Lets Go JF!: Taifa Kwanza!

Apr 27, 2006
26,588
10,364
- Wananchi wote JF, twendeni sasa kuelekea kwenye mwisho wa Mbio zetu za Ubunge wa EAC: Tuwapigie Wabunge wa Jamhuri kuwaomba kura zao wapigie mabadiliko, wapigie Change! Wapigie Taifa kwanza na wapigie JF: Do something and be part of the change!

- Tunataka kuwaelmisha wananchi kuhusu EAC, kwamba Tanzania ni mwanachama wa EAC, Faida na hasara zake, tunataka kuhakikisha tutawakilisha mawazo na wananchi huko EAC yakitokea kwa wabunge wa Jamhuri ambao ni wawakilishi wao kikatiba, tunataka maoni yao wananchi kabla ya kutoa maamuzi ya aina yoyote huko EAC, na muhimu kuliko yote ni kulinda masilahi ya wananchi na hasa taifa letu katika EAC!

- Jana tulikuwa Arusha, na Zanzibar, leo in another 15 minutes tutakuwa Radio Uhuru Live kwenye maswali na majibu kwa hiyo kama una tatizo piga simu utuulize live, Jumatatu tutakua Clouds Radio na TV Live, NA THEN TUTAANZA SAFARI YA KUELEKEA DODOMA, kwa hiyo twendeni mbele people!, twendeni pamoja JF mbele zaidi!

- MUNGU AIBARIKI TANZANIA NA AIBARIKI JF!


William KUMEKUCHA!
 
Maswali yangu nimemtext mbunge wangu, ndo watakaowachagua! Hongera mdau
 
Tusaidie ni sababu gani zilizosababisha kuvunjika kwa EAC 1977 na kwanini unatumia rushwa Kama ushawishi wako kwa wabunge?
 
William, naona umebadilika baada ya kuingia kwenye mchakato wa kugombea ubunge, kila la heri mkuu tupo pamoja.
 
William, naona umebadilika baada ya kuingia kwenye mchakato wa kugombea ubunge, kila la heri mkuu tupo pamoja.

Le Mutuz! Baharia! FM ES ! Sauti za umeme! @new York , USA kafiri haachi asili
 
Yes, we need change with caution.
Nilifurahia sana mada yako hapa JF iliyoshauri tuwe makini na EA.
Wish you all the luck!
 
Le Mutuz! Baharia! FM ES ! Sauti za umeme! @new York , USA kafiri haachi asili

- Ndio kwanza tumemaliza mahojiano na Radio Uhuru, sasa tunaenda Karimjee kwenye maombolezo ya Mzee Mahundi, and then tutakwua Radio Clouds, mwendo ni mdundo hakuna kulala mpaka kieleweke, people twende pamoja JF mbele na Taifa kwanza!

WWilliam.
 
Kwanza ushaonesha dharau hapa kabla hujafika kokote siku ile umeleta hapa uzi wako ,tulipokuuliza maswali ukakatisha mazungumzo kuwa umechoka,
akumulikae mchana usiku atakuunguza!!
Mi kwa upande wangu sina heri na mtu yeyote wa ccm,
 
Mkuukwanza Hongera sana kwa hatua uliyofikia, mimi sina Tatizo na wewe kabisa mkuu,Tatizo langu liko CCM na kama unavyo jua Bunge la EA halina nguvu kama Bunge lanchi husika na kwa Tanzania kama unavyo jua masilahi ya CCM ndo yanaangaliwakwanza na si masilai sasa ya watanzania

- Unawezaukawa na aidea nzuri sana ila Hilo Bunge lenu si kitu kabisa na Bunge lenye lassay ni la Jamhuri ambao kuna CCM wengi sana,
- Na kulekumbukeni Wakenya ni wajanja sana kuliko hata wazungu na inavyo elekea hataMkuu wetu anaendeshwa na wakina Museven, mimi huwa nasikitika sana Hizi speedza EA community,

- Jumuiaya Ulaya ina miaka mingi sana kuliko hii yetu ila hata kujakufikia umoja wasarafu iliwachukua miaka mingi sana cha ajabu huku tunazungumzia shirikishowaka EU wenye miaka takribani 75 make walianza miaka ya 1958 huko,

- Mkuuhaya ndo ya kuangalia huko inakuwaje jumia haina hata miaka 15 waanze mambo yashirikisho wakati Jumuia ya Ulaya au hata ECOWAS hawajafikia huko na wana miakachungu nzima tangia waanze,

Kila laheri mkuu na mungu akutangulie huko ila endapo utashinda tunataka Vitendo na siuanze kuwatumikia mafisadi kwa kutetea masilahi yao EA

 
- Ndio kwanza tumemaliza mahojiano na Radio Uhuru, sasa tunaenda Karimjee kwenye maombolezo ya Mzee Mahundi, and then tutakwua Radio Clouds, mwendo ni mdundo hakuna kulala mpaka kieleweke, people twende pamoja JF mbele na Taifa kwanza!

WWilliam.
Mkuu naona unatumia tu... je ni wagombea wote ama ni team yako ya kampeni? Naelekea Dodoma huenda tukakutana Chako ni CHako manake pale ndipo huwa hata serikali ya Tanzania inatengenezewa. Kila la kheri nenda rudi salama umefanikiwa.
 
watoto wote wa viongozi kama wewe mtapita tu izo kampeni ni mbwembwe za za kusema siku izi watu wanawekana kwenye ajila, anamuweka ndugu yake na ndugu yake ana uwezo vile vile.
Haiwezekani miaka zaidi ya 20 ukae ugenini unaludi hata miezi mi5 haijaisha unapewa cheo.
Mi najua lazima upite nyie si matajili bwana.
 
Najua wazi TANZANIA inakuhitaji and Nawashauri wabunge Wote vijana please kuweni kwenye kampeni ya kumweka huyu kijana mwenzetu!

Najua umeiva, and you know where to press the button for things to start moving, wish you all the best... Inshaalah.
 
Watoto wa vigogo mnashangaza, kwanini mnakimbilia siasa. Leo mnajifanya "Taifa Kwanza" mkiishapata mnabadilika na mna fanya "CCM Kwanza" au "Sisi Kwanza"
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom