Leo naomba nimtetee mheshimiwa raisi wangu ndugu J M Kikwete

This is none sense...wengi wamechangia ila hata kipengele cha kwanza kuhusu Kenya hakina maana, sijui hiyo ni political science ya wapi.. Wakoloni waliwaachia Wakenya majengo tena ni Nairobi to na barabara ni majuzi tu wameweza kuwa sambamba na sisi kwenye miundo mbinu mbali na hapo Nairobi kwenye pot holes za kutosha, huwezi kulinganisha barabara za Tanzania 2005 na barabara za Kenya...na hayo majengo wakoloni waliacha yana nini cha maana? viwanda vingi Kenya ni vipya sema tu imekuwa ni base ya wakoloni walipokuwa EA na kingine ni J. Kenyatta International airport ambayo hiyo pia ni mali ilikuwa robbed kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki. Wakoloni walichukua madini yetu? Kenya wana madini kama sisi..hizi zote ni facts Tanzania na JK ameshindwa kabisa tena mara 50 Mkapa amefanya kazi kwa mfano reforms za TRA, barabara zote mnazosikia zimeunganisha nchi ni Mkapa alianza na uchumi ulikuwa umekaa sawa mbali na ufisadi unaosemwa kafanya Mkapa. JK is total failure na unaposema maamuzi ya Chama vs Serikali, eti Waziri wako anafanya upuuzi unaogopa chama kitavunjika?? kina Kibaki waliacha vyama na kujiunga kwingine, maslahi ya Taifa kwanza then Chama hiyo ndiyo formula... utendaji pembeni na siasa pembeni, ndiyo maana na hoja kuwa Waziri si lazima awe mwanasiasa, tunataka watu intelligent siyo wanasiasa wanakuwa mawaziri hao si watendaji.
 
Well, bwa mdogo umejitutumua, ila kumtetea mkuluunahitaji kuwa na hoja nzito sio rahisi kiasi hichi, uko shallow kinoma dogo.Kwa mfano tunapoongelea swala la ukubwa wa nchi kama kigezo cha kushindwakuendelea, umeniudhi sana tena sana, kwani nchi yetu ni jangwa?! tuna ardhibikra yakutosha yenye rutuba tosha, lakini wapi kilimo kinatushinda, madinije?mito? maziwa? bahari? mbuga za wanyama? mlima kilimanjaro? dogo jipange,unatia aibu wasomi wenzako, kajipange tafadhali.

Kuna lawama nyingine hatustahili kuzitoa, kuhusu madini nshaelezea. Kuhusu kilimo, je wewe una shamba? Kama jibu ni ndiyo shamba lako lina ukubwa gan? Umeajiri watu wangapi kwa mwaka unapata faida gani kutoka kwenye hilo shamba? Unatumiaje maji yanayokuzunguka katika kilimo? Na umewaelimisha wangapi juu ya kilimo bora na cha kisasa?
Kama hauna shamba ni kwa nini hauna shamba wakati aridhi ya kutosha ipo?
 
Hapo unasoma science ya siasa na uongozi wa umma! Ungeishia darasa la saba usingefaa hata kufagia barabarani!
 
Unafahamu kuwa mwanzoni British ndiye aliyekuwa ana teknolojia ya juu kuliko nchi zote za ulaya? unafahamu kuwa aliwahi kufanya maoesho ya teknolojia yake na kualika nchi nyingine kwenda kushuudia? anatambua kuwa tokea wageni wale walimuibia mbritish teknolojia yake? na je unatambua kuwa huo ndo ukawa mwanzo wa kufichwa kwa siri za teknlojia? na je unatambua kuwa ni vigumu sana na kwa kuifundisha nchi nyingne teknolojia yake labda kwa makubaliano maalumu? na je unatambua kuwa nchi za magharibi haziwezi kupromote maendeleo yako kwa kukupatia teknolojia yao kwa sababu wanaamini na wewe utaendelea na watakosa nafasi ya kukunyonya? Na je unatambua kuwa mwl Nyerere alikuwa anapewa teknolojia na nchi za kijamaa wakati ule wa vita baridi ya ubapari na ujamaa? Na je unatambua kuwa cku hizi ujamaa haupo tena? NADHANI UMENIELEWA, SASA TUFANYAJE KUIKOMBOA TZ YETU?

Kumbe na wewe unayafahamu so what to do?
Nadhani tungerudi kulekule kwanza kwenye Azimio la Arusha na kufuata siasa yetu ya UJAMAA NA KUJITEGEMEA then tunaweza kufanya hizo special agreemants tukapata Technology kutokt mataifa Mengine kama China na Russia sio lazima yale ya Magharibi kwani mbona Wachina na Warusi wanayapa mataifa mengine teknolojia hadi ya Nuke? Siasa ya kimagharibi inaishia kwenye uwekezaji ambao in Turn hauna tija yoyote kwetu. Kwani tusipochimba madini tukatafuta hiyo Technology kwanza hatutaipata? Leo hao waochimba wanatupatia 3% kwa mali yetu ni ujinga gani huo au ni tamaa? All in all bila technology hakuna development sidhani kama hata historia inaonesha development ambayo imetokana na uwekezaji nadhani ni Industrial which purely is technology in base.
 
Vp kama kanda ya ziwa ingekuwa nchi unadhan ingekuwa maskini kama ilivyo sasa?
Vp kama Pwani nayo ingekuwa nchi?Tanzania mikoa inagawana umaskini na utajiri wake, pili ni vigumu kwa central government kucontrol the whole state, wasimamizi wa local government si sawa na wa central government, maendeleo ya nchi kiujumla unategemea usimamizi na umakini wa central government na sio local government.
unanchoongea na dhani labda ni kutokana na uelewa mdogo au vipi,kwanza

  • kanda ya ziwa kuwa nchi au pwani sio kigezo cha kuwa tajiri maana hiyo ni mikoa tu au kanda,na wakuu wake huteuliwa na rais wa nchi maana ndio kapewa power hiyo kwa hiyo hata kama kanda ya ziwa ingekuwa nchi na rais wake akawa kikwete ingekuwa masikini hivyo hivyo maana iko chini yake sasa,
  • kwa kawaida wananchi hawachagui rais ili rais yule aende tra akakusanye kodi za bidhaa,au akaendeshe katapila ajenge barabara au abebe chaki aingie darasani afundishe watoto ,hapana hatuchagui rais ili ayafanye yeye,anachaguliwa ili ateue timu imara itakayoweza kutekeleza yote kwa vitendo,kwa hiyo ubora wa rais yeyote utauona kwenye timu yake inavyotekeleza yale anayoiagiza timu yake ifanye,ndio maana tumempa mamlaka ya kuteua mawaziri,wakuu wa mikoa na wengine wengi ili hao watekeleze yale rais amepanga kufanyia wananchi,wanaposhindwa wale sio wao ni rais maana aliomba ridhaa ya kuliongoza taifa kumbe hajui timu aipange vipi kwa hiyo RAIS ndio msaliti namba moja kwa yote unayoona mikoa ilivomasikini
 
Kuna lawama nyingine hatustahili kuzitoa, kuhusu madini nshaelezea. Kuhusu kilimo, je wewe una shamba? Kama jibu ni ndiyo shamba lako lina ukubwa gan? Umeajiri watu wangapi kwa mwaka unapata faida gani kutoka kwenye hilo shamba? Unatumiaje maji yanayokuzunguka katika kilimo? Na umewaelimisha wangapi juu ya kilimo bora na cha kisasa?
Kama hauna shamba ni kwa nini hauna shamba wakati aridhi ya kutosha ipo?
acha kuchosha watu,mwalimu wa shule ya msingi hapa dar anaweza kuwa na shamba la mahindi tunduma au rukwa au singida hata kama yanagawiwa bure?hiyo nauli ya kwenda kuangalia shamba kila mwezi atatoa wapi? na ili apate faida ya hicho kilimo inabidi aje auzie dar maana yake apakie kwenye gari toka tunduma alete dar atawezaje kwa mtaji gani?watu wamenunua tu viwanja wa laki 6 au 7 hapo bagamoyo na unakuta mtu anamiaka mitatu hajaenda maana mtu anafanya kazi ya laki mbili tatu hapaq kila tarehe 20 ikifika anaangalia saa na kalenda kila baada ya nusu saa ili tarehe moja ifike,fikiri kabla ya kunena
 
asante kwa kutuchangamsha kaka nitajibu hoja zako kwa kifupi sana.

1. kuhusu kufananishwa na majirani zetu ni kwamba ukubwa wa tz ni advantage na siyo dis. kwa sababu tz kwa ukubwa
wake ina rasilamali kubwa kuliko majirani zake kwahiyo kosa ni kufananisha tz na majirani ni kwamba tz ilibidi iwe na
maendeleo makubwa kuliko majirani kwa sababu ya resources nyingi tulizo nazo.

2. kuteua marafiki. ndio maana kuna kitu kinaitwa benefit of doubt huwezi kuwahukumu watu kuwa hawafai kama
hujawahi kuwa hawafai kwahiyo basi la msingi ni kubadilisha badala ya kuchagua majina unayoyafahamu inabidi
uwe na usahili ambao utazingatia yafuatayo elimu, ujuzi, uzoefu na uadilifu. hata kama mtu humjui kabisa lakini
kama anaweza kutimiza vigezo hivyo basi anafaa haijali ni kabila gani wala anatoka wapi kwani watu hawa wote
wana record zao huko walikotoka na kwa kutumia usalama wa taifa utazipata zote.

3. kuchelewa kufanya maamuzi ni wekaness kubwa sana ya JK na sababu ni moja ukishawachagua watu kwa misingi ya
kiurafiki unajenga wazungu wanaita personal feeling na ktk kazi yeyote hii ni lethal kwa maana inakufanya unashindwa
kufanya maamuzi maziti kwa sababu ya kufanya vitu kwa udugu badala ya umma. natofautiana nawe kwani naamni
kuwafukuza wezi na mafisadi ingekuwa plus kwa chama chake na si negative.

4. hakuna nchi duniani inayoendelea eti kwa kuomba misaada na hasa misaada ya kujikimu mfano mzuri aliotupa JK kwy
kampeni baada ya kubanwa sana kuhusu safari zake za nje alitaja neti za mbu kwahiyo unaweza kuona kuwa siyo
technology anayoifuata huko. cha msingi ni yeye atumie muda wake mwingi hapa ndani kwa kuwatumia wataalamu
wetu na kama tunaitaji tech. basi tuna import watu wanakuja kutufundisha wazalendo hiyo new tech. and then tunawa
timua kwenda kwao.

masomo mema kaka

Je unadhani Tanzania nzima ina hizo resources? naamini unatambua kuwa kuna mikoa ina resources na mingine haina na hata hiyo yenye resources ni sehemu kidogo tu ya mikoa hiyo yenye resources. na vp kuwa na resources tusizojua kuzivuna wala kuzitumia? unadhani zitaweza kutusaidia?
Je katiba yetu inasema nini kuhusu uteuzi wa wasaidizi wakuu wa raisi? naamini zile sio nafasi zinazotangazwa na watu kutuma maombi, zile na non competition positions, unaipata kutokana na ukaribu wako naanayeteua na si competition positions ambazo zinapatikana kutokana na skills,knowledge and experience, hata USA presidents and British PMs mara nyingi wanateua watu wao wa karibu wanaodhani wataweza kufanya nao kazi.
 
Foolishness thread.
Rudi matumbi
historia hubaki historia enzi yote so hongera kwa historia yako. Swali
'amefanya nn kwa mtanzania huyu mtu' ndani ya miaka 7. Naomba jibu.
 
Kuna lawama nyingine hatustahili kuzitoa, kuhusu madini nshaelezea. Kuhusu kilimo, je wewe una shamba? Kama jibu ni ndiyo shamba lako lina ukubwa gan? Umeajiri watu wangapi kwa mwaka unapata faida gani kutoka kwenye hilo shamba? Unatumiaje maji yanayokuzunguka katika kilimo? Na umewaelimisha wangapi juu ya kilimo bora na cha kisasa?
Kama hauna shamba ni kwa nini hauna shamba wakati aridhi ya kutosha ipo?
Nilikuwa najiuliza iweje kanumba kaishia elimu ya sekondari tu na akawa na mali zote hizo alizokuwa nazo,nimekuta kumbe muda mwingine usomi sio kuelimika,ndio maana wako wasomi wengi wakubwa wamepanga nyumba tena chumba kimoja kwa mtu ambaye hata shule hajaenda,YAANI KWA UNAVYOONEKANA HATA UKISOMA MPAKA UWE PROFESA BADO UTAKUWA SHALOW TU YAANI HATA UKIFUNGIWA MAKITABA MIAKA 30 ALAFU UKITOLEWA BADO UTAKUWA HUJAELIMIKA,maana kusoma ni kitu kimoja na kuelimika ni kitu kingine,wewe hujaelimika
 
Foolishness thread.
Rudi matumbi
historia hubaki historia enzi yote so hongera kwa historia yako. Swali
'amefanya nn kwa mtanzania huyu mtu' ndani ya miaka 7. Naomba jibu.

Hata uhuru wa kumuandika humu na kumtukana ni moja ya mambo aliyofanya kama hujui raisi ana uwezo wa kuzuia na asitokee hata mmoja wa kukataa.
 
nashukuru kwa kueleza jinsi katiba yetu ilivo mbovu,sikatai rais asisafiri,anatakiwa asafiri lakini kwa vitu kweli vinamuhitaji rais kama kuhuzuria mikutano ya jumuiya za madola,un na mambo ambayo kweli mkuu wa nchi hizi warsha zinazofanyika ugaibuni za mambo ya nishati,kilimo ,tabia nchi awaachie mawaziri,wakurugenzi na makatibu wa kuu,hata vifursa vya biashara vidogo vidogo ni aibu raisi kwenda marekani eti ili apige picha na 50cent au rihhana,sio vibaya kupiga nao picha lakini mkuu wa nchi hiyo spare time umetoa wapi?

lengo langu ni kutaka kuwafanya watanzania wenzangu kutafuta majibu ya maswali yao na sio kulalamika wakati kila kitu kipo mikononi mwao tena kwa kuzingatia tupo kwenye mchakato wa kuandika katiba mpya.

Wewe kama unajiita msomi wa Political Science, ni bora uende kijijini ukachunge kuku. Kwa kuwa tuna uhuru wa kutoa maoni, basi unahaki ya kufanya hivyo. Nasikitika kuwa kwa makusudi na ama kwa sababu fulani unajifanya kumtazama Kikwete kwa jicho la makengeza. Uchaguzi wa mwaka 2005, Kikwete alipata 81% ya kura zote zilizopigwa. Uchaguzi Mkuu wa mwaka juzi kapata 62% baada ya kudaiwa kuchakachua. Je, kushuka huko kwa kura kunaonyesha nini kama si imani ya wananchi dhidi yake kushuka? Kwa nini? majibu ni mengi, rushwa, ufisadi, kubebana na kutochukua hatua sahihi kwa muda sahihi. Hizo ziara zake nje ya nchi zinaligharimu taifa mabilioni mangapi ukilinganisha na matokeo ya ziara hizo?<br><br>Mikataba mingapi ambayo haina maslahi kwa taifa bali maslahi binafsi ya watu wachache? kuleta hao unaowaita wanateknolojia kubwa na kufunga nao mikataba inayowanufaisha wao binafsi na wale wanaosaini nao mkataba kwa niaba yetu kuna faida gani?<br><br>Kumpa mtu nafasi ya uongozi wakati alikusaidia kufika hapo ulipo badala ya kufuata sifa za mtu kwa nafasi husika kunalipeleka wapi taifa kama si kuliangamiza kabisa? Mtu aliyekusaidia kufikia malengo yako unaweza kuwa na ubavu wa kumkoromea akiteleza? Hajioni kuwa na yeye anaubia katika nafasi uliyo nayo?. Nchi yetu si masikini na wala si changa. Mnaojiita wasomi na mna mawazo ya aina hii, basi taifa hili liko uchi. Nchi inakila aina ya raslimali, utasemaje ni maskini? viongozi tulio nao akiwemo huyo unayemtetea wamejaa ubabaishaji, usanii, ubinafsi, si makini, si wazalendo wala waadirifu. wanawaza mambo yao, nyumba zao ndogo na marafiki zao. Hakuna anayewaza juu ya watanzania wa leo na kesho ndiyo maana mauzauza ni mengi. Unayejaribu kumtetea ameshashindwa, na wewe mtetezi wake ushindwe na ulegee.[/

Je kuna tofauti yeyote ya kiutawala kati ya JK na watangulizi wake unayoiona?
Je kuna tofauti ya kiutawala wa kichama kati ya CCM na vyama vingine? kama unaziona hizo tofauti ni zipi? ukinijibu nitakwambia kitu hapo.
 
Jamani huyu msomi "uchwara" kama anavyojipambanua mwacheni akae na mindset mbovu hadi atakapong'amua! Huwezi ukawa na akili timamu ukapoteza muda kuandika hii mada! It's the problem of having poor vision and lack reasoning! Naungana na waliosema kuwa "elimu unayosoma haitakusaidia kama haya ni mawazo yako, badili fani please".

wek argument
 
This is none sense...wengi wamechangia ila hata kipengele cha kwanza kuhusu Kenya hakina maana, sijui hiyo ni political science ya wapi.. Wakoloni waliwaachia Wakenya majengo tena ni Nairobi to na barabara ni majuzi tu wameweza kuwa sambamba na sisi kwenye miundo mbinu mbali na hapo Nairobi kwenye pot holes za kutosha, huwezi kulinganisha barabara za Tanzania 2005 na barabara za Kenya...na hayo majengo wakoloni waliacha yana nini cha maana? viwanda vingi Kenya ni vipya sema tu imekuwa ni base ya wakoloni walipokuwa EA na kingine ni J. Kenyatta International airport ambayo hiyo pia ni mali ilikuwa robbed kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki. Wakoloni walichukua madini yetu? Kenya wana madini kama sisi..hizi zote ni facts Tanzania na JK ameshindwa kabisa tena mara 50 Mkapa amefanya kazi kwa mfano reforms za TRA, barabara zote mnazosikia zimeunganisha nchi ni Mkapa alianza na uchumi ulikuwa umekaa sawa mbali na ufisadi unaosemwa kafanya Mkapa. JK is total failure na unaposema maamuzi ya Chama vs Serikali, eti Waziri wako anafanya upuuzi unaogopa chama kitavunjika?? kina Kibaki waliacha vyama na kujiunga kwingine, maslahi ya Taifa kwanza then Chama hiyo ndiyo formula... utendaji pembeni na siasa pembeni, ndiyo maana na hoja kuwa Waziri si lazima awe mwanasiasa, tunataka watu intelligent siyo wanasiasa wanakuwa mawaziri hao si watendaji.

Nadhani historia ya Kenya enzi za ukoloni hauifahamu vizuri na after ukoloni unafahamu kuwa waliiba mali za EAC, pia inaonesha ufahamu uhusiano wa chama na serikali, kwa kukusaidia kufahamu huo uhusiano hebu iangalie serikali ya TZ na CCM pia jenga picha kama CHADEMA , CUF au NCCR wangeshika dola serikali zao zingekuwa na uhusiano gani na vyama vyao?
 
Ukikua utaacha. Kwa utoto wako najua utasema na hii ni weak argument.
 
Kumbe na wewe unayafahamu so what to do?
Nadhani tungerudi kulekule kwanza kwenye Azimio la Arusha na kufuata siasa yetu ya UJAMAA NA KUJITEGEMEA then tunaweza kufanya hizo special agreemants tukapata Technology kutokt mataifa Mengine kama China na Russia sio lazima yale ya Magharibi kwani mbona Wachina na Warusi wanayapa mataifa mengine teknolojia hadi ya Nuke? Siasa ya kimagharibi inaishia kwenye uwekezaji ambao in Turn hauna tija yoyote kwetu. Kwani tusipochimba madini tukatafuta hiyo Technology kwanza hatutaipata? Leo hao waochimba wanatupatia 3% kwa mali yetu ni ujinga gani huo au ni tamaa? All in all bila technology hakuna development sidhani kama hata historia inaonesha development ambayo imetokana na uwekezaji nadhani ni Industrial which purely is technology in base.

Binafsi naamini kuwa kwa sasa lile Azimio la Arusha haliwezi kufanya kazi kwa sasa kwa sababu ujamaa kwa Tanzania ya sasa ni kitu kigumu sana, mi nadhani kama wataalamu wetu wakikaa na kutoka na kitu kinachofanana na Azimio la Arusha lakini liwe Azimio linaloendana na maisha yetu ya sasa.
 
Wewe taja kimoja cha maendeleo ambacho Rais aliye kabla ya Kikwete amekifanya na Kikwete hajakifanya zaidi. Utatafuta sana hutopata jibu, utabaki na chuki binafsi na za kidini tu kama Mtei.

Mkapa enzi yake uchumi uliimarika sana lakini toka huyu bwana kaingia ni kuponda mali kufa kwaja ; uchumi umezorota kwasababu ya kuwalinda wezi wa maliasili yetu, wanaiba mpaka Twiga jamaa anawalinda!!
 
Back
Top Bottom