leo yamemkuta jamani!!!!!!!!!!

ndo hivyo mkuu,yaani jamaa hata nikimpigia simu swali la kwanza ni kama nimepata nafasi ya usalama wa taifa au njia ya kumnasua mchumba atoke kwenye hiyo kazi

ha haha , vijana bana. huyu jamaa anatafuta kazi ya usalama wa taifa, hakuna jipya hapo.
lakini mwambie akumbuke kuwa taifa lenyewe ni kama halipo vile , sasa huo usalama wa nini ?
 
asidanganyike, hiyo habari ya miaka sita haina ukweli wowote. anatakiwa afikirie nje ya mduara. kufunga ndoa ni sehemu tu ya mapenzi. kwani nani hajui sheria za huko majeshini?? lakini mbona wana waume, wana wake, na wana watoto kabla ya muda waliowekewa?

na kwa taarifa zaidi ni kuwa hata weza pata kazi kama ya huyo binti kwa sababu yeye anafuata mwanamke na si kazi- hawata mkubalia. hapo ni huyo mama ndo anaona rafiki yako hafananiii kwahiyo ametumia kigezo cha kazi.
ushauri ninao weza kumpa
1. aongee na huyo dada kuwa wao wataishi kama mke na mume ila ofisini ndo mwanaume hatapata haki za mume. mama akizaa atapata haki za watoto kutoka ofisini. ndoa ofisini itatambulika baada ya hiyo miaka sita
2. akikataa anatakiwa kukubali hiyo hali, hili la kusema amesubiri siku nyingi halitakiwi ktk kuchukua maamuzi ya maisha. amesubri siku nyingi , lakini hajui ni siku ngapi zimebaki, na zina uzito gani ukilinganisha na hizo zilizopita
nashukuru sana nitajaribu kumshauri
 
ha haha , vijana bana. huyu jamaa anatafuta kazi ya usalama wa taifa, hakuna jipya hapo.
lakini mwambie akumbuke kuwa taifa lenyewe ni kama halipo vile , sasa huo usalama wa nini ?
sasa sijui atanielewa,labda atacheka tu
 
kwani huyo my girlfriend wake yuko kwenye field au yuko ki-tech? Kama huwa anatoka na kwenda kwenye mission mbalimbali basi aachane naye. Nalog off
 
ndo hivyo mkuu,yaani jamaa hata nikimpigia simu swali la kwanza ni kama nimepata nafasi ya usalama wa taifa au njia ya kumnasua mchumba atoke kwenye hiyo kazi
Ni pm tumuumbue huyu mwanaizaya, hakuna kitu kama hicho.. ama la atafute msichana mwingine. Huyu dada angekuwa anamhitaji jamaa yako huyo, basi kuna namna ingefanyika kumu-accomodate jamaa huyo. otherwise ni uzushi.
 
wikiend ilikuwa ngumu kwa rafiki yangu jamani wana mmu
Jamaa alikuwa na mchumba wake na wakati amemaliza chuo ikatokea nafasi ya usalama wa taifa na huyo dada aakapewa huo mchongo na akaenda kusoma kwa miezi kadhaa na wakiwa na mipango ya kufunga ndoa baada ya binti kurudi na walikuwa wanapendana sana.
Nyongo imeingia leo baada ya kuambiwa na wazazi wa binti kuwa taarifa walizonazo ni kuwa binti kulingana na nafasi ambayo ameandaliwa harusiwi kufunga ndoa na mtu ambaye si usalama wa taifa labda mpaka baada ya miaka sita na binti ana miaka 26 kwa sasa na mvulana ana miaka 32.
rafiki yangu amechanganyikiwa maana alimsubiri binti kwa muda mrefu na walipanga kufunga ndoa mwaka kesho 2012.
ameniomba ushauri ili kama aweze kusaka nafasi ya usalama wa taifa au aweze kumsubiri hiyo miaka 6 na kinachomuuma ni kwamba mchumba wake inabidi ajilengeshe kwa mtu yeyote ambaye ni usalama wa taifa au wamchagulie.
wana mmu huyu jamaa yuko njia panda hajui afanye nini,mpaka nimemuonea huruma.
naombeni msaada wenu wa mawazo angalau nipate kufkishia maana nimekwama!!

mpe pole huyo bwana. Hakuna ukweli wowote hapo, huyo dada anamdanganya. Kwanza nafasi za usalama wa taifa ni kupeana ndugu, hawatangazi na hata ukituma maombi (write in) kamwe hautaitwa, huyo dada ana mwanaume aka mpenzi wake ndo alimpa mchongo wa kuingia. Nasema hivyo kwani nina ushahidi wa watu 5 wameoa au kuolewa na mtu wa usalama. Wanachofanya ni vetting tu. Si kuna watu wa usalama hapa jf? Mpeni ukweli, kwani siku hizi si mnajitangaza mpate maujiko? Na si mmeingia kwa jina la anko au kaka na mnafanya kazi za magamba? Huyo dada anajua huyo kaka hawezi kuingia usalama wa taifa kwani hana anko hata kama ana elimu nzuri na huyo aliyemuingiza tiss atamuwekea kauzibe, tunawajua.
 
wikiend ilikuwa ngumu kwa rafiki yangu jamani wana mmu
Jamaa alikuwa na mchumba wake na wakati amemaliza chuo ikatokea nafasi ya usalama wa taifa na huyo dada aakapewa huo mchongo na akaenda kusoma kwa miezi kadhaa na wakiwa na mipango ya kufunga ndoa baada ya binti kurudi na walikuwa wanapendana sana.
Nyongo imeingia leo baada ya kuambiwa na wazazi wa binti kuwa taarifa walizonazo ni kuwa binti kulingana na nafasi ambayo ameandaliwa harusiwi kufunga ndoa na mtu ambaye si usalama wa taifa labda mpaka baada ya miaka sita na binti ana miaka 26 kwa sasa na mvulana ana miaka 32.
rafiki yangu amechanganyikiwa maana alimsubiri binti kwa muda mrefu na walipanga kufunga ndoa mwaka kesho 2012.
ameniomba ushauri ili kama aweze kusaka nafasi ya usalama wa taifa au aweze kumsubiri hiyo miaka 6 na kinachomuuma ni kwamba mchumba wake inabidi ajilengeshe kwa mtu yeyote ambaye ni usalama wa taifa au wamchagulie.
wana mmu huyu jamaa yuko njia panda hajui afanye nini,mpaka nimemuonea huruma.
naombeni msaada wenu wa mawazo angalau nipate kufkishia maana nimekwama!!

kwenye red hapo mkuu

Hivi jamaa amejiuliza kwa nini kaambiwa hilo na wazazi wa binti badala ya kuambiwa na binti mwenyewe maana kwa vyovyote vile mtu huwa karibu zaidi na mpenzi wake kuliko na 'wakwe watarajiwa'??!
Nikiamini kuwa wazazi hao sio usalama so hizo taarifa kama zipo ni classified wamepataje!? kwa mfano kama nao wamepewa na mtoto wao ambaye alizipokea au hata kuzisikia kitambo tu wakati akianza kozi labda akakaa nazo pekeyake kwa muda wote huo ambao jamaa yako amekuwa akisubiri, hata kama wewe utasema wako poa na wanapendana,mi naona kinyume chake, naona kuna tatizo katika mawasilliano baina yao ambalo kama ni kweli, kwenye mapenzi ndilo tatizo kubwa kuliko mengine yote coz mengine huwa ni matokeo tu ya hilo!
Labda kama kuna taarifa inapungua katika maelezo yako, vinginevyo jamaa kaliwa, asipoteze muda wake bure!
 
Ampige mimba kama isipoingia atajua kuwa kweli huyo ni usalama wa taifa la magamba,
ikiingia huyo si usalama wa taifa.
 
Umemaliza! Hawa hata usalama wa whatever uliwaruhusu kuoana inaidi rruksa ya kuazaa wapewe na wazazi. Isisahau ratoiba ya mechi inabidi wazazi wa mdada wahusike!
kwenye red hapo mkuu

Hivi jamaa amejiuliza kwa nini kaambiwa hilo na wazazi wa binti badala ya kuambiwa na binti mwenyewe maana kwa vyovyote vile mtu huwa karibu zaidi na mpenzi wake kuliko na 'wakwe watarajiwa'??!
Nikiamini kuwa wazazi hao sio usalama so hizo taarifa kama zipo ni classified wamepataje!? kwa mfano kama nao wamepewa na mtoto wao ambaye alizipokea au hata kuzisikia kitambo tu wakati akianza kozi labda akakaa nazo pekeyake kwa muda wote huo ambao jamaa yako amekuwa akisubiri, hata kama wewe utasema wako poa na wanapendana,mi naona kinyume chake, naona kuna tatizo katika mawasilliano baina yao ambalo kama ni kweli, kwenye mapenzi ndilo tatizo kubwa kuliko mengine yote coz mengine huwa ni matokeo tu ya hilo!
Labda kama kuna taarifa inapungua katika maelezo yako, vinginevyo jamaa kaliwa, asipoteze muda wake bure!
 
Mwambie huyo rafiki yako asijisononeshe! Ndio thawabu ya kujionyesha kwa mwanamke umezimia sana hata pumzi huwezi kuvuta bila yeye! Kama wengi walivo sema huyo si riziki na ashukuru mungu imetokea sasa hivi kabla hajamuoa! Angemuingizia machungu ya ajabu! Sasa hivi mwambie avute pumzi ndeeeeeefu, halafu asonge mbele, atafute ki-mwana kingine fresh kilicho wazi kwake! Wataishi na atashukuru mungu alimwacha 'the so called mwanafunzi usala wa taifa.
 
Back
Top Bottom