LHRC: Wabunge upinzani wafunika CCM; Makinda dhaifu!

Jamani mbunge wetu tangu achaguliwe tulimuona kwenye msafara wa waziri yeye yuko bize bongo, sisi tukiwa na shida tunampataje, simu zao walizoacha huku vijijini hazipatikani, contacts zingine kama email hawaachi, viongozi acheni kuwa mbali na watu wenu!
 
Hapo ndo watanzania walalahoi wanatarajia wabunge wao wataleta mabadiliko chanya.
Ni ndoto kuyafikia madadiliko chanya kama bunge letu litajazwa na watu 400 wengi wao wasio wazalendo, ningependekeza wabunge wawe wanapimwa kwa michango yao si kwa jimbo wanalotoka tu bali mchango wao kwa taifa ikiwezekana waweze kuwajibishwa hata kabla ya kipindi chao kwisha nafikiri at least itaongeza chachu ya uwajibikaji wakiwa bungeni.
 
DSN
Tuko pamoja Mwenyekiti wa CCM anajitahidi kusafisha uozo ili chama kionekane kipya ameamua kumtosa rafiki yake kipenzi ili angalau kurudisha imani ya wananchi kwa chama, lakini wabunge hawalioni hilo ndiyo wanazidi kumtwisha mzigo na wakitoka hapo wanasema hawajui kwanini wananchi wanaichukia CCM, hawajui wananchi wa sasa ni wa DOT.COM wanawaona wabunge wao wanavyopiga makofi na kupitisha mambo yasiyo maslahi kwa taifa. Ningekuwa mimi Mukama, Nape ningemsaidia Mwenyekiti wangu kwa kuwaonya wabunge wa design hii.

Na nyie mnaoonekana kumhurumia mwenyekiti wenu wa chama cha Magamba hamjui kwani wabunge wanatekeleza yale waliyotumwa na mabwana zao. Mswada unaletwa bungeni kwa masilahi ya watawala, na wabunge wa chama cha magamba waliishaelekezwa kwenye kamati zao. Sasa awaonye kwa lipi wakati lililokusudiwa linakamilishwa? - BIG UP WABUNGE WA USHINDANI
 
Aaahh!!hiyo ni kweli sbb Bunge lililopita tumelifuatilia wananchi kiukweli ccm huwa wanakipitisha kitu(Sheria)kwa maslahi yao na kifupi "WANAWASALITI HATA WANANCHI WALIOWACHAGUA"ccm a.k.a Chama cha MAGAMBA tupa kule
 
Hujasema, ni mbunge wa jimbo lipi tukusaidie? Maana wengi tunabanana nao kwenye foleni kila siku ndani ya jiji letu Dar es Salaam
 
Napata Shida sana kupata jibu hivi CCM kama CCM [sina tatizo nacho kama chama/Taasisi na katiba yake Perfect...mabadiliko kidigo yanaitajika kuendana na nyakati].Tatizo ni hawa watendaji/wanachama viongozi [Hivi Kweli CCM aina ENGINE-THINK TANK]. Hii Think Tank amabyo ni watu ambao hawako kufungamana pande yoyote [Bias] ile ila kuegemea ukweli. Mwendendo wa maamuzi ya kutegemea uamuzi wa chama naomba kuita ulevi wa KITAASISI.

Nimezaliwa nimekuta Mwasisi wa CCM akiwa hai,na kupitia kusoma historia nimeona na kujifunza vitu muhimu na vya msingi kwa utamaduni na asili yetu ni vyema kuvienzi. Kweli ukubwa dawa lakini kuna baadhi ya wakubwa [Kwa Maana ya Umri ] baadhi yao uwezo wao wa kufikiri na kuchanganua mambo haswa ya msingi ya kitaifa,ni tatizo kubwa sana ni hafadhari ya kijana mwenye umri wa miaka kumi na nane.

CCM ilipaswa kuwa na vitengo muhimu na wajibishi kwa wanachama na viongozi, sijui kama vipo manake kama vingekuwepo haya yote yasingetoke.Vitengo hivyo ambavyo vingekuwa na jukumu la kutathimini mchango wa kila mbunge ama kiongozi yoyote yule ndani ya CCM na Taasisi zake [SIO MAADILI hiyo najua wanayo na -Kama sikosei One of the RACHEL was the Member].Kupitia tathimini hiyo wanachama na viongozi waliofanya vizuri wangepewa pongezi na nishani kwa utumishi mwema na kukubali yale waliyoyatenda yameleta faida kwenye chama.Vivyo hivyo kwa watakaofanya ovyo na kutuhumiwa kwa matendo na mwenendo wao unaotia doa kwenye chama wawajibishwe mapema kabla UMMA aujawahukumu.

Vitengo hivyo vinavyotakiwa kuundwa na kuendeshwa na wanachama ambao ni Wanataaruma wa fani mbalimbali na wale ambao uadilifu wao sio wa kutiliwa shaka popote pale. Kwa ujumla wao timu hiyo [Think Tank] inaundwa na vikundi vinavyo tathimini mwelekeo na mahitaji ya UMMA wa Watanzania wa sasa hivi na siku zijazo na kutumia tafiti [Research kujua ukweli halisi wa matatizo ya watanzania y] hivyo basi wao kuwa Think Tank ya CHAMA CHA MAPINDUZI kulingana na mahitaji ya nyakati husika haswa. [On-spot].

Wabunge wa kupitia tiketi ya CCM ukiwaangalia na kutathimin muuonekano wao wakati wote wa Bunge, Msemo wa Mwalimu JK, ukimwangalia machoni useme eeh uyu kweli? na sio hata wewe?. Wengi wao mwonekano wao ni wa kutia shaka. Mbaya zaidi ukiwasikia wanavyochangia wamekaa KIUSHABIKI ZAIDI na SIO KIMAUDHUI ZAIDI [CONTENTS].

Mwalimu Julius K Nyerere wakati fulani kama sikosei alikua anautubia wakati ule wa mzee wa kilalacha ameshika speed kwenye uchaguzi, Mwalimu alisema zamani mtanzania alikua akipewa nafasi ya kuongea [Ili akizungumzia Umoja wa Mataifa] watu walio kwenye kikao husika, walikua wanasubili kwanza Mtanzania huyo amalize kuongea ,ndio watoke kwenda kuvuta ugoro ama sigara zao, kwa misingi kuwa wakiondoka kabla ya Mtanzania huyo ajamaliza kutoa mhadhala wake watapitwa na mambo muhimu ya kuchukua kwa faida ya Mataifa yao.

Hapo Mwalimu alimaanisha Watanzania walikuwa na maudhui [Content] ya kuiachia hadhara husika,vivyo hivyo kwenye bunge la zama hizo hata japo lilikuwa la Chama kimoja bado watu walikua na chakumfanya mtu kusikiliza.

Kwa sasa ukweli ulio wazi bila kuficha wabunge wa Chama cha Mapinduzi kwa lugha ya Dot.Com tunasema Wanaboa Kinoma [Boring or dull].Wakiinuka wabunge wa Upinzani kama Zitto, Tindu Lissu, Mnyika na Halima unasikia hamu kusikia watasema nini chenye kuleta matumaini.[Ludi kwa Mwalimu hapa kidogo Picha unaiona]. Tena Kidotcom tunasema WANAWAKILISHA haswa yaani wakiwa FULL na Takwimu [Data] na kwa kuwakilisha huko kunaendana na hisia halisi za mada husika na si mbwembwe za kishabiki kuliko ukweli halisia.

Chadema imejengwa na wabunge aina hiyo hapo juu na kuwa na mvuto kwa UMMA, kwa kuwa wako kwa ajili ya Taifa, kitu ambacho wabunge wa CCM hawana umakini huo,Ninakuwa na hamu kuona wabunge wa CCM wakiwa na Makarabrasha yenye takwimu mezani kwao kwa ajili ya kutoa na kuchangia mada ama hoja husika, tunasema kudadavua kile walichokielewa ndani ya muswada husika lakini wapi?

Wabunge wa CCM uwa wakipewa nafasi wanaanza kutoa pongezi karibu muda wote mpaka salamu kwa marafiki zao na wanafamilia wao, Jamani wabunge muda unaopewa ni wa wapiga kura wako, si wako kutoa historia ya ushindi wa kimbunga na vijembe vya taarabu.[You Guys be serious].

