Leo ndio ilizaliwa Tanzania

Kwenye Passport za Wazanzibari kwenye pahala pa kuzaliwa pameandikwa Zanzibar, kwa sababu kama Zitto alivyoeleza Zanzibar linatambulika kama lilikuwa taifa.
inashangaza kuona pahala pa kuzaliwa kwa Watanzania wengine hapaandikwi TANGANYIKA ijapo kuwa napo palikuwa ni taifa.

muungano umeua identity ya Mtanganyika, na labda ilikuwa rahisi kufa kwa Identity hiyo kwa sababu taifa la Tanganyika lilikuwapo kwa mda mdogo zaidi kuliko taifa la Zanzibar.

au labda identity ya mtanganyika imekufa kwa sababu watu hawakuitaka tokea hapo mwanzo, haikuwa deal kwao kwa vile wapo wachaga, wahaya, wazanaki, wagogo.... nk.

muungano wetu kwa kweli haupo equal katika mambo mengi. unahitaji marekebisho ya hali ya juu.
 
Na mimi nafikiri structure ya Muungano tuliyo nayo sasa hivi inakidhi haja. Hakuna sababu za msingi ni kwa nini tuwe na serikali tatu wakati kuna kila sababu za kutokubalika kuwa na serikali moja.

Jambo moja la kuzinganitia ni kwamba nchi haiwi nchi kwa sababu ya idadi ya watu au sehemu ilipo kijiografia. Nchi inakuwa nchi kwa sababu ya sabaabu ya historia ya mapambano ya kujitambua (a history of struggles for self identification).

Kuna makosa makubwa na madogomadogo ambayo tunahitaji kuyarekibisha ili kuimarisha zaidi huu muungano wetu. Baadhi ya makosa haya na hatua za kuchukua katika kuyarekibisha ni kama hizi:

i) Kwa kiasi kikubwa Zanzibar imebaki jina na mamlaka yake kama nchi yameporwa na kumezwa sana na Muungano. Kwa mfano, leo hii wazanzibar hawawezi kujichaguliwa viongozi wao bila mkono wa watu wa Tanganyika (sipendi sana hili la kujiita Bara-nitaeleza sababu baadaye). Sote tunajua kwamba, kwa mfano, kama wazanzibari wangekuwa na uhuru kamili wa kuchagua viongozi wao Karume asingekuwa mgombea wa CCM 2000 na wala asingekuwa Rais wa Zanzibar. Vilevile, sote tunajua kwamba kama wazanzibar wangekuwa na uhuru kamili wa kuchagua viongozi wao, leo hii CCM isingekuwa madarakani huko Zanzibar. Sote tunajua kabisa kuwa bila maguvu ya viongozi wa muungano kutoka Tanganyika Abdul Wakil na Karume mdogo wasingekuwa marais wa Zanzibar. Tunajua pia kwamba isingkuwa matumizi ya ovyo ya maguvu ya viongozi wa muungano, Komando Salmin Amour angekuwa Rais wa wamu moja tu huko Zanzibar. Naamini hili ni jambo mojawapo ambalo linawaumiza sana wazanzibar kichinichini.

ii) Kila siku na hatua kwa hatua tumeendelea kuwapokonya wazanzibar nafasi muhimu katika serikali ya Muungano. Kitendo cha kuondoa nafasi ya Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais lilikuwa ni kosa kubwa na lilitia doa la kutisha kwa nafasi ya Zanzibar katika muungano. Tena tulizidi kuwatukana wazanzibar kwa kumfanya Rais wao kuwa cabinet member. Ajabu hata yeye naye alikubali na anaendelea kukubali! Hata hivyo angakataa vipi wakati anajua bila ya hao jamaa zake wa muungano kamwe asingekuwa mgombea wa CCM wala Rais wa Zanzibar? Naamini wanzibar wengi hawakupenda Rais wao anyang'anywe nafasi muhimu katika serikali ya muungano na wala hawapendi Rais wao apewe hadhi ya uwaziri kama waziri mwingine kwenye cabinet ya muungano. Lakini ndiyo hivyo tena kama kawaida ya CCM wanaendelea kulia ndani ya mioyo yao na kuongea pembeni, hawataki kuyaweka haya mambo hadharani na kuyasema kwenye vikao vyao husika.

iii) Tunafanya makosa kufikiri kwamba Tanzania bara ni matajiri sana na kwamba Zanzibar haiwezi kujiendesha kiuchumi bila msaada wa serikali ya Muungano. Huu ni upofu wa kihistoria. Ukweli ni kwamba kabla ya Muungano wa 1964, Zanzibar ilikuwa na GDP kubwa kuliko Tanganyika na hata per capital income ya mzanzibari ilikuwa kubwa kuliko ya mtanganyika. Kwa kifupi, standard living ya wazanzibar ilikuwa juu zaidi kuliko ya mtanganyika kabla ya muungano. Kilichotokea baada ya muungano ni utekwaji nyara wa raslimali na njia zingine za kiuchumi za wazanzibar kwa kuziamishia katika muungano.

iv) Kosa moja ambalo Mwalimu Nyerere alilifanya personally ni kufuta neno Tanganyika baada ya kuanza kutumika serikali ya muungano. Alichofanya Mwalimu katika hili ni kujaribu kufuta historia ya mapambano ya uhuru kwa watanganyika. Wakati mwingine inapofika 9 December huwa najiuliza hivi tunasherehekea kitu gani hasa? Sisi tulipigania uhuru wa Tanganyika lakini tunapoenda kusherehekea siku ya uhuru hiyo 9 Desemba tunasherehekeaga kitu gani hasa wakati hata kutamka neno Tanganyika tunaona ni dhambi au utovu wa nidhamu au hata kukosa uzalendo? Kimsingi alichofanya Mwalimu Nyerere ni sawa na alichofanya Mobutu kwa kufuta Democratic Republic of Congo na kuita Zaire (naomba nieleweke mapema kwamba siwafananisha Nyerere na Mobotu isipokuwa katika hili). Lakini ukisoma historia ya DRC huoni popote ni wapi jina Zaire lilitoka zaidi ya mapenzi yake Mobutu. Vivyo hivyo nikisoma historia ya Tanganyika na Tanzania, sipati picha hili neno Tanzania Bara lilitoka wapi hasa zaidi ya kwamba yalikuwa ni mapenzi ya mwalimu Nyerere mwenyewe na kwa sababu alizozijua mwenyewe.

Katika kuimarisha zaidi muungano wetu, ni muhimu tuchukue hatua kadhaa zikiwemo hizi:

i) Lazima turudi kwenye misingi ya muungano. Mambo ya Zanzibar tuwaachie wazanzibar na mambo ya muungano yabaki kuwa ya muungano. Mambo ya muungano yanapaswa kuwa machache na hayana haja ya kwenda zaidi ya defence and security, foreign affairs na currency. Niliwapongeza sana wazanzibar, kwa mfano, walipoamua kuwa na mfumo wao tofauti kabisa wa elimu mwaka juzi na naendelea kuunga sana mkono juhudi za ZFA kuhakikisha kwamba Zanzibar inashiriki katika michezo ya kimataifa kama nchi.

ii) Lazima turudishe hadhi ya Zanzabar katika muungano. Hii ni pamoja na kuwa na makamu wa wawili wa rais-Zanzibar na Tanganyika. Ili kuepuka gharama za liserikali likubwa, hatuna sababu ya kuwa na nafasi ya waziri mkuu katika serikali ya muungano. Tuache undumila kuwili wa kutaka kuwa republic and at the same time tunataka tuwe parliamentary system of governance. Kama tumeamua kwamba Rais wetu ndiye atakuwa mkuu wa nchi na serikali, hatuna haja tena tuwe na mkuu mwingine wa serikali bungeni. Ni uhuni mtupu kwamba nje ya bunge Rais ndiye mkuu wa cabinet na ndiye anaye chair mikutano yote ya cabinet, halafu tukiwa bungeni waziri mkuu ndiye anakuwa mkuu wa serikali. Kwangu mimi nafasi ya waziri mkuu haina haja and it is a position that we can do without. Badala yake, tuimarishe nafasi ya makamu wa urais na tunaweza kabisa kuamua makamu wa rais wote wawili wawe wabunge na kwa kuwa ni wasaidizi wa rais mojawapo ndiye awe mkuu wa serikaki bungeni.

