Lembeli aunga mkono migomo/maandamano.

samirnasri

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,388
213
Mbunge wa kahama james lembeli ameunga mkono migomo na maandamano vinavyoendelea hapa nchini kwa kudai kuwa tanzania sio kisiwa kwa kuwa migomo na maandamano vinatokea pote duniani. Lembeli pia amesema migomo ilikuwepo tangu enzi za mwalimu na kuna watu ambao walichapwa viboko ambao leo hii ni wabunge. Pia kasema inasikitisha wanafunzi wanapanga foleni kwenye benk masaa matatu halafu wakiingia ndani wanaambiwa pesa hazijaingia, katika hali kama hii ni vigumu kwa wanafunzi kukaa kimya hata angekuwa yeye angelalamika. Ameitaka serikali itoe mikopo kwa wakati ili kuepusha migomo. Lembeli pia amewataka wabunge kuacha kujadili mambo ya migomo na maandamano bungeni badala yake waielekeze nini cha kufanya kuliko kunyoosheana vidole. Source: bungeni dodoma.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom