Leo tujifunze namna ya kuomba maji kwa lugha za makabila tofauti tofauti

vukani

JF-Expert Member
Dec 30, 2009
245
165
Ndugu wana JF, leo nataka tujifunze namna ya kuomba maji kupitia lugha za makabila tofauti tofauti.

Hivi karibuni nilikwenda Wilayani Babati, kule nikakutana na watu wa kabila moja liitwalo Wasandawi, nilikuwa na kiu, lakini nilipata tabu sana kuomba maji maana lugha pekee ambayo nilitakiwa kuwasiliana nao ilikuwa ni Kisandawi, basi ilikuwa kaazi kweli kweli.

Kipare:
Nighenja mazi ya kunwa=Nisaidie maji ya kunywa

Kinyawezi:
Nalilomba minze kakunwa=Naomba maji ya kunywa

Kichaga:
Ngikundi Mringa= Naomba maji ya kunywa

Kingoni:
Nitangatilai manji mlongo wangu=Naomba maji ya kunywa ndugu yangu

Kimasai:
Njaaghe Ngare= Naomba maji ya kunywa

Kihehe:
Ndisuka Ululenga= Naomba maji ya kunywa

Kimeru:
Ngitelewa Mringa= Naomba maji ya kunywa

Kijaluo:
Miaa pi= Naomba maji ya kunywa

NIMEPATA MSAADA KWA MJUVI WA LUGHA YA KIJAPANI

Kijapani:
Kwanza inabidi useme:- 1. kao nodo itai - nina kiu
2. mizu nomu itai - nina hamu ya kunwya maji
Ukisha sema moja kati ya hayo hapo juu ndio unaunganisha na lingine kati ya haya hapa:-
1. omizu kudasai
2. omizu chodai
3. omizu onegai shmasu
Kihaya:

Ninshaba amaizi= Naomba maji ya kunywa


Kimanda:
Nisuka masi gakunywa=Naomba maji ya kunywa

Kiswidi:
Kani jag be att får ett glas vatten=Naomba maji ya kunywa

Kisimbiti:
Ndasabha amanshe ghukunywa=Naomba maji ya kunywa

Waluguru:
Nigaile machi ya kunyuwa=Naomba maji ya kunywa

Kizulu:
ng'icela amanzi=Naomba maji ya kunywa

Kimatengo:
Naa masi ga kuunywa=Naomba maji ya kunywa

Kidachi,
Ik wil water om te drinken, au Kan ik heb water te drinken **'Wil' tamka vil, na 'Water' tamka 'Vata=Naomba maji ya kunywa

Haya wengine mtajazia hapo.
 
Back
Top Bottom