iii) Lazima tuweke historia ya nchi sawasawa kwa kurudisha jina la Tanganyika katika matumizi ya kawaida. Na hapa siongelei kuanzisha au kurudisha serikali ya Tanganyika kwa sababu hatuhitahi kuwa nayo. Naongelea kurudisha tu matumizi ya neno Tanganyika katika maisha yetu ya kila siku na katika vitabu vyetu ya kiraia na kihistoria. Muhimu zaidi, ifikapo 9 Desemba, tuache unafiki, tuende uwanja wa taifa kwa uhuru kabisa na kifua mbele tukienda kusherehekea uhuru wa Tanganyika na sio Tanzania au Tanzania Bara maana hakuna kitu kama hicho. Tarehe 26 April vilevile sote tutoke kifua mbele na kwa uhuru kabisa bila kujisonya tukasherehekee muungano wetu.
 
Kitila... Niliposoma article ya Kyoma I only had one sentence in my mind... kwanini Tanzania bara kusiitwe Tanganyika? na wewe naona umeona kitu hicho hicho... nakubaliana nawe.
 
Kitila... Niliposoma article ya Kyoma I only had one sentence in my mind... kwanini Tanzania bara kusiitwe Tanganyika? na wewe naona umeona kitu hicho hicho... nakubaliana nawe.

MM

Ni hivi; population na eneo linaloifanya taifa la Tanzania kwa kiasi kikubwa imaanishe Tanzania bara!

Kwa nini;

1. Leo hii Zanzibar ikijitenga na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania... kipande kilichobaki kitaendelea kustahili kuitwa Tanzania. bila hata kurudishiwa jina la awali la Tanganyika na bado ika-make sense.

2. Leo Tanzania Bara ikijitenga na Zanzibar... Itakuwa ni miujiza Zanzibar ku-retain jina la Tanzania.


Kwa maana nyingine tukubali kwamba wale wanaopendekeza serikali tatu ni wale wanaozifikiria nchi hizi mbili Zanzibar iliyokuwa Tanganyika zina ukaribu wa Eneo, Watu, rasilimali. Kitu ambacho sio kweli.
 
(iii) Lazima tuweke historia ya nchi sawasawa kwa kurudisha jina la Tanganyika katika matumizi ya kawaida. Na hapa siongelei kuanzisha au kurudisha serikali ya Tanganyika kwa sababu hatuhitahi kuwa nayo. Naongelea kurudisha tu matumizi ya neno Tanganyika katika maisha yetu ya kila siku na katika vitabu vyetu ya kiraia na kihistoria. Muhimu zaidi, ifikapo 9 Desemba, tuache unafiki, tuende uwanja wa taifa kwa uhuru kabisa na kifua mbele tukienda kusherehekea uhuru wa Tanganyika na sio Tanzania au Tanzania Bara maana hakuna kitu kama hicho. Tarehe 26 April vilevile sote tutoke kifua mbele na kwa uhuru kabisa bila kujisonya tukasherehekee muungano wetu.

Nakuunga mkono kwa sababu hii...

1. Penye Tanzania Bara pana Tanzania Visiwani hakuna Tanzania bara na Zanzibar -- hii ilikuwa mrengo wa kuelekea Serikali moja nadhani ndio iliyokuwa nia. yaani nchi zote mbili zilikuwa zife kabisa... Zanzibar na Tanganyika lakini watawala wetu hawaelekei kuipenda hii... hivyo haitatokea. then we should opt for option 2. below

2. Penye Zanzibar pana Tanganyika. Kwa kuwa tuna-embrace Zanzibar then tu-embrace Tanganyika kwa ajili ya historia tu sio mabadiliko ya uongozi
 
Naomba kuuliza.
Hivi Z'bar si tayari wanashiriki katika mashindano ya mpira wa miguu ya Afrika kama nchi? Je, katika mashindano hayo nyimbo za Taifa huwa zinapigwa kabla ya mchezo na bendera za Taifa hupererushwa. Kama Z'bar inashiriki kama nchi huwa wanapeperusha bendera ipi na nyimbo ipi ya Taifa la Z'bar ambayo hupigwa?

Natanguliza shukrani.
 
Kyoma, PM me your number
Mkuu Zitto salam!Tunashuru kwa uwepo wako tena!Tulikuwa tukikutafuta sana wakati wa ile hoja ya madini.But nafikiri ni majukumu pengine yalikubana!Anyways its good to see that you're around!Karibu US pia!
 
Wakuu mbona habari hii inazidi kuwa nzito pale kwenye jina tu wakati hoja ya Muungano wenyewe ni nzito kuliko majina. hakuna mtu aliyeibatiza tanganyika kuitwa Tanganyika isipokuwa mkoloni. Zaire wamebadilisha majina weee na mpaka kesho suluhu ya jina haiwezi kupatikana kwani kila mtawala huitazama nchi hiyo kwa kutazama imani yake na hasa imekuwa tunatumia muda mrefu sana kuzungumzia mgawanyo wa Mkoloni ktk ku rule nchi zetu (devide and rule) badala ya kutazama mambo muhimu yanayotuweka hapa.
Jamani niite Mkandara, Bob, Msilanga. Kishimba yote haya hayawezi kupotosha who I am!..as a fact jina nalolipenda mimi linaweza kuwa kivutio zaidi na motisha kwangu..
Hivyo kama kuna kuvunjika kwa Muungano tunaweza beba jina lolote lile tunalolipenda sisi Bara ama Visiwani after all, initially Zanzibar ilikuwa including Lamu na Mombasa. Kama sikosei ni ktk makubaliano ya viongozi wa Hizbu na Kenyatta yaliyofanyika huko Kenya ndio yaliigawa mipaka mipya kwa makubaliano ya kumrudisha Sultan..
Haya hicho kisiwa cha Unguja pekee kimekuwa kikiitwa Zanzibar mara nyingi ktk mazungumzo ya watu na Pemba imesahaulika kwa kiasi kikubwa sana na sidhani kama inafahamika nje ya mipaka yetu. Zaidi ya hapo Tanganyika pia ilikuwa na mipaka hadi Burundi na Rwanda kabla ya hawa watawala wakoloni hawajagawana nchi zetu kutona na kushindwa kwa Mjarumani vita ya kwanza..
Kwa hiyo wakuu haya maswala ya jina isiwape taabu sana.. Bara inaweza kuitwa Bongo na ikaendelea kujulikana kama Jamhuri na kisibadilike kitu..
Tuzungumzie mambo mazito anayotuangushia Zitto, Kyoma na Kamundu nadhani suluhu ya Muungano wetu ni muhimu zaidi ya majina.
 
