Leo ni Siku ya Demokrasia

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,551
Leo ni Siku ya Kimataifa ya Demokrasia. Maadhimisho yanafanyika hapa kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja. Maadhimisho haya yameandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania TCD. Maadhimisho yameanza kwa maandamano. Swali ni "Kwenye nchi zenye demokrasia ya kweli, Jee Tanzania nasi tumo humo?.
 
tunajivutata, watu wa political science wanasema bado tuna Infant democracy kwamba bado transion yetu ni poor..hatuna political acceptance and tolerance..
 
Mgeni rasmi ni Mwenyekiti wa TCD, Pius Msekwa. Vyama vyote vya siasa vimealiwa. UDP imewakilishwa na Mwenyekiti wake Taifa Mzee John Memosa Cheyo. Chadema yupo Victor Kimesera. CCM, Cuf , TLP, PPT na DP pia vimewakilishwa. Vyama vingine kikiwemo NCCR, Mhh,...
 
Hivi, hii siku ilianza kuadhimishwa lini? Maana Chadema wanasema imeanza kuadhimishwa baada ya wao kutoa "List of Shame" September 15, 2007 na wao leo walipaswa kuadhimisha miaka miwili ya list of shame lakini wamelalaaaaaaaaaa. Wameshindwa kutumia nafasi hii kujibeba.
 
Hivi sasa Msekwa anahutubia. Awali Mzee Kimesera katika salaam za Chadema alikumbushia List of Shame na kusisitiza political tolarance iliyopo ni ya uwongo na unafiki.
 
........ Swali ni "Kwenye nchi zenye demokrasia ya kweli, Jee Tanzania nasi tumo humo?.

Tupo kwa kuwa kwetu sisi demokrasia ni kuchagua na kuchaguliwa, na ile uchaguliwe lazima uwe na chama cha siasa.
 
Sisi tunaiga tu demokrasia, Tazama kule Pemba mambo yalivyo, Nani anaweza kupaza sauti yake na kuona kuwa mambo kama yale hayatokei hapa Tanzania Mbona watu wananyiwa demokrasia yao kule. Leo ni Siku ya kukemea mambo yote yanatokea kule Pemba
 
Mzee Cheyo alisisitiza nchi moja, vyama tofauti vyenye sera tofauti kwa lengo moja la kushika dola. akasema tutabanana hapa hapa mpaka kieleweke. CUF wamemaka sana kuhusu vurugu ya undikishaji Pemba na kuuliza ni demokrasia gani ya vifaru na kutupiana mabomu ya machozi?.
 
Msekwa amezungumzia historia ya vyama vingi nchini na kusisitiza ni serikali ya CCM enzi za Mzee Rukhsa aliporuhusu mfumo wa vyama hivyo, hivyo CCM inataka upinzani wa kweli ushamiri.Msekwa ameukejeli upinzani uliopo bungeni na kusema ni upinza legelege ambao hauna uwezo wa kuendesha serikali kivuli.Alifafanua lengo la serikali kivuli kwenye bunge la vyama vingi, ni pale inapotokea hoja za serikali zimeshindwa bungeni, Waziri Mkuu anajiuzulu na serikali kivuli ndio inatwaa madaraka ya kuongoza serikali, akauliza kwa serikali kivuli ilipo bungeni, kutokana na uchache wao hata uwezo wa kuunda serikali kivuli hawana.Pia alizungumzia siasa za Zanzibar na kukiri ni mgogoro, tangu uchaguzu mkuu wa 1995, Zanzibar ilikuwa mgogoro, ule wa 2000 pia ni mgogoro, wa 2005 ni mgogoro tena na ujao wa 2010, dalili za wazi zimeshaanza kujitokeza, hali inayoashiria Zanzibar haina political tolarance ya mfumo wa vyama vingi.Msekwa alimalizia kwa kutoa changamoto vyamo vyote viwahamasishe wagombea wanawake na kuwapitisha kwa wingi kwenye uchaguzi wa 2010.Baada ya hotuba ya Msekwa, ndio ukawa mwisho wa maadhimisho ambapo MC ni mtangazaji Eshe Muhidin aliyesema na yeye atagombea ubunge mwaka 2010, japo hakusema kupitia chama gani.
 
Kweli wanaadhimisha democrasia,manake kule Pemba washaanza democrasia yao ya kuwanyima haki yao raia wa kule na kuwatesa. Kwa democrasia hii nitakubali.
 
Back
Top Bottom