Lema: Rais akiendelea kufikiri yeye ni Mungu basi Mungu atasitisha maisha yake kabla ya 2020

Status
Not open for further replies.

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Habari wanaJF,

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema akihutubia wakazi wa kata ya Sombetini alikuwa akifafanua juu ya kilichotokea baada ya mzozo wake na Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo na hatua ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kumpongeza Mkuu huyo wa Mkoa.

Aidha Mbunge huyo katika Video niliyoambatanisha hapa amesema kuwa "Kitu kimoja ambacho rais anafikiri yeye ni Mungu na kwasababu amefikiri yeye ni Mungu, basi Mungu atasitisha maisha yake kabla ya Uchaguzi wa 2020".

Lakini Mwanzo whotuba yake alianza kwa kuimba wimbo wa "Majanga" wa msanii Snura Mushi kuelezea ugomvi wake na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Mashaka Gambo

 
Lema ameingia kwenye 18 za kitengo na nila shaka hawato mjibu ila watamuacha aropoke ili wamalize vizuri. Huwez kuongea maneno kama haya uachiwe lazima alipia garama
Halafu MUNGU atalipia pia gharama za atakachofanywa lema na hao watu wenu
1bf9f0332634660920b56a2beed93654.jpg
 
Polisi mburuzeni mahakamani amlete huyo Mungu anayesema atamwuua Magufuli kama shahidi yake.Nakumbuka kesi moja mtu alisema alikosea sababu shetani ndiye aliyemsababishia hilo tatizo.Hakimu akasema kesi naipanga wiki ijayo ukamlete huyo shetani hapa mahakamani atoe ushahidi kuthibitisha hayo uliyosema.Mahakama huwa hazina dini kwa hiyo hazitambui Mungu KAMA KIUMBE kisichoonekana.

Huyo MUNGU aliyemsema Lema atamwua Magufuli anatakiwa Lema AMPELEKE mahakamani.
Jamhuri imkamate Lema imuweke ndani hadi atakapomleta huyo Mungu ambaye Lema ana uhakika atamwua Magufuli kabla ya uchaguzi.Kisheria inakubalika .Kamateni LEMA.Na kama hatamleta huyo MUNGU MAHAKAMANI AHESABIWE KUWA yeye ndiye muuaji mwenyewe.Na hao walioshangilia kusema na iwe hivyo wote kamata .
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom