Malalamiko na Ushauri kuhusu madai ya utapeli kwenye mtandao wa KUPATANA

Kun Jr

JF-Expert Member
May 29, 2013
700
360
Nimetapeliwa laki na themanini muuzaji wangu akapotea hewani moja kwa moja. Sijui nifanyeje hapa nilipo najipooza tu.

Dah! nimeingia cha kike bila kujijua..
========

Malalamiko mengine zaidi...
Habari zenu WanaJF,

Leo ndo nimeelewa kwamba kupatana.com ni mtandao wa kitapeli baada ya ndugu yangu kutapeliwa laki moja ambayo nimemkopesha mimi.

Jamaa yangu alikuwa na shida ya laptop used ndo akaingia kupatana kuangalia kama anaweza kupat.ndo akapata apple macrobook kwa sh 200,000/= mpya kabisa kwa mujibu wa tangazo.akawa ameipenda kafanya mawasiliano na muuzaji ambaye yuko Iringa yeye Dodoma.

Wakakubaliana atume advance ambapo pesa nyingine atamalizia akpokea mzigo kwa njia ya bus ila cha kustaajabsha pesa imetumwa mpaka sa hivi hamna mawasiliano kati ya mteja na muuzaji.

Ushauri kwa operators wa KUPATANA

Ningependa ku bring this up kwa operators wa site ya kupatana.com kwamba kuna watu wanaiua ile site na kuondoa credibility yake kwa kuwa idad ya matapeli wamekua wengi kupatana.com. Sa sijui hawa matapeli wamewa notice na kuwachukulia hatua gan coz at the end of the day wao nao pia wana-lose visit kwenye site yao.

NB: Najua kwamba wao wametoa precaution kuwa usitumie mtu pesa bila kuuona mzigo wako na pia najua hawahusiki kwenye sales zozote.

I think operators wa kupata ni vyema wangekua wanazifuta ads za hao matapeli coz waziwazi na mtu asiemjanja anaweza kunaswa kwenye mtego kirahisi.

I also recommend kwamba waweke option ya ku-report tangazo lolote la kitapeli ili wao waweze kutambua hayo matangazo na kuyafuta pia hata kufuta accounts za hao matapeli..

Au wadau mnaonaje?!
 
Nadhani wamiliki wa kupatana wanahaja ya kureview selling and buying process za kupatana maana watu wanatapeliwa sana. Au watoe elimu ya kutosha.

Mimi kidogo nitapeliwe Gari, Mungu mkubwa roho iligoma kabisa kufanya biashara na wale watu ingawa nilikuwa nashida na pesa. Kuna tapeli anajifanyaga wa jombe, huyo kaliza wengi.
 
Wa iringa... amesha liza watu sanaaa
 
Kama kichwa kinavyosema hapo juu nimetapeliwa laki na themanini muuzaji wangu akapotea hewani moja kwa moja sijui nifanyeje hapa nilipo najipooza tu
dah nimeingia cha kike bila kujijua

Kwani kupatana si wameji register na Brela, hao ndio wa kukomalia kwa nini wanaruhusu matapeli kutumia mitandao yao bila ya x-check credibility za muuza bidhaa/mali?
 
Kama kichwa kinavyosema hapo juu nimetapeliwa laki na themanini muuzaji wangu akapotea hewani moja kwa moja sijui nifanyeje hapa nilipo najipooza tu
dah nimeingia cha kike bila kujijua

Umekuja Dar siku za karibuni kutoka Mkoani sio?
 
shtuka wewe...usiwe zoba kihivyooo..we unatoaje pesa bidhaa hujaikamata mkononi...mi nilishawahi kuiona Toyota Raum eti 4m muuzaji kidada flani matata (uzuri nilienda na wife) tulipotoka pale wife akaniambia aisee huyu dada CHANGU na hiyo gari usinunue tena...tukamalizie nyumba yetu MBWENI...tushahamia tumeachana na kodi zenu za majungu na TRA.
 
Huwa nashangaa sana watu wanaotoa pesa katika biashara za kwenye mitandao kabla ya kuona bidhaa physically.

Kabla hujanunua kitu kutoka kwenye mitandao kama kupatana hakikisha unaiona bidhaa physically au kama uko mbali na muuzaji na hauna uwezo wa kumtuma mtu unayemfahamu akaione bidhaa husika badala yako achana na hiyo biashara mara moja haijalishi una shida kiasi gani na hicho kitu.
 
Na vipi kwa wale wanaoagiza magari nje kupitia mitandao?
 
Na vipi kwa wale wanaoagiza magari nje kupitia mitandao?
Siku hizi hiyo mitandao/makampuni yanayojihusisha na ununuzi wa magari mengi yao yana mawakala hapa nchini. Licha ya hivyo ni vizuri kusoma Sera za kampuni/mtandao husika endapo aina yeyote ya utapeli itatokea au mteja kupokea mzigo usiokidhi makubaliano waliyo afikiana na muuzaji.
 
shtuka wewe...usiwe zoba kihivyooo..we unatoaje pesa bidhaa hujaikamata mkononi...mi nilishawahi kuiona Toyota Raum eti 4m muuzaji kidada flani matata (uzuri nilienda na wife) tulipotoka pale wife akaniambia aisee huyu dada CHANGU na hiyo gari usinunue tena...tukamalizie nyumba yetu MBWENI...tushahamia tumeachana na kodi zenu za majungu na TRA.

mke wako kamjuaje kuwa huyo dada Changu?? something is wrong somewhere
 
Kupatana wako vzr tu.Wanaoibuwa ni u wege wao tu.Mi nimeuza gari kupatana na sikutoa funguo na docs kabla mkwanja haujaingia bank na sipokei hela nusu
Yani me nawiki siku hata kumi hazizidi nimetoka kuuza gari kupatana bila longo longo wala mtu kati WA kumgawia hela ya mteja kwani mteja sahihi kaja katest gari tukaenda bank akadeposit mzigo tukaenda kukabidhiana gari na documents,kuhusu maelezo kupatana wametoa warning kabisa usinunue kitu au kulipia bidhaa bila kuiona sasa kama mtu anakurupuka bila kusoma masharti huyo kataka mwenyewe,vinginevyo kupatana bonge LA msaada kwa e-business ya bongo.
 
Kama kichwa kinavyosema hapo juu nimetapeliwa laki na themanini muuzaji wangu akapotea hewani moja kwa moja sijui nifanyeje hapa nilipo najipooza tu
dah nimeingia cha kike bila kujijua
Pole sana kijana. Ugeni wa online business ndio umekufanya upigwe. Ila usiwaze piga moyo konde. Kwa kupatana huwezi kuwabana kwasababu kwenye terms na conditions wamekuandikia kuwa usikubali kutoa hela kabla hujaiona bidhaa.

Kuna jamaa yangu aliibiwa Pikipiki na mteja kutoka kupatana. Pia kuna mmoja ilikua kidogo aibiwe gari Caldina mwishoni akaibiwa simu na mteja alietaka kununua gari yake.
 
Back
Top Bottom