Leo Nimeshangaa sana

chuchunge

JF-Expert Member
Aug 17, 2007
212
154
Wana JF,
Hope mu wazima,leo asubuhi nikiwa natokea kwangu maeneo ya njiro,nilipita nje ya nyumba ya Mheshimiwa Fatma Makongoro Nyerere anayojenga karibu na General Tyre,Wafungwa walikua ndio wanapanga concrete tiles chini asubuhi ya saa 2,Ninajiuliza kwa maadili ya viongozi ni sahihi kutumia wafungwa kwa kazi kama hizo especially ya mtu mkubwa serikalini anyejua sheria za nchi?
 
Wafungwa wanafanya kazi zozote za kijamii tena sio kwa viongozi tu bali hata kwa raia wa kawaida. Ukiwahitaji nenda Magereza utalipia pesa kisha utapewa kulingana na mahitaji yako, hivyo sio makosa hata kidogo.
 
Kama amelipia sio tatizo, ila kama hakulipia ndio tatizo. wafungwa wanapaswa kuzalisha badala ya kukaa na kula bure bila kuzalisha. Kwanza wanatakiwa kufanya kazi za kijamii kuliko kukaa bure.
 
Ni sahihi kabisa, wewe pia ukiwahitaji kwa kazi yoyote nenda kaonane na mkuu wa gereza afu atakuambia ulipe kiasi gani kulingana na kazi unayotaka kufanyiwa.
 
Mtoa mada hajui kwamba hata yeye akitaka kujenga watakuja tu.Tena hawana uswahili kama mafundi mafundi wa uswazi! Pia wanajenga vizuri sana.ukishalipia magereza hakuna tatizo.
 
Wafungwa ni labor iliyopo tayari muda wowote!..nadhani kuna namna ya kulipia and then wanaletwa eneo lako la kazi!
 
tatizo lako ni
1.. wafungwa kuwa nje ya gereza kabla ya saa mbili asubuhi? Au
2.. wafungwa kufanya kazi za ujenzi kwa mtu binafsi? Au
3.. wafungwa kufanya kazi za ujenzi kwa mtu binafsi ambaye ana wadhifa serikalini? Au
4.. wivu wa kimaendeleo? Au
5.. HUJUI?
 
Hakuna tatizo lolote hapo.Hawa wanatumika kama vibarua .Ukiwahitaji unaenda magereza na gharama zao zipo chini ,pia wanafanya kazi yenye uhakika.
 
Back
Top Bottom