Tufike sehemu Wabunge wa CCM mvutike na kuwa wadadavuaji, tuache Ulevi wa Kitaasisi kuwa Ujuvi wako Kutaka KUJUA MAMBO ndani ya MUSWADA itakua ni KULETA UJUAJI [Tafsiri ya Kiswahili ambayo wengi wao naona ndio tatizo hili,ilikuwepo mpaka kwenye mashule miaka hiyo] kwani ulimwengu wetu sasa wa wadadisi wa miswada na hoja kwa kina, ndio wanaotakiwa na Jamii ili kutuonyesha huo UJUAJI ILI WAJUE KUWA UNAJUA NA SIO WA KUBULUZWA na lengo lako ni kujenga kitu bora,hata kama wote mnasafiri boti moja.Sio kwa kuwa Chama chako kwa kuwa ndio kinaunda Serikali basi wewe uwe Bwana au Mama NDIO MZEE.Kama hayo ndiyo yatakayo endelea basi msilalamike kwa yale yanayopigiwa kelele na UMMA.
 
lakini ktk kura za ndiyo au hapana za hoja ya lissu, pinda na wabunge wengi wa cuf walimuunga mkono lissu. Labda cuf nao washajicheki.
 
Hawa wabunge wa ccm wako kwa maslahi yao wenyewe siyo kwa ajili ya wanchi. Tusisahau, wabunge wangi wa CCM hawakuwa changuo la wananchi bali changuo la mafisadi; kwa hivyo basi tusione ajabu wasipokuwa ndani ya bunge au kuto kushiriki katika hoja zozote kwa sababu siyo wawakilishi halali wa majimbo yao.
 
Tathmini ya utendaji wa wabunge iliyofanywa katika Mkutano wa Tatu wa Bunge la 10 uliomalizika wiki iliyopita, umeonyesha kuwa wabunge wa upinzani wameonyesha ufanisi mkubwa ilinganishwa na wale wa chama tawala.

Taarifa ya tathmini hiyo iliyotolewa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) ambacho kilifanya kazi hiyo, inaonyesha kuwa wabunge wa upinzani wametoa mchango mkubwa wa kushiriki katika mijadala mbalimbali na kuuliza maswali na kutaka serikali iwape majibu katika mkutano huo na kuwafunika wabunge kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho kinaunda serikali.

Ofisa wa Uangalizi wa Bunge wa LHRC, Merick Luvinga, alisema wabunge wa upinzani walihoji mambo ya msingi na kutaka wapatiwe majibu wakati wa kuchangia muswada wa Uhuru wa Mahakama. Kadhalika, wananchi wameshauriwa mwaka 2015 katika Uchaguzi Mkuu kutowapigia kura wabunge ambao wameshindwa kutoa mchango wowote kwa maandishi au mdomo kwa ajili ya kutetea maslahi yao na badala yake wamekuwa kimya tangu mwaka 2005 hadi leo.

LHRC kimesema mkutano wa tatu wa Bunge la 10 wabunge wa upinzani walisimama imara na kuibana serikali licha ya kuwa wapo wachache tofauti na wale wa CCM ambao mara zote walitumia muda wao mwingi kuunga mkono hoja kwa asilimia 100 hata kama hazikuwa na maslahi kwa wapiga kura wao.

Luvinga alitoa tathmini hiyo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za kituo hicho. Alisema wabunge wa upinzani ni wachache na kwamba utafiti wa kitalaam unaonyesha kwamba ulipofika wakati wa mijadala wao walikuwa makini ikilinganishwa na wale wa CCM ambao wakati mwingi walikuwa nje na waliitwa kwa kengele ili waingie ndani kupiga kura kuamua jambo fulani kama kumeibuka utata na kisha baada ya hapo walitoka nje. Aliongeza kuwa wabunge hao waliitwa kuingia ndani ili kupiga kura huku wakiwa hawajashiriki katika mijadala hiyo na hivyo kuwafanya wapitishe maamuzi ambayo hawajui kiini chake. Kuhusu wabunge ambao hawajawahi kuchangia kwa mdomo au maandishi tangu mwaka 2005 hadi mkutano uliopita, Luvinga alisema watu wa namna hiyo wanatakiwa kuadhibiwa kwa kunyimwa kura mwaka 2015.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Imelda Urio, alisema miswada mbalimbali inayowasilishwa bungeni kwa hati ya dharura inawanyima haki wananchi kushiriki katika kutoa maoni yao. Alisema miswada ya serikali ni kitu kinachowahusu wananchi moja kwa moja na kuongeza kuwa isiwe inawasilishwa kwa hati ya dharura kama ilivyofanyika katika Mkutano wa Tatu wa Bunge uliopita. Katika mkutano huo ulioanza Aprili 5 na kuahirishwa Aprili 17, mwaka huu, serikali iliwasilisha kwa hati ya dharura tatu muswada wa Mapitio ya Katiba wa mwaka 2011 ili usomwe kwa mara zote, lakini uliahirishwa baadaye kutokana na ushauri wa Kamati ya Bunge ya Sheria, Katiba na Utawala kufuatia wananchi na wadau mbalimbali kuukosoa kuwa una kasoro nyingi.

Kuhusu mahudhurio na ushiriki wa wabunge katika kila mkutano, Urio alisema tathmini inaonyesha kwamba utoro ni mwingi pamoja na baadhi ya wabunge kusimama na kutoa shukrani nyingi za kuwashukuru wananchi, chama wanachotoka, rais na wabunge wenzao kwa kuchaguliwa katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka jana badala ya kutumia muda wanaopewa kuzungumza mambo ambayo yatasaidia kutatua matatizo yanayowakabili wananchi. Aliwataka wabunge kuweka maslahi ya wananchi mbele na kuacha itikadi za vyama kama ilivyofanyika katika mkutano uliopita kwa kuwa wakiendelea na mwenendo huo hawatafanikiwa kuwaondoa Watanzania katika dimbwi la umaskini na matatizo mengi yanayowakabili.

Kwa upande wa usimamizi wa Bunge, LHRC kilimshauri Spika wa Bunge, Anne Makinda, kurejea na kusimamia kanuni za chombo hicho ili kudhibiti maudhui na kuwepo kwa taratibu kwa wabunge kutoa hoja na kuzitetea. Kituo hicho kimesema hivi sasa baadhi ya wabunge wanageuza mhimili huo kuwa kijiwe cha mabishano yasiyokuwa na tija.
CHANZO: NIPASHE
 
Ni ujinga wenu kumchagua mbunge wakati hana hata makazi kwenye jimbo lake.
Baada ya miaka mitano anakuja mnampa tena kura kwa takrima ya tisheti na kofia na buku moja. Kazi kwenu. Mie mbunge wangu mnyika nikimhitaji nampata kwa njia nyingi tuu. Ili kuonyesha kuwa tuko nae karibu, daraja lililobomoka kwenye barabara ya baruti (bahama mama) chuo ameanza kulijenga
 
Na Asha Bani

WANAHARAKATI wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) wamesema Spika wa Bunge, Anne Makinda, ameshindwa kusimamia vizuri kanuni na maadili ya Bunge katika kujadili masuala yenye maslahi kwa wananchi.

Kwa mujibu wa wanaharakati hao, udhaifu huo wa Spika Makinda nusura usababishe uvunjifu wa amani bungeni.

Kaimu Mkurugenzi wa LHRC, Imelda Urio, alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za kituo hicho.

Alisema Spika Makinda, amesababisha kutokea kwa mvurugano bungeni kutokana na kutotumia vyema kanuni hivyo kupoteza mantiki ya maana ya vikao alivyokuwa akiviongoza jambo ambalo ni kinyume na maadili.


Aliyataja mambo ambayo Spika huyo aliyafanya bungeni ambayo hayakuwa na manufaa kwa taifa lakini yalichukua nafasi kubwa kujadiliwa kuwa ni kupitishwa miswada kadhaa kwa kura za jumla kwa ushabiki bila kujali uzito wa hoja mbadala.


Miongoni mwa miswada iliyoelezwa kupitishwa kishabiki ni ule wa uendeshaji wa mahakama uliopitishwa Aprili 16 mwaka huu, licha ya kupingwa kwa hoja na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu (CHADEMA).


Urio alieleza mjadala mwingine uliokuwa na maslahi kwa taifa lakini kutokana na kutokuwepo na usimamizi mzuri wa kanuni uliweza kuchukua sura ya chama badala ya taifa kuwa ni mjadala wa muswada wa marejeo ya Katiba.


Alisema udhaifu mwingine uliojitokeza bungeni ni kitendo cha wabunge kutumia muda mrefu kuzungumzia mambo ambayo hayakuwepo kwenye mjadala hivyo kupoteza muda wa kujadili hoja zilizokuwa zikijadiliwa.


"Huu ni ukiukwaji wa kanuni namba 64 (b), kwa mfano baadhi ya wabunge walirudia kutoa pongezi na shukrani ambazo tayari zinakuwa zimeshatolewa na Spika au kiongozi wa shughuli za serikali bungeni kwa mujibu wa kanuni namba 151 (4)," alisema Imelda.


Alisema kutokana na ukiukwaji wa kanuni hizo za Bunge wabunge wamekuwa wakitumia muda mrefu kutoa lugha za maudhi zisizo za staha ndani ya ukumbi huo huku akitolea mfano wabunge waliosikika wakisema maneno mbalimbali likiwemo la ‘funga mlango tupigane'," alisema Imelda.


Pamoja na mambo mengine alisema kumekuwepo na mahudhurio mabaya hasa kwa wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Alitolea mahudhurio ya kikao cha Aprili 16 mwaka huu ambacho wabunge 128 hususani wa CCM hawakuwepo wakati wa kujadili na kupitisha muswada wa sheria ya usimamizi wa mahakama 2011, kinyume na kanuni ya 143 (1).

Alisema kumekuwepo pia na uwasilishwaji wa miswada kwa hati ya dharura au kwa taarifa za muda mfupi kwani katika kikao kilichopita cha Bunge miswada mitatu kati ya mitano iliyowasilishwa katika kikao hicho imewasilishwa kwa hati za dharua pasipokuwa na sababu za msingi na kuwanyima wadau fursa ya kuchangia.


Aliitaja miswada hiyo kuwa ni wa Katiba, usimamizi wa mahakama na mabadiliko ya sheria mbalimbali.


Naye mratibu wa shughuli za Bunge, Merick Luvinga, alisema kuwa wananchi wanatakiwa kuwa makini kwa kuchagua mbunge atakayewawakilisha bungeni na si kwa maslahi yake binafsi kwani wabunge wengi huwatumia wananchi wao kama mhuri lakini wanapoingia bungeni husahau majukumu yao.

Katika hatua nyingine LHRC imetoa mapendekezo kwa Bunge na kuwataka wabunge kutumia fursa waliyopewa kuwawakilisha wananchi waliowachagua na kujadili maslahi ya wananchi na taifa bila kuingiza ushabiki na maslahi ya vyama katika hoja zinazotolea.
 
huyu ni Kunguru ...kwani kunguru ni mwoga , mwaribifu, asiyefuata taratibu na hana hata damu kuashiria uhai
 
Adiriki kukataa hata ushauri wa Spika mzoefu zaidi, Mzee Pius Msekwa, kwamba yafaa spika na naibu wake wote wakawa na taaluma ya uanasheria huku yeye hujibu eti 'SI LAZIMA'.

Ngoja wanasheria humo waje waanze kukuperekesha puta shauri yako na ubishi wako, mimi simo. Uspika ni zaidi ya kusimamia tu kikao na kuelekeza mkono kwa nani akazungumze na yupi atoke nje; yapo mambo kede kede na uwezo wa kuwa QUICK AND ACCURATE PROBLEM SOLVER zaidi ya kusimamia haki wakati wote ndani na nje ya mijadala.

Hebu angalia hadi viporo vya hoja ya Mhe Godbless Lema uamuzi wake hadi kubebwa mbele kwenda kutubana ki-muda huko mwezi wa sita; nini zaidi hapo, spika bado anasubiri wanasheria wa kukodi waje wakamtafunie mambo.

Mzigo kweli kweli jaama!!!
 
  • Thanks
Reactions: LAT
makinda anajuwa anachokifanya alishasema atasimamiya haki kutotenda haki kunaweza sababisha uvunjifu wa amani yawezekana anacho kifanya kwa sasa nikutikisa kibeliti yawezekana ameona kwamba kinaweza mlipukia
 
CDM = Umma wa watanzania bila kujali itikadi, maslahi ya umma
CCM = Ubinafsi, nafasi zao katika ubunge kupitia ccm bila kujali maslahi ya umma:whoo:
Wabunge wengine sijui wanachaguliwaje, labda kwa rushwa

CDM= Chama Dada cha Mafisadi

CCM= Chama Cha Masikini
 
makinda anajuwa anachokifanya alishasema atasimamiya haki kutotenda haki kunaweza sababisha uvunjifu wa amani yawezekana anacho kifanya kwa sasa nikutikisa kibeliti yawezekana ameona kwamba kinaweza mlipukia

Kama hajui wajibu wake au pengine keshausahau napenda nimkumbushe huyo Makinda kuwa "Anapaswa kujuwa kuwa dhamana aliyo pewa ni kulinda, kusimamia na kuhakikisha HAKI na misingi yote iletayo HAKI kwa mtu mmoja mmja na kwa Taifa zima inalindwa, inaimarishwa na kusimamiwa". Kama jukumu hilo anaona haliwezi namshauri ni bora akajivua gamba haraka ili kupisha watenda kazi wenye uwezo thabiti kuchukua nafasi yake.
 
huyu mama, yupo kama speaker kwa malengo ya wachache, kwa ufupi ni kwamba hiyo nafasi kwake ni maji marefu, atajutia nafasi hii, amezoea kuropoka kama mwanamipasho, tusubirie!
 
Back
Top Bottom