Lema to Nassari: "Nitakupa mil. 10.... Jipe moyo utashinda"

Thread uchwara ndio hizi......karatasi linaweza kugharamia kitu gani katika kampeni? unaweza kwenda kwenye mgahawa ukapewa chakula na baada ya chakula ukawaonesha likaratasi kwamba haya ndiyo malipo?

ndo nn umeandika ?
 
x+x=2x uliwahi kuitumia ofsi gani hapa chini ya jua?mahesabu yote yapo kwenye alama za tarakimu kamili,hakuna alphabet.hivyo karatasi na maneno aliyopewa kamanda Nassari yalisimama kama xy.
 
na wewe ushawahi kusikia msemo "Justice delayed is justice denied"?

Mtu mkweli hawezi kuahidi mwenzie fedha halafu anakuja kumpa kikaratasi cha pep talk. Alidanganya, Nassari akakosa plan ya fund raising maana alitegemea kuwezeshwa na Lema, matokeo yake akashindwa kufikisha ujumbe wa kampeni , akashindwa, kikaratasi hakikusaidia.

Je hata angepewa hizo 10m zingetosha kufanya kampeni?mesage ilikuwa wazi,watumainie watu wako wanao kuamini uyashinda,Dogo alikwenda na umma ukampa imani iliyomfanya kuaminiwa na chama,leo kwa thumni zao huyooo Mjengoni.well done Lema,Dogo hata kura za maoni asingeshiriki kwa kufikiri bila fedha haiwezekani.
 
Ulevi huu ndio nisiokubaliana nao......
Mbona wewe ujaachana na mimi? kwa nini unahubiri usichokisimamia? ukiniita Jitu kwangu ni sifa kubwa....tafuta kitabu kinaitwa ALIITWA JITU ndio utanielewa.

Duh! No Fear, umenikumbusha mwaka 1986 nilipokisoma kitabu hicho Aliitwa Jitu pamoja na kile cha Wahuni waliobadilika

Nikirudi kwenye mada, ni kweli Godbless anaweza kuonekana alimdanganya Joshua. Vyovyote vile ilivyokuwa, kwamba alidanganya au alifanya makusudi; jambo hilo la kukosa pesa (ambalo lilikuwa ni tumaini la Joshua) lilimfanya aanze kuutumia uwezo ulio ndani yake katika level nyingine. Kama kiongozi alipaswa kupitishwa katika darasa la kutokutegemea mtu bali watu pamoja na uwezo alionao ndani yake.

Ni kweli kuwa unapopitishwa katika darasa kama hilo in due time linamachungu na kuumiza kama si kuvunja moyo. Lakini kama kiongozi, tabia ya kulalamika inaondoka unaanza kuitazama kama changamoto ambayo lazima uipatie jibu.

Nafurahi, kwasasa, kwasababu Joshua alishindwa. Kujifunza kwa kushindwa ktk uchaguzi ambapo ulikuwa na matumaini ya kushinda kunazidi kuifunua tabia kiongozi ndani ya mtu. Angekuwa mwingine angevunjika moyo na kushindwa kabisa kusimama katika zamu ya pili.

Alishindwa, akasimama tena kuingia katika mapambano mtaji wake mkubwa ukiwa ni watu wa jamii yake. Ndiyo, watu hao ndiyo:
- waliopanga naye mikakati ya kampeni
-waliomsikiliza alipohutubia
- waliomtia moyo kila alipotaka kukata tamaa
- waliotia moyo wakati wote wa kampeni
- waliokwenda kumpigia kura
- walihakikisha wanalinda kura
- waliosema pamoja naye "TUMEANZA NA MUNGU, NA TUMEMALIZA NA MUNGU" baada ya ushindi.
 
Sugu+na+mistari.JPG
Hivi huyu ni nani anayehutubia Wakuu? Simpati vizuri
 
Thank you Gaijin, what an exquisite mind u have, huna ushabiki wa kuangalia mambo kinazi-nazi, na kichama chama, unasema mambo kama yalivyo. Ni kweli kabisa hawa wanapenda chongo wanaita kengeza, pengo wanaita mwanya, wanakubali kuwa clouded with partisan sensationalism.

hapana, delayed justice haiwezi kuwa justice. Kama mtu alistahili kushinda toka zamani akashindishwa hapo hakuna justice, period. Haijalishi amekuja kushinda lini.

Lema alimdanganya Nassari kwamba atampa milioni kumi akishinda tiketi ya CHADEMA, Nassari akashinda akenda kwa Lema kuchukua hela za kumsaidia kufanya kampeni, akapewa kikaratasi cha pep talk. Huyo mtu tayari ni muongo, sasa bila ushabiki wala unazi tuseme ukweli, Lema alimwongopoea Nassari.

Kumbe wengi tunapigwa chenga na tafsida/tamathali za semi, hivi mtu nikikuambia njoo nikung'ate sikio halafu nikakunong'oneza jambo, utasema nimedanganya, ilinipasa nikung'ate kabisa kabisa utokwe na damu? au kwa kuwa kuna kitu msimbazi kimetajwa.
 
Kumbe wengi tunapigwa chenga na tafsida/tamathali za semi, hivi mtu nikikuambia njoo nikung'ate sikio halafu nikakunong'oneza jambo, utasema nimedanganya, ilinipasa nikung'ate kabisa kabisa utokwe na damu? au kwa kuwa kuna kitu msimbazi kimetajwa.

u made my day!

wanafalsafa wanasema "thinking about thinking itself"
 
Thread uchwara ndio hizi......karatasi linaweza kugharamia kitu gani katika kampeni? unaweza kwenda kwenye mgahawa ukapewa chakula na baada ya chakula ukawaonesha likaratasi kwamba haya ndiyo malipo?

Nyie magamba mmezoea kutumia hela mkidhani ndio zitawaletea ushindi! Kuna mbunge huko Mbozi alikuwa na 17,000 tu, akatoka Dar akaenda kugombea na sasa ni MP!? We endelea kushangaa tu wakati wenzio tunasonga mbele!
 
Niliwahi kuongea na Mbunge mmoja wa
Magamba, nikamwambia nataka kugombea ubunge 2015.Binafsi nilitarajia angeweza kunipa mbinu za kisiasa ili niweze kusonga front, cha ajabu aliniambia ''kijana'' tafuta hela,uwe na hela za kutosha.Akanitajia Matajiri kadhaa eti nijitahidi wawe upande wangu, nitashinda. Teeeeh...teeeeh kazi tunayo.

Magamba sisi ni wafuasi wenu lakini kama pesa imekuwa kigezo cha kupata uongozi basi kuna kibarua 2015.
 
Thread uchwara ndio hizi......karatasi linaweza kugharamia kitu gani katika kampeni? unaweza kwenda kwenye mgahawa ukapewa chakula na baada ya chakula ukawaonesha likaratasi kwamba haya ndiyo malipo?

tumaini, jipe moyo na utashinda,

Hiyo ya njano ndiyo mil 10
 
19 Reactions
Reply
Back
Top Bottom