Wakuu mbona habari hii inazidi kuwa nzito pale kwenye jina tu wakati hoja ya Muungano wenyewe ni nzito kuliko majina. hakuna mtu aliyeibatiza tanganyika kuitwa Tanganyika isipokuwa mkoloni. Zaire wamebadilisha majina weee na mpaka kesho suluhu ya jina haiwezi kupatikana kwani kila mtawala huitazama nchi hiyo kwa kutazama imani yake na hasa imekuwa tunatumia muda mrefu sana kuzungumzia mgawanyo wa Mkoloni ktk ku rule nchi zetu (devide and rule) badala ya kutazama mambo muhimu yanayotuweka hapa.
Jamani niite Mkandara, Bob, Msilanga. Kishimba yote haya hayawezi kupotosha who I am!..as a fact jina nalolipenda mimi linaweza kuwa kivutio zaidi na motisha kwangu..
Hivyo kama kuna kuvunjika kwa Muungano tunaweza beba jina lolote lile tunalolipenda sisi Bara ama Visiwani after all, initially Zanzibar ilikuwa including Lamu na Mombasa. Kama sikosei ni ktk makubaliano ya viongozi wa Hizbu na Kenyatta yaliyofanyika huko Kenya ndio yaliigawa mipaka mipya kwa makubaliano ya kumrudisha Sultan..
Haya hicho kisiwa cha Unguja pekee kimekuwa kikiitwa Zanzibar mara nyingi ktk mazungumzo ya watu na Pemba imesahaulika kwa kiasi kikubwa sana na sidhani kama inafahamika nje ya mipaka yetu. Zaidi ya hapo Tanganyika pia ilikuwa na mipaka hadi Burundi na Rwanda kabla ya hawa watawala wakoloni hawajagawana nchi zetu kutona na kushindwa kwa Mjarumani vita ya kwanza..
Kwa hiyo wakuu haya maswala ya jina isiwape taabu sana.. Bara inaweza kuitwa Bongo na ikaendelea kujulikana kama Jamhuri na kisibadilike kitu..
Tuzungumzie mambo mazito anayotuangushia Zitto, Kyoma na Kamundu nadhani suluhu ya Muungano wetu ni muhimu zaidi ya majina.
True..ufuatao ni baadi tu ya utitiri huo wa mabadiliko ya majina..
Austria-Hungary - Austria, Hungary, Slovakia, etc.
Pashtun - Afghanistan
Persia - Iran
Mesopotamia and Assyria - Iraq
Dahomey - Benin
Burma - Myanmar
Cymru - Wales
Éire - Ireland
Nippon and Nihon - Japan
Goryeo - Korea
Lan Xang - Laos
Cyrenaica - Libya
Nyasaland - Malawi
French Sudan - Mali
Middlebrook Islands or the Brook Islands - Midway Islands
Doclea or Zeta - Montenegro
German Southwest Africa - Namibia
Pelew - Palau
Lusitania - parts of Portugal and Spain
Soviet Union - Russia
Ar Rabi and Arabia - Saudi Arabia
Temasik or Simhapura - Singapore
Aram - Syria
Tanganyika and Zanzibar - Tanzania
Siam - Thailand
Byzantine Empire - Turkey
Ellice Islands - Tuvalu
Rhodesia - Zimbabwe and Zambia


 
Tusisahau pia kujiuliza ni mambo gani hasa yalikuwa kiini halisi cha muungano wetu ili tuweze kujua kuwa kama.."Yale yanayotutenganisha ni mengi kuliko yale yanayotuunganisha" or the other way around..pamoja na consequences za kuwa ama kutokuwa na muungano!Due to that..there is a few i would like to share..We cannot start it without mentioning the name of the father of our Nation..The late Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Nyerere's regional East African legacy was somewhat mixed. Although he was once committed to
creating an East African Federation, his socialist ideals clashed with his East African ideals. As he struggled to create socialism in his own country, he had to create barriers against free movement of capital, labour, and resources in and out of Kenya and Uganda. Socialist planning in one country proved to be incompatible with an open-door Pan-East-African policy.
Have African scholars done enough research on whether socialism in one country is compatible with pan-African integration among several countries?
On the other hand, Nyerere's Tanganyika did form a union with Zanzibar. This remains the only case in Africa of previously sovereign states uniting into a new country-and surviving as one entity for more than three decades. What used to be sovereign Tanganyika and Zanzibar became the United Republic of Tanzania in 1964.
Nyerere strengthened the union when he united the ruling Afro-Shirazi Party of Zanzibar with the ruling party of Tanganyika to form the new Chama cha Mapinduzi, the Party of the Revolution. Will this union of Zanzibar and Tanganyika survive Nyerere's death? Once again have African scholars done enough to find out why Africans find it so hard to unite? Has Nyerere's political behaviour ruined it all? We can all see that one side is disssatisfied with the union where as the side that bears the burden supports it!
Then Waungwana tuwekeeni hapa wazi kuwa yepi hasa ni manufaa ya muungano?
 
