Zion Daughter
JF-Expert Member
- Jul 9, 2009
- 8,921
- 4,235
Hakijaharibika kitu,Kupitia wanachi serikali itaamka na kwenda mahakamani kupinga.Lakn bila PUBLIC PRESSURE mabadiliko hayatakuwepo....upo?dont blame juhudi za wapigania Haki.kwani wewe umefanya nini ?Hawa waache ujinga. Mahakama imeamru ilipwe na hapo wanapinga maamuzi ya mahakama. Maamuzi ya mahakama yanapingwa mahakamani.
Watu waache kutufanya mataahira, kinachotakiwa waangalie ni vipi tumeingia katika hali tuliyoingia? Uongo ulikuwa wapi? Nani kamdanganya nani?
Huu ndio ukweli ambao haujasemwa ambao utaendelea kuwaumiza wananchi na watu wengi. Waishinikize bunge waunde kamati mpya waangalie ni kwanini badala ya kuikoa nchi kutokana na giza na kulipa mapesa mingi sasa tunalipa mapesa bure. mitambo iliyokuwa mibovu ndiyo sasa inatupa umeme kupitia symbion. wale wabunge waliosema tusinunue wako wapi leo?
Kuna unafiki mkubwa na hawa LHRC inatakiwa waandamane siyo kwa kupinga malipo ya dowans bali kudai tume huru ya kuchunguza tatizo kwa ujumla wake kuanzia kwa wabunge waliochunguza mara ya kwanza nao wachunguzwe kuwa je walikuwa na manufaa binafsi ya kisiasa na kiuchumi au vipi. Kuna mambo mengi ya kuangalia kwa ujumla wake na siyo hizi dalili za juujuu tu.