LHRC yaishtaki serikali ya Tanzania ICC

PISTO LERO

JF-Expert Member
Mar 8, 2011
2,819
1,454
Katika hali inayoleta matumaini kituo cha haki na sheria kimeishaki serikali katika mahakama ya icc.

Akizungumzia hatua hiyo bibi helen kijo,alisema hatua hiyo ni ya mwanzo na hawatarudi nyuma hivyo kuwaomba watanzania kuwaunga mkono.

Bibi kijo amesema kuwa wameiomba mahakama hiyo kufanya uchunguzi wa mauwaji ya raia wasio na hatia yanayofanywa na serikali kupitia jeshi la polisi na kusema wamefungua pia shauri kama hilo katika mahakama ya africa.

Amesema kitendo cha serikali kuwahamisha watendaji wanaofanya mauwaji hayo na kuwapeleka sehemu nyingine bila kuwawajibisha hakivumiliki na kuwa hawata kaakinya mpaka watendaji hao watakapo wajibishwa na sheria kufata mkondo wake.

Huku akitolea mfano wa kamanda wa mkoa wa iringa aliye hamishiwa iringa kwa kosa la mauwaji
na kurudia kitendo kilekile cha kuwauwa raia wasio na hatia na mpaka sasa hajachukuliwa hatua yoyote,huku serikali kupitia waziri wa mambo ya ndani kwa kitumia kodi za walalahoi wakijaribu kuficha ushahidi.

Bibi kijo amesema ni lazima serikali iwawajibishe wote waliohusika na mauwaji ya watanzania na kusema si iringa pekee,ni pamoja na mikoa yote ambayo mauwaji kama hayo yalipotokea.
 
Sio serikali iwawajibishe wenye makosa, ni serikali yenyewe ndiyo inapaswa kuwajibishwa..hapa nina maana kuwa serikali yote.
 
hivi serikali ikishitakiwa kwa kosa la jinai au makosa nani hupelekwa lupango pindi serikali inaposhindwa kesi
 
Serikali haishitakiwi ICC! Hii ni mahakama ya makosa ya jinai ya kimataifa, inahukumu watu tu, haina jurisdiction juu ya States... Sema wame-apply for investigation, and that's upon the Prosecutor to accept or decline entering into oinvestigation.
 
hivi serikali ikishitakiwa kwa kosa la jinai au makosa nani hupelekwa lupango pindi serikali inaposhindwa kesi

Mkuu lazima wawepo wahusika
Kenya akina UHURU KENYATA na WILIUM RUTO, Riberia CHARLES TELLOR, Ivory Coast GBAGBO nk

Sijui umegundua nin, hasa kwa jiran zetu wakenya?
 
Kwa mahali tulipofika, lazima tukubaliane kwamba hiyo ni hatua sahihi ili ukweli ujulikane- kabla ya machafuko yasiyo ya ulazima. Damu ya watz haiwezi kumwagika hivi hivi kwa maslahi ya watu wachache na familia zao wanaotaka kubaki madarakani kwa nguvu huku wananchi wameshawachoka.
Ukiwatoa kwa kura wanaiba -jibu ndo hilo ICC. Nitafurahi kama taarifa hiyo ni ya kweli.
 
Safi sana dr.Hellen Kijo Bisimba,Dhaifu ameshindwa kuongoza nchi.
"Yana Mwisho"
Naanza kuiona 'The Hegue " kwa mbali ikianza kuinyemelea Tanzania.mwanzo mzuri mama,kaza uzi.Haiwezekani watu washindwe kufanya kazi zao, halafu wajihalalishie mauaji na vitisho ili waendelee kukaa madarakani.Tunahitaji nchi huru ya kuwajibishana pale tunaposhindwa kutekeleza majukumu yetu.Sio kutishana tishana.
 
hivi serikali ikishitakiwa kwa kosa la jinai au makosa nani hupelekwa lupango pindi serikali inaposhindwa kesi

Mkuu lazima wawepo wahusika
Kenya akina UHURU KENYATA na WILIUM RUTO, Riberia CHARLES TELLOR, Ivory Coast GBAGBO nk

Sijui umegundua nin, hasa kwa jiran zetu wakenya?

Hapa kwetu kamuhanda, arusha, morogoro, mara nakwingineko wapo wahusika.

Serikali ni watu na wapo wanaeleweka na mashahidi wapo kama vile Nape - morogoro nk
 
km ni kweli hii italeta heshima. serikali makini lazma iheshimu wananchi ambao ndio wameiweka madarakani.
 
Jamani hii serikali sijui lini itakuja kusikia
Dr Slaa alisema mtajuta kuichagua CCM na sasa kweli inatokea
 
Katika hali inayoleta matumaini kituo cha haki na sheria kimeishaki serikali katika mahakama ya icc.

Akizungumzia hatua hiyo bibi helen kijo,alisema hatua hiyo ni ya mwanzo na hawatarudi nyuma hivyo kuwaomba watanzania kuwaunga mkono.

Bibi kijo amesema kuwa wameiomba mahakama hiyo kufanya uchunguzi wa mauwaji ya raia wasio na hatia yanayofanywa na serikali kupitia jeshi la polisi na kusema wamefungua pia shauri kama hilo katika mahakama ya africa.

Amesema kitendo cha serikali kuwahamisha watendaji wanaofanya mauwaji hayo na kuwapeleka sehemu nyingine bila kuwawajibisha hakivumiliki na kuwa hawata kaakinya mpaka watendaji hao watakapo wajibishwa na sheria kufata mkondo wake.

Huku akitolea mfano wa kamanda wa mkoa wa iringa aliye hamishiwa iringa kwa kosa la mauwaji
na kurudia kitendo kilekile cha kuwauwa raia wasio na hatia na mpaka sasa hajachukuliwa hatua yoyote,huku serikali kupitia waziri wa mambo ya ndani kwa kitumia kodi za walalahoi wakijaribu kuficha ushahidi.

Bibi kijo amesema ni lazima serikali iwawajibishe wote waliohusika na mauwaji ya watanzania na kusema si iringa pekee,ni pamoja na mikoa yote ambayo mauwaji kama hayo yalipotokea.

Tanzania sio MWANACHAMA wa ICC; Kwahiyo hiyo Itaishia to the nearest dust bin...
 
Back
Top Bottom