Nyerere strengthened the union when he united the ruling Afro-Shirazi Party of Zanzibar with the ruling party of Tanganyika to form the new Chama cha Mapinduzi, the Party of the Revolution. Will this union of Zanzibar and Tanganyika survive Nyerere's death? Once again have African scholars done enough to find out why Africans find it so hard to unite? Has Nyerere's political behaviour ruined it all? We can all see that one side is disssatisfied with the union where as the side that bears the burden supports it!

This is not true!.. Nyerere alivunja vyama vyote vya Zanzibar na kuunda CCM chama kimoja akawaweka wananchama wa vyama vyote ndani ya chama kimoja....Ndio tukawaona kina Babu, Seif Hamad na Salim na kadhalika wakishika nafasi za Uongozi ktk chama.
Hatua hii pamoja na kuwa ya Kidikteta lakini ilifanya kazi safi ya Muungano huo hadi vyama vingi vilipoanza kujitokeza upya. tatizo la Zanzibar vyama hivi vilirudi kwa mgawanyiko wa imani ile iliyotangulia na aliyoivunja mwalimu..
Tatizo kubwa la mwafrika demokrasia inasimama kwa makundi ya makabila, race ama dini.Haya maneno ya Mrengo yametumika weee lakini trust me hakuna mwafrika anayeelewa kitu mathlan tofauti ya CCM na Chadema ktk mrengo. Very few leaders if not all Tanzanians wanaweza kujieleza nini tofauti kati ya Conservative ama Progressive.
 
This is not true!.. Nyerere alivunja vyama vyote vya Zanzibar na kuunda CCM chama kimoja akawaweka wananchama wa vyama vyote ndani ya chama kimoja....Ndio tukawaona kina Babu, Seif Hamad na Salim na kadhalika wakishika nafasi za Uongozi.
Hatua hii pamoja na kuwa ya Kidikteta lakini ilifanya kazi safi ya Muungano huo hadi vyama vingi vilipoanza kujitokeza upya. tatizo la Zanzibar vyama hivi vilirudi kwa mgawanyiko wa imani ile iliyotangulia na aliyoivunja mwalimu..
Tatizo kubwa la mwafrika demokrasia inasimama kwa makundi ya makabila, race ama dini.Haya maneno ya Mrengo yametumika weee lakini trust me hakuna mwafrika anayeelewa kitu mathlan tofauti ya CCM na Chadema ktk mrengo. Very few leaders if not all Tanzanians wanaweza kujieleza nini tofauti kati ya Conservative ama Progressive.
Kwani jina CCM si lilitokana na mapinduzi hayo ya zanzibar ama?Je tunawaenzi wananchi na maslahi yao ama sera na ilani za vyama vya kisiasa? ama tunataka tu tujisikie vizuri?
Its time to look both sides of the coin!Kama muafaka ukifikiwa..then fine!Tuendelee na muungano ambao una manufaa kwa pande zote!This is no more an idealistic issue!Its more like a reality!
It is time to discuss on what issues excactly brings us together vs the ones that separates us!Then we weigh in as to which outweighs which and the consequences of the choice..then we negotiate..then we reconcile..and finally we might reach the deal!
 
This is not true!.. Nyerere alivunja vyama vyote vya Zanzibar na kuunda CCM chama kimoja akawaweka wananchama wa vyama vyote ndani ya chama kimoja....Ndio tukawaona kina Babu, Seif Hamad na Salim na kadhalika wakishika nafasi za Uongozi.
Hatua hii pamoja na kuwa ya Kidikteta lakini ilifanya kazi safi ya Muungano huo hadi vyama vingi vilipoanza kujitokeza upya. tatizo la Zanzibar vyama hivi vilirudi kwa mgawanyiko wa imani ile iliyotangulia na aliyoivunja mwalimu..
Tatizo kubwa la mwafrika demokrasia inasimama kwa makundi ya makabila, race ama dini.Haya maneno ya Mrengo yametumika weee lakini trust me hakuna mwafrika anayeelewa kitu mathlan tofauti ya CCM na Chadema ktk mrengo.
Very few leaders if not all Tanzanians wanaweza kujieleza nini tofauti kati ya Conservative ama Progressive
.
Progressives ni wale ambao wako willing kubadilisha sheria za nchi hata kama zinakinzana na maslahi ya vyama vyao!Progressive ni kuwa on "THE PEOPLE'S SIDE"
 
Hapana mkuu Mapinduzi yalitokea January 12, mwaka 1964, Muungano April 24 mwaka 1964 na CCM ilizaliwa miaka 13 baadaye - tahere 5 Feb 1977, kama sikosei.
 
Hapana mkuu Mapinduzi yalitokea January 12, mwaka 1964, Muungano April 24 mwaka 1964 na CCM ilizaliwa miaka 13 baadaye - tahere 5 Feb 1977, kama sikosei.
Ohoo!Sasa tuko pamoja kuwa muungano ulikuwa na mshike mshike toka kitambo tu lakini badala ya kutafuta the real solution..wakaingiza itikadi ili kuwaaminisha wale waliokuwa na mawazo tofauti!
CHAMA CHA MAPINDUZI MANAKE HALISI IPI HIYO?Naomba jibu tafadhali!
 
Zanzibar received its independence from the United Kingdom on December 19, 1963, as a constitutional monarchy under the sultan. On January 12, 1964, the African majority revolted against the sultan and a new government was formed with the ASP leader, Abeid Karume, as President of Zanzibar and Chairman of the Revolutionary Council. Under the terms of its political union with Tanganyika in April 1964, the Zanzibar Government retained considerable local autonomy.

On April 26, 1964, Tanganyika united with Zanzibar to form the United Republic of Tanganyika and Zanzibar. The country was renamed the United Republic of Tanzania on October 29, 1964.
To form a sole ruling party in both parts of the union Nyerere merged TANU with the Zanzibar ruling party, the Afro-Shirazi Party (ASP) of Zanzibar to form the CCM (Chama cha Mapinduzi-CCM Revolutionary Party), on February 5, 1977. The CCM was to be the sole instrument for mobilizing and controlling the population in all significant political or economic activities. He envisioned the party as a "two-way street" for the flow of ideas and policy directives between the village level and the government. On April 26, 1977, the union of the two parties was ratified in a new constitution. The merger was reinforced by principles enunciated in the 1982 union constitution and reaffirmed in the constitution of 1984.

Tumwage hoja kwa hoja!
 
Jmushi1,
Mkuu nachojaribu ni kuweka record sawa sio kujenga hoja yoyote ile.
Kama umesoma vizuri maelezo yangu yaliyotangulia utaona kwamba nilisema toka Muungano wetu na Zanzibar mwaka 1964 hadi kuzaliwa kwa CCM 1977, kulikuwa bado matatizo yapo na kama habari uliyoiandika ilivyosema kwamba Nyerere alijenga nguzo za Muungano huo kwa kuunda chama kimoja cha CCM. Baada ya kuundwa CCM toka 1977 hadi majuzi kabla ya vyama vingi hatukuwa na matatizo ya Muungano kabisa. nachokataa toka kwa mwandishi huyu ni pale aliposema Nyerere aliuganisha chama cha Afro Shiraz na TANU kuunda CCM..
Hapo ndipo niliposema sio kweli kwa sababu CCM iliundwa ni pamoja na kuvivunja vyama vyote vya Upinzani vikiwemo Hizbu na Umma party na ndio maana ktk CCM mpya tuliweza kuwa na viongozi wengine toka Hizbu ndani ya CCM.
Kwa hiyo mwandishi aliposema:- To form a sole ruling party in both parts of the union Nyerere merged TANU with the Zanzibar ruling party, the Afro-Shirazi Party (ASP) of Zanzibar to form the CCM (Chama cha Mapinduzi-CCM Revolutionary Party), on February 5, 1977.

Hii inapotosha ukweli na ndio nia yangu kuweka record straight na sii kupinga hoja yako..
 
The other factors that we also cannot ignore like i said before is the one to do with The late Mwalimu Nyerere's legacy!
Its fair enough to say that we should look at our constitution!That has been my pledge all the times here at jf!Looking at other factors..i would like to touch on some maters that are directly linked to our union well being together with the legacy of our previous presidents as well as the current one!
I will touch some constructive points derived from the Mkapa's reign!
Benjamin Mkapa's term of presidency ended just after the October 2005 elections. As an acknowledged disciple of Julius Nyerere (the first president of the United Republic of Tanzania), he has vowed to safeguard and maintain the Union of Tanganyika and Zanzibar.
His really fears was that he will be the president that "lost" Zanzibar. That is apparent if CUF wins presidential elections in Zanzibar in 2005. It has been an open policy of CUF to reform the Union government structure in a manner that seems suspicious to ardent Union supporters like Mkapa.

We actually saw in 2000, how Mkapa reacts when he sees the Union in danger. Back then a big rift had emerged between Salmin Amour (the then outgoing president of Zanzibar) and the rest of CCM clashed heads both in Zanzibar and the Tanzania Mainland. Salmin Amour was very bitter as many of his initiatives had been crashed to ground by his party counterparts mainly in the Tanzania Mainland.
He was exceptionally bitter in the infamous "matchbox incident", in which he said those attempting to stop Zanzibar from joining the Organization of the Islamic Conference (OIC) were "shaking the matchbox" in vain.
He meant to say that no one could stop him from making Zanzibar join OIC! He was devastated when the then Tanzania Mainland CCM and government leaders stopped him. He vowed to make changes to the structure of the Union to prevent similar embarrassments in the future. For that reason, he planned to have his ardent supporter and Chief Minister, Dr. Mohammed Gharib Bilal, as the Zanzibar presidential candidate in the 2000 elections.
Dr. Bilal won 44 out of 74 (60%) votes cast by the members of a special committee of CCM in Zanzibar. Abdisalaam Issa Khatib was second with 13 (18%) votes. Amani Abeid Karume was third with 9 (12%) votes.

The final Zanzibar presidential candidate was to be decided by the CCM central committee in the Tanzania Mainland. Salmin Amour actually wanted to send only one name, that of Dr. Bilal, to the central committee to ensure his nomination. He failed to do that.
He was devastated when Mkapa and other CCM leaders crashed his choice and nominated Abeid Amani Karume instead, the third winner, as the 2000 CCM's presidential candidate for Zanzibar.

That is a clear example of what Mkapa did to prevent any possible shake-up of the Union status quo in a bid to safeguard the Nyerere's Union legacy.
It is the same reason that will make Kikwete to disallow a possibility of the Union shake-up under his watch as the Tanzanian presidency elections nears in 2010! He will do whatever it takes, to prevent CUF from getting in power in Zanzibar, just like how it happened before when the Zanzibar government was allowed to play foul in the 2005 elections.
As a matter of fact, it is widely believed that Nyerere in 1995 blessed Salmin Amour's wrongful snatching off of the presidency from Seif Sharif Hamad, the CUF's candidate. Kikwete like Mkapa who was the respectful disciples of Nyerere, might just do the same as his predescor in 2005.
 
Back
Top Bottom