Leo zamani (kabrasha la kumbukumbu)

5: Leo ni tar 13/9 Siku ya 257 bado siku 109 kumaliza mwaka 2016
Matukio ya leo kitaifa
-1990 katibu mkuu wa ccm marehemu Kolimba asema ukiritimba wa ccm umekwisha hivyo wana ccm wana uhuru zaidi wa kujiletea maendeleo bila misuli na ruhusa ya chama

Kimataifa
- 2000 ni siku ambayo taifa la Palestine lingetangazwa
-1997 mazishi ya mama Theresa wa Calkuta aliyefariki tar 5/9..hivi karibuni katangazwa mtakatifu
Hiyo 1990, swala la mwenyekiti lilichukuliwaje/lilipokelewaje?
 
Leo ni tar 14/9 Siku ya 258 bado siku 108
Matukio ya kitaifa
-Mwaka 1967 Tanzania iliacha rasmi kutumia fedha ya pamoja iliyokuwa ikitumiwa na Kenya na Uganda
-1990 Marehemu Horace Kolimba katibu mkuu wa ccm alitoa rai kwa ccm kuachana na dhana ya chama kushika hatamu na kuiachia serikali kufanya mambo kwa uhuru zaidi! Miaka 2 baadae mfumo wa vyama vingi uliruhusiwa rasmi Tanzania

Kimataifa
Mwaka 2003 serikali ya Guinea Bissau yapinduliwa na mkuu wa majeshi wa nchi hiyo! Rais aliyepinduliwa ni Kumba Yala. Mapinduzi hayo yasiyo na umwagaji wa damu yaliyotokana na rais kushindwa kuwalipa wanajeshi
1891ndio siku ilipigwa penalty ya kwanza kwenye soka huko uingereza
 
1473831342117.jpg
1473831347398.jpg
Huyu ndie rais Kumba laya wa Guinea Bissau aliyepinduliwa! Daima alipenda kuvaa hiyo kofia nyekundu isiyoendana na vazi la suti hata kwenye mikutano ya kimataifa
 
Leo ni tar 15/9 ni siku ya 259 bado siku 107 kumaliza mwaka 2016
Kitaifa:
Mwaka 1970 mwalimu aliteuliwa kuwa mgombea pekee wa urais Tanzania kwenye ukumbi wa Diamond jubilee ...aliyempendekeza ni Sheikh Karume kupitia vyama vya TANU na AFRO SHIRAZ PARTY
1979 mahakama ya rufaa yaanzishwa, hivyo ni baada ya kuvunjika kwa jumuiya ya Africa mashariki ambapo pia mahakama ya Afrika mashariki ilivunjika
Kimataifa
1963 Ahmed Ben bera aliapishwa kuwa rais wa Algeria , alipinduliwa mwaka 1965
1821 Guetamalla yapata uhuru
1821 Honduras nayo yapata uhuru
1821 Nicaragua yapata uhuru
1821 El Salvador yapata uhuru
1821 Costa Rica yapata uhuru
 
Leo ni tar 16/9 ni siku ya 260 bado siku 106 kumaliza mwaka 2016
Matukio ya kitaifa
Mwaka 1992 mwalimu Nyerere alisema ili nchi iwe na demokrasia ya kweli ilihitaji vyama vichache vya siasa
1993 baraza la habari lapokea tuzo ya uandishi bora kimataifa wakati huo baraza lilikuwa chini ya Jenerali ulimwengu
Kimataifa
Mwaka 1736 kufariki dunia mwanafizikia fahrenheit..huyu ndio mgunduzi wa kipimo joto kwa kutumia zebaki (mercury themometer)
Uhuru wa Autralia Mexico na Malaysia 1963
 
Leo ni tar 17/9 Siku ya 261 bado siku 105 kumaliza mwaka 2016
Matukio ya kitaifa
Mwaka 1972 Mathias Joseph awa askofu wa kwanza mtanzania jimbo la Dodoma
1962 Ana Libunga ateuliwa mkuu wa kwanza wa wilaya mweusi nchini Tanganyika

Kimataifa
1828 kifo cha Chaka mwanazuoni wa kizulu
1978 kifo ya rais wa Angola Augutino Neto
 
Leo ni tar 18/9 ni siku ya 262 bado siku 104 kumaliza mwaka 2016
Kitaifa
Dr. Living stone avumbua ziwa Nyasai then) linalotenganisha Tanzania na Msumbiji na malawi
Kimataifa
1474172203810.png

Nimeweka hii screenshot kwa makusudi kwakuwa hili tukio ni la tar kama ya leo mwaka 1862 lakini hapo inasoma tarehe ya jana
 
Watu wengi wanamtazama Samwel Doe kwa ubaya tu lakini naomba niwajulishe kuwa katika nchi inayo ongoza kwa wingi wa maraisi ni Liberia lakini katika hao wote ni Doe pekee ndie aliekuwa mzawa halisi wengine wote ni wageni waliopandikizwa na Marekani,uchumi kipindi cha Doe ulipanda na mpaka leo ukienda Monrovia majengo makubwa ya serikali yalijengwa kipindi cha Doe.Doe alitolewa kwa mpango maalumu ili Helen aingie madarakani na aliefanya kazi ni Chales Teila ila alipomtoa akajitangaza yeye kuwa rais,na ndio maana na yeye alitolewa I'll azima ya kumuweka mama madarakani,someni ka historia
Mkuu ingekuwa ni vema kama hako kahistoria ungetuletea humu
 
Leo ni tar 19/9 ni siku ya 263 bado siku 103 kumaliza mwaka 2016
Matukio ya kitaifa
-Mwaka 1967 taasisi ya kuratibu na kusimamia bei za vitu(tume ya bei) yaanzishwa rasmi
-Mwaka 1995 wagombea 4 wa kiti cha urais Tanzania washiriki kwenye mdahalo wa kisiasa uliofanyika kilimanjaro hotel
Benjamin mkapa CCM
Augutino Lyatonga Mrema NCCR-MAGEUZI
John momose cheo UDP
Prof Ibrahim Haruna Lipumba CUF
Matukio ya kimataifa
-Mwaka 1956 mkutano wa kwanza wa waandishi na wasanii weusi wafanyika Paris ufaransa
-Mwaka 1893 wanawake waruhusiwa kupiga kura kwa mara ya kwanza huko New Zealand
 
Leo ni tar 20/9 Siku ya 264 bado siku 102 kumaliza mwaka 2016
Matukio ya kitaifa
Mwaka 1974 Joha Akida achaguliwa kuwa kuwa mwakilishi kwenye mkutano wa kimataifa
Kimataifa
Mwaka 1984 majeshi ya marekani yashambuliwa mjini Beirut
 
Back
Top Bottom