WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 956
Hasa wanawake. "I love you etc etc,kumbe moyo wake upo mbali kabisa,anataka ile 70,000/week!
Huyu sasa atakuwa hataki mpenzi bali yuko mawindo mengine kabisa.
Haya ya watu kuwa waongo yapo pia katika zile 'njia za kawaida' ambazo binadamu tumezitumia kwa miaka mingi kutafuta penzi na hakuna tofauti yoyote na wale wanaotafuta online. Ukisoma baadhi ya michango katika ile link ya BBC wako waliobahatika kupata true love online.
Kuna watu wanaona online dating kuwa ni kitu chema na unaweza kufanikiwa kumpata barafu wa moyo wako. Kwa maoni yangu, Online dating inaweza kuwa hatari kuliko kukutana na mtu ana kwa ana ambapo unawezafanya initial screening haraka kwa kumtizama, kumsikiliza na kumsoma mtu ukajua haraka kuwa una deal namtu gani.Online sana sana utasoma mistari ya mtu tu na mtu huyo anaweza kuwa sivyo unavyomfikiria.Niliwahi kuona sinema ambapo kila mmoja alikuwa anamdanganya mwenzie kuanzia jinsi yake( sex), anavyofanana hadi aliko, anachofanya kujipatia riziki n.k.Wengine wanakuwa sio watu wema - hasa ughaibuni ambako unaweza kukutana na serial killers! Kama ni online dating basi ni afadhali ukutane na watu wa kwenu kwa maana jamii yako, nchi yako etc.
Ni bahati nasibu - unaweza kula au kuliwa.