaza hali ya hatari Sheria ya 1984 Na.15 ib.6 ya katiba ya jamhuri ya Muunago wa Tanzania​




32​
(1) Bila ya kuathiri Katiba hii, au sheria iliyotungwa naBunge kwa ajili hiyo, Rais aweza kutangaza hali ya hatari katikaJamhuri ya Muungano au katika sehemu yake yoyote.

(2) Rais aweza tu kutangaza kuwa kuna hali ya hatari iwapo-
(a) Jamhuri ya Muungano iko katika vita; au
(b) kuna hatari hasa kwamba Jamhuri ya Muunganoinakaribia kuvamiwa na kuingia katika hali ya vita; au
(c) kuna hali halisi ya kuvurugika kwa amani ya jamii aukutoweka kwa usalama wa jamii katika Jamhuri yaMuungano au sehemu yake yoyote kiasi kwamba nilazima kuchukua hatua za pekee ili kurejesha amanina usalama; au
(d) kuna hatari dhahiri na kubwa, kiasi kwamba amani yajamii itavurugika na usalama wa raia kutoweka katikaJamhuri ya Muungano au sehemu yake yoyoteambayo haiwezi kuepukika isipokuwa kwa kutumiamamlaka ya pekee; au
(e) karibu kutatokea tukio la hatari au tukio la balaa au labaa ya kimazingira ambalo linatishia jamii au sehemuya jamii katika Jamhuri ya Muungano; au
(f) kuna aina nyingineyo ya hatari ambayo kwa dhahiri nitishio kwa nchi.

(3) Endapo inatangazwa kwamba kuna hali ya hatari katikaJamhuri ya Muungano nzima, au katika Tanzania bara nzima auTanzania Zanzibar nzima, Rais atatuma mara nakala ya tangazohilo kwa Spika wa Bunge ambaye, baada ya kushauriana naKiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni, ataitisha mkutano wa Bunge, ndani ya siku zisizozidi kumi na nne, ili kuitafakari hali yamambo na kuamua kupitisha au kutopitisha azimio, litakaloungwamkono na kura za wajumbe wasiopungua theluthi mbili yawajumbe wote, la kuunga mkono tangazo la hali ya hatarilililotolewa na Rais.

(4) Bunge laweza kutunga sheria inayoweka masharti kuhusunyakati na utaratibu ambao utawawezesha watu fulani wenyekusimamia utekelezaji wa mamlaka ya Serikali katika sehemumahususi za Jamhuri ya Muungano kumuomba Rais kutumiamadaraka aliyopewa na ibara hii kuhusiana na yoyote kati yasehemu hizo endapo katika sehemu hizi kunatokea yoyote katiya hali zilizotajwa katika aya ya (c), (d) na (e) za ibara ndogo ya(2) na hali hiyo haivuki mipaka ya sehemu hizo, na pia kwa ajiliya kufafanua utekelezaji wa mamlaka ya Serikali wakati wa haliya hatari.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania​


(5) Tangazo la hali ya hatari lililotolewa na Rais kwa mujibuwa ibara hii litakoma kutumika-
(a) iwapo litafutwa na Rais;
(b) endapo zitapita siku kumi na nne tangu tangazolilipotolewa kabla ya kupitishwa azimio lililotajwakatika ibara ndogo ya (3);
(c) baada ya kupita muda wa miezi sita tangu tangazohilo lilipotolewa; isipokuwa kwamba kikao cha Bungecha weza, kabla ya muda wa miezi sita kupita,kuongeza mara kwa mara muda wa tangazo hilokutumika kwa vipindi vya miezi mingine sita kwaazimio litakaloungwa mkono na kura za wajumbe wakikao hicho wasiopungua theluthi mbili ya wajumbewote;
(d) wakati wowote ambapo mkutano wa Bungeutalitengua tangazo hilo kwa azimio litakaloungwamkono na kura za wajumbe waiopungua theluthi mbiliya wajumbe wote.

(6) Kwa madhumuni ya kuondoa mashaka juu ya ufafanuziau utekelezaji wa masharti ya ibara hii, masharti ya sheriailiyotungwa na Bunge na ya sheria nyingine yoyote, inayohusuutangazaji wa hali ya hatari kama ilivyotajwa katika ibara hii,​

yatatumika tu katika sehemu ya Jamhuri
 
Maandamono haya yanatuhusu kila mmoja bila kujali kazi yako ili tuwe na uhakika na ustawi mzuri wa uchumi wetu bila mi-tapeli ya Dowans.
 
Maandamano yakiruhusiwa tutakwenda kusikiliza hotuba kalikali za wanaharakati na wanasiasa machachari kisha iweje baada ya hapo? Yaani hivyo tu ndo itazuia serikali isilipe Dowans? HAPANA, twendezi zaidi ya hapo, hotuba zimetuchosha. Tunachotaka ni kwenda kumtoa mkoloni mwizi magogoni! Kama ni maandamano ya mdundiko na hotuba hazina tija, twendeni tukawashikishe adabu japo kwa kuanzia kuchoma ofisi zote za SSM zitakazo kuwa mbele yetu ili wajue hatutanii! Mkikataa ni hili basi itakuwa mnafanya usanii!
 
Naona kumbe watu wengi sana hatujui vile silaha ya MAANDAMANO inavyofanya kazi kuliko vurumai. Ngojeni basi kidogo mtagundua siri yake baadaye kidogo.

Maandamano yakiruhusiwa tutakwenda kusikiliza hotuba kalikali za wanaharakati na wanasiasa machachari kisha iweje baada ya hapo? Yaani hivyo tu ndo itazuia serikali isilipe Dowans?

HAPANA, twendezi zaidi ya hapo, hotuba zimetuchosha. Tunachotaka ni kwenda kumtoa mkoloni mwizi magogoni! Kama ni maandamano ya mdundiko na hotuba hazina tija, twendeni tukawashikishe adabu japo kwa kuanzia kuchoma ofisi zote za SSM zitakazo kuwa mbele yetu ili wajue hatutanii! Mkikataa ni hili basi itakuwa mnafanya usanii!
 
Mh Nimechoka Mie na kelele za kwenye keyboard.

Kuna mtu mwingine tena aliyekuja na ID ya maandamano, watu tukapanga mikakati wee, mpaka leo sijaona maendeleo.

Sasa imefika wakati tuandamane ukweli, tutoke barabarani, hata kama kuna waoga nao watatoka.

Jamani tarehe ya kuanza maandamano iwekwe na tuanze.
 
nafikiri Sasa Watanzania wanaanza kuelewa nini maana ya ukombozi.Tuwaunge mkono wanaharakati wote.
 
LHRC mbona hamtangazi tu tarehe au nanyi mshapokea mlungula kutuliza inshu yaani kwa wabongo kwa sasa kinachotakiwa ni initiator mengine yote tuachieni wananchi wenyewe tutajua hayo mabomu ya machozi watapiga hadi yaishe mwisho wa siku kitaeleweka tu.
 
jamani nna mashaka kama tunaweza tukawa wengi katika tukio hili nahisi wengi hawana taarifa.....nmekuwa nkijaribu kuwauliza watu wengi kuhusu ttukio hili wemeonekana hawajui lolote so naomba waahusika watangaze basi walau kwenye redio ili waananchi wajue na wafike cku hiyo
 
Hali ni mbaya kifedha CCM, mafisadi wamegoma kukisaidai fedha chama chao mpaka walipwe kwanza fedha za DOWANS. Isipolipwa chama kitazidi kuwa hali mbaya zaidi na JK ndipo atang'olewa kwa urahisi uenyekiti CCM Taifa.
 
Wama Jamii kwanza Naunga maandamano. Lakini pia nafikiri wao kama wanasheria wawe na utamaduni wa kuifuatilia hii mikataba pale inapoundwa. Hii itatusaidia kujua kama mikataba ni mibovu na tuandamane kuikataa mikataba yenyewe na sio kuandama kwa ajili ya matokeo ya mikataba. Leo hii kuna mikataba mibovu chungu nzima hii Dowans chamtoto. KUZUIA NI KUZURI KULIKO KUTIBU.
 
"Kituo cha Sheria"....na ni sheria hizi hizi ndo zimeamulu kulipwa kwa tozo la 111bL. Sasa watuambie wanapingana na mahakama ya nchi ambayo ndio mtafsili wa sheria zetu au wao wanatafsiri vp sheria iliyo amua kulipa kwa tozo hiyo
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom