Leo ndio Siku Aliyokufa Brenda Fassie, May 9 - Yule alikuwa Mwanasiasa?

Cable

Member
Apr 20, 2012
25
4
Wadau,

Samahani inaweza ikawa sio mahali pake ila nimesikia leo kupitia Arusha Mambo habari hizi za kumbukumbu ya kifo cha Brenda Fassie wa South Africa na kuwa Mzee Mandela na Rais wa sasa wa Afrika Kusini walikwenda kumjulia khali hospitalini kabla ya kifo chake, nikajiuliza hivi yule dada alikuwa Mwanaharakati, Mwanasiasa au Mwanamuziki?

Ila mchango wake kwa ukombozi wa Afrika ya Kusini ulikuwa mkubwa sana na utakumbukwa kwa vizazi vingi vijavyo, Je Tanzania tuna wanamziki wanaoweza kusaidia harakati za sasa za kuleta mabadiliko katika nchi au wao bize na nyimbo za mapenzi?

Arusha Mambo ambao leo wanapiga nyimbo za SA the best wamenifanya niwaze jambo hili,, hapa tunao watu wa mifano ya Brenda Fassie, Chaka Chaka, Miriam Makeba, Oliver Mutukuzi..... ambao waliimba kukosoa na kutaka mabadiliko katika nchi zao???
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom