Leo anaitwa dikteta, je kesho ataitwa nini?

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,216
113,519
Hii ni mahsusi kwa wale wadau wa kubadili gia angani.

Hebu leo tulonge kinadharia tete [ingawa baadaye yaweza kutokea na kuwa uhalisia].

Hivi ikitokea Magufuli anaamua kujiuzulu urais kwa sababu za kuhujimiwa na wana CCM wenzake ndani ya chama chake halafu akatangaza kujiunga na UKAWA kupitia moja ya vyama viundao huo umoja, ghafla naye hatakuwa dikteta na dikteta uchwara kama alivyokuwa yule jamaa mwingine ambaye dunia nzima ilitangaziwa kuwa yeye ni bonge la fisadi?

Je, atapokewa kwa nderemo, hoi hoi, vigeregere na vifijo?

Nauliza tu maana siasa na unafiki ni kama kuku na yai.

Halafu, vipi UKUTA? Bado upo hiyo tarehe 1 Oktoba? [Hapo nilikuwa nachomekea tu]
 
Jibu rahisi, akija kwa malaika atabadilika na kuwa kama malaika walio wengi kwa nini asipokelewe.
Ukweli ni mtendaji mzuri ila anahitaji moderation. He performed quite well with Ujenzi anyway!
 
Magufuli sio mbaya ila anakunja sana yeye ndo yeye upande wa pili wapo hapo mengine yanaenda safi.
 
Mi niko poa kabisa.

Naona thread zako za siku mbili tatu zimekuwa ki pro-Magufuli, wakati mwanzoni ulikuwa very skeptical. Umeanza kumkubali Mheshimiwa Rais? Inawezekana spidi yake imekukosha

Hapana, mimi wala si pro-Magufuli wala anti-UKAWA.

Mimi ni pro-consistency na anti-flip flopping [hypocrisy].

Pia ni pro-common sense.
 
Kuna tofauti kati ya Siasa na Injiri;
Magu akija UKAWA kwa kadiri atakavyokidhi matakwa ya Muda tutampokea tu na tutamkubali...
Ilimradi kufanikisha lengo kuu kumtoa nyang'au madarakani....

Kitu kingine "Kwenye siasa kuna maslahi ya kudumu pekee"

Madhara ya UKUTA yalishatimilizwa na yanazidi kutimilizwa kila siku tu ni Mbinu za kukabiliana na "Utawala''
 
Hii ni mahsusi kwa wale wadau wa kubadili gia angani.

Hebu leo tulonge kinadharia tete [ingawa baadaye yaweza kutokea na kuwa uhalisia].

Hivi ikitokea Magufuli anaamua kujiuzulu urais kwa sababu za kuhujimiwa na wana CCM wenzake ndani ya chama chake halafu akatangaza kujiunga na UKAWA kupitia moja ya vyama viundao huo umoja, ghafla naye hatakuwa dikteta na dikteta uchwara kama alivyokuwa yule jamaa mwingine ambaye dunia nzima ilitangaziwa kuwa yeye ni bonge la fisadi?

Je, atapokewa kwa nderemo, hoi hoi, vigeregere na vifijo?

Nauliza tu maana siasa na unafiki ni kama kuku na yai.

Halafu, vipi UKUTA? Bado upo hiyo tarehe 1 Oktoba? [Hapo nilikuwa nachomekea tu]
Watanzania kwa navyowajua watamwita Obama wa Bongo, Mandela wa Tanzania , Nyerere Junior , Rais kipenzi cha watu jama tumpe muda Rais Magufuli mbona mdogo mdogo tutafika mtaka vyote kwa pamoja hawezi pata yote tatizo letu tunataka tuanze kukimbia wakati alitukuta ndo kwanza tunambaa subira yavuta kheri.
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Mkuu heshima mbele.

Mimi nasikitika sana baada ya upepo kutubadilikia tulipokubali mapokezi ya yule jamaa tuliyemtangaza kama symbol ya ufisadi. Siku hizi tumekuwa hatuleti hoja fikirishi kabisa na wala hatuhoji mambo kwa nguvu za hoja, ni kama tumepigwa ganzi. Mwanzoni nilikuwa naona kama mchezo vile, lakini sasa naona kumbe ndio hali halisi. Tumeshaitwa majina mengi so far, lakini kwakweli hili jina la Nyumbu linakera sana. Basi tena, tumeshakuwa wa hivyo. Tulishakosea kuzichanga karata zetu na sasa tunahesabu gharama.
 
Nyani Ngabu vipi mkuu?? Naona thread zako za siku mbili tatu zimekuwa ki pro-Magufuli, wakati mwanzoni ulikuwa very skeptical. Umeanza kumkubali Mheshimiwa Rais? Inawezekana spidi yake imekukosha
Mkuu Dr. Wansegamila na watanzania wengi wa aina yako. Sijaona sehemu yoyote ambayo mwanzisha thread ameonyesha u-pro-Magufuli ila swali alilouliza ni swali zuri sana kw mtu uliye neutral na usiyefungamana na siasa za vyama.
 
Hii ni mahsusi kwa wale wadau wa kubadili gia angani.

Hebu leo tulonge kinadharia tete [ingawa baadaye yaweza kutokea na kuwa uhalisia].

Hivi ikitokea Magufuli anaamua kujiuzulu urais kwa sababu za kuhujimiwa na wana CCM wenzake ndani ya chama chake halafu akatangaza kujiunga na UKAWA kupitia moja ya vyama viundao huo umoja, ghafla naye hatakuwa dikteta na dikteta uchwara kama alivyokuwa yule jamaa mwingine ambaye dunia nzima ilitangaziwa kuwa yeye ni bonge la fisadi?

Je, atapokewa kwa nderemo, hoi hoi, vigeregere na vifijo?

Nauliza tu maana siasa na unafiki ni kama kuku na yai.

Halafu, vipi UKUTA? Bado upo hiyo tarehe 1 Oktoba? [Hapo nilikuwa nachomekea tu]
Akihama chama akiwa Rais ujue na Mars na Jupiter zitagongana na utakuwa mwisho wa dunia. Imagine toka Mars una gap ngapi na inachukua miaka mingapi ya mionzi ya jua? That what it will take.
 
Mkuu wakati wa uchaguzi mabango yalikuwa CHAGUA MAGUFULI suala la vyama halikuwepo.

Hakuna shule ya udikteta ni tabia ya mtu na atabaki nayo hadi kiama.

Hawezi kujiunga na UKAWA baada ya kujidhihirisha hafanyi kazi kwenye mazingira ya utaratibu.

Hatapokelewa atapopolewa
 
Jibu rahisi, akija kwa malaika atabadilika na kuwa kama malaika walio wengi kwa nini asipokelewe.
Ukweli ni mtendaji mzuri ila anahitaji moderation. He performed quite well with Ujenzi anyway!
Tema mate chini alifanya hivyo kidikteta sasa niambie impact ya utendaji wake kitaifa
 
Nyani Ngabu kama we ni pro-common sense unatakiwa kufahamu kuwa siasa ni game of chance, suala la kumpokea fulani lilikuwa ni sahihi sababu fund ya kampeni haikuwepo,pia ukinyamaza watu wanakusahau,so wakati mwingine inabd uongee hata kama huna mantiki ili mradi unajua tu kujenga hoja.
 
Back
Top Bottom