Mshana jr!Leo ni tar 14/9 Siku ya 258 bado siku 108
Matukio ya kitaifa
-Mwaka 1967 Tanzania iliacha rasmi kutumia fedha ya pamoja iliyokuwa ikitumiwa na Kenya na Uganda
-1990 Marehemu Horace Kolimba katibu mkuu wa ccm alitoa rai kwa ccm kuachana na dhana ya chama kushika hatamu na kuiachia serikali kufanya mambo kwa uhuru zaidi! Miaka 2 baadae mfumo wa vyama vingi uliruhusiwa rasmi Tanzania
Kimataifa
Mwaka 2003 serikali ya Guinea Bissau yapinduliwa na mkuu wa majeshi wa nchi hiyo! Rais aliyepinduliwa ni Kumba Yala. Mapinduzi hayo yasiyo na umwagaji wa damu yaliyotokana na rais kushindwa kuwalipa wanajeshi
1891ndio siku ilipigwa penalty ya kwanza kwenye soka huko uingereza
Google (Horace Kolimba v/s Julius Nyerere. Kuna mwandishi aliitwa Alex Kowe fictitious name.) Ni majibizano kati ya mwl na Kolimba mwaka 1994.Hapana kaka nitaipataje?
Huwa namkubali sana ToshNimeukuta huu Uzi juju naomba nirudi tar ya Jana 11/9/1987 hii ni Siku maarufu kwa ragae roots,mwanamziki mashuhuri wa mziki wa ragae PETER TOSH alipigwa risasi na kufariki shambulio lililofanywa nyumbani kwake na Rafiki yake kipenzi LEPO ,inaniuma saana
marekebisho kidoogo kwenye day counting, leo ni siku ya 272 bado siku 94 kumaliza mwaka!, otherwise nimependa sana huu uzi na ninaufuatilia, asante mshana JrLeo ni tar 28/9 ni siku ya 292 bado siku 74 kumaliza mwaka 2016
Kitaifa
Mwaka 2004 Rais wa Tanzania Benjamin mkapa awaapisha majaji wanne kwenye nafasi ya ujaji baadhi yao ni Jaji Mohamed Chande Othman, Jaji Kipenka Musa , Jaji Manento nk
1918 majeshi ya ujerumani yaliingia Tanzania kupitia Songea wakati vita ya kwanza ya dunia ikiendelea
1983 serikali ya Tanzania yakanusha taarifa za BBC kuwa bandari ya Dar es salaam inakimbiwa na wateja kutokana na ushuru mkubwa wa kutoa mizigo na mambo mengine pia
Kimataifa
1745 kuimbwa kwa mara ya kwanza wimbo wa taifa wa uingereza ukijulikana kama 'God save the Queen'
1970 kifo cha Gamel Nasser rais wa Misri wakati huo
Duuu hilo jibu la mwisho kiboko kumbe madikteta wote wanafanana majibu
Ahsante sana naomba pia ujikite sana kwenye historia ya TZ maana vijana wengi hatufahamu sana historia ya TanzaniaTar 29/9 ni siku ya 273 bado siku 93 kumaliza mwaka 2016
Matukio ya kitaifa
Mwaka 1911njia ya reli ya Dar-Tanga ilifika Moshi kwa mara ya kwanza na kufanya ijulikane kama Dar- Tanga- Moshi railways
Matukio ya kimataifa
Mwaka 1950 mashine ya kwanza ya kujibu sauti bila msaada wa mtu ilizinduliwa huko marekani (telephone auto answer machine)
1829 jeshi la kwanza la polisi lilizinduliwa huko London uingereza