Lema 'pasua kichwa' CHADEMA

Nimekaa na kusoma kwa umakini nikijua ni habari, kuja kuangalia mwishoni kumbe imetoka uhuru?
kwa hao kila kukicha ni udaku tuu, wajiunge na magazeti kama ijumaa na mengine ya udaku...
 
Lema tumemchagua wenyewe sababu ni mpambanaji. Wote mnao mlalamikia ina onyesha amewashika pabaya na sio mkazi wa Arusha
 
Lema anaboa men!!
Kwa lipi?
Usiwe mrahisi wa kufikiri na kuona makengeza!!!

Kama Lema....mtu mmoja anaweza kuzuia mazishi ya watu watano Tarime (haijalishi ni kwa sababu gani)...yani ameweza kuwakalia kooni serikali ya wilaya na mkoa maalumu wa Kipolisi mpaka wakashindwa kuzika. Basi mimi mtu huyo lazima nimuheshimu! atakuwa wa kipekee sana!

Sipendi ordinary people doing ordinary things!!
 
Mwenye kuandika hiyo si chadema ni ccm kajifanya chadema hata msemeje Lema ni shujaa piga ua.
 
Namjua vizuri Lema ni pumba sana, upeo wake wa ufahamu ni mdogo sana, ni mtu wa Controversy kila wakati sijui huyo ubunge kaupataje

Hapo kwenye red ni matusi kwa Lema personally, lakini hapo kwenye bold nyeusi unawatukana wana_A-town.

Kama unataka kujua ameupataje, Mwambie Mwenyekiti wa Chama Chako aende A-town akafanye mkutano then aseme hayo ulosema uone itakuwaje.........Nakushauri Kikwete ndo aende, coz akienda mtu kama NEPI, hata huo mkutano hataufanya kabisa!!
 
Najua watu wasiotaka kuambiwa ukweli watakataa lakini huu ndio ukweli wenyewe. Wote wanaweza kuhamasisha maandamano ila wanachozidiana kwa hili ni jee hayo maandamano yana tija yoyote au ni kujitafutia umaarufu?
Nilitaka nisijibu ila hasira imenipanda kuona huu upotoshaji wa magamba.They are really going to hell! Kama hii ndo kazi waliyompa Nepi basi amekuja kukimalizia kabisa badala ya kukisaidia. Kama Nepi anataka japo afike 2012 aachane kabisa na cdm apambane na madui wa ndani ya magamba otherwise anakipeleka chama makaburini si muda mrefu.Hizi propaganda za kitoto za kizamani,za akina kingunge labda wasiojua mtawadanganya! Hatudanganyiki period. Habari hii imetungwa na magamba wamekaa studio wakahojiana wenyewe kwa wenyewe nendeni huko na uchuro wenu! Mtawapata wajinga welevu mtaambulia matusi kama hapa.Hakuna mbunge mwanamapinduzi atakaye mpinga Lema labda ni magamba. Mbona hamjasema Mdee na Mnyika mbona walisisitiza maandamano yataendelea na huo ndo msimamo wa cdm na wala siyo wa wabunge! Jamani jaribuni kuvinunua vyombo vya habari ambavyo ni credible kidogo ili uongo wenu uaminike japo kwa siku moja. Yaani unatumia UHURU kuponda CDM hata mtoto wa chekechea atakucheka.Watakucheka watu!!!!!!!!!
 
Lema 'pasua kichwa' CHADEMA[/h] * Kauli zake zadaiwa kuudhi wenzake
* Mbunge adai zinakidhalilisha chama
* Ashangaa baadhi kumwona kama shujaa
* Ataka chama kimuwajibishe, vinginevyo...

NA STEPHEN BALIGEYA, DODOMA

KAULI za majigambo zinazotolewa na mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema (CHADEMA), kwamba ataendelea kuhamasisha maandamano usiku na mchana, zimemweka kitanzani. Hatua hiyo inatokana na baadhi ya wabunge wa CHADEMA, kudai kuwa kauli na matendo ya Lema yamekuwa yakikidhalilisha chama hicho mbele ya umma.

Akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, mbunge mmoja wa CHADEMA, amesema kuwa anakusudia kuwasilisha malalamiko ndani ya chama hicho juu ya kauli hizo. Hata hivyo, amesema anatarajia kupata wakati mgumu wakati wa kuwasilisha hoja, hivyo kutokana na viongozi wa juu kukaa kimya bila kumchukulia Lema hatua za kumrekebisha. “Ni mtu anayeshangaza sana, taswira yetu mbele ya jamii imechafuka, lakini jambo la kusikitisha viongozi wa juu wako kimya na wengine wanamchukulia kama shujaa,” alisema mbunge huyo.

Ameongeza kuwa ni ngumu kwa viongozi na wabunge wa CHADEMA kujivua lawama za kuwa chama kisichojali maendeleo ya Watanzania na badala yake kuhamasisha fujo. "Kweli unaamua kuropoka mbele ya umma kwamba tutaandamana usiku na mchana, mpaka kieleweke, hivi tujiulize anataka kieleweke kitu gani wakati uchaguzi umekamilika?" alihoji.

Pia, ameeleza kushangazwa kwake na baadhi ya wabunge wenzake wa chama hicho kujigamba mbele ya Bunge kuwa vyama vingine navyo viitishe maandamano kama vitapata watu. "Huu ni upofu wa kisiasa, hivi unaweza kusema CCM wakiamua kufanya maandamano hawapati watu, na je, unataka kusema CUF wakiandamana hawapati watu? Waache kujidanganya," aliongeza.

Alisema iwapo vyama vingine vitakuwa na sera ya maandamano kama Chadema inavyotaka iwe, hakuna shaka nchi itakosa mwenyewe, kwani lazima kila mwananchi ana mapenzi na chama fulani, hivyo kusema hawatapata watu ni hadaa tupu.

"Hivi kama sisi tuna watu wengi kiasi hicho, tulishindwa nini kupata viti 50 ikilinganishwa na vile ilivyopata CCM? Pamoja na udhaifu tunaozungumzia, lakini ukweli unabaki kuwa CCM ndiyo chama chenye watu wengi na siku kikiamua kujibu mapigo patakuwa hapatoshi.

"Unajua siku ile tunajadili Muswada wa Katiba hapa Dodoma, aliamua kwenda kuhamasisha wanafunzi wa UDOM na kuwapa sh. 5,000 kila aliyekubali kuungana na fujo zake," aliongeza mbunge huyo.

Alisema pamoja na Mkuu wa Mkoa Dodoma, Dk. James Msekela, kueleza wanafunzi kuwa anajua mgomo na fujo zao yupo mwanasiasa (mbunge) nyuma, Lema alijitokeza papo hapo na kusema yeye ndiye aliyewafuata.

Kwa maelezo hayo, mbunge huyo anasema imefikia hatua watu wenye akili timamu wanaona kwamba, CHADEMA kinaongozwa na watu wasio na uchungu na Watanzania kutokana na matendo yanayoendelea.

“Tumekuwa tukiwasema viongozi wa CCM ambao kila kukicha wanakemeana, lakini kwetu hata kumuonya Lema juu ya kauli zake tumeshindwa na badala yake heshima ya chama inazidi kushuka,” alisema.

Juzi jioni akichangia kwenye bajeti ya serikali kwa mwaka 2011/12, Lema alisema CHADEMA kitaendelea kuandamana usiku na mchana ili mradi taa ziwekwe barabarani.

"Tena nataka niwaambie kuwa mimi ndiye niliyezuia maiti Tarime wasizikwe na mwenzangu Tundu Lissu akaja kupigilia msumari wa mwisho," alijigamba Lema.

Mbunge wa Mwibara, Alphaxard Lugola, alisema mbunge huyo amezoea kuzuia maiti wasizikwe, hivyo kuna siku atazuia hata maiti za watu wengine ambazo hazijatokana na vurugu kama za Tarime.

"Lema, kuna siku ukimaliza kugombea maiti wa Nyamongo, utagombea maiti wanaotokana na vifo vya kawaida, kwani itakuwa mazoea hivyo kuwa vigumu kuacha," alisema Lugola.

Source: UHURU

Kumbe ni Lema , huyu mtoto sio rizki mbona A town wanamjua sana
 
anaeuliza lema aliupataje ubunge arusha mjini namuomba akamuulize lowasa na hawala yake batrilda burian atakupajibu sahihi..maana kama ni pesa ilitumika sana kuanzia kununua sukari, kanga, t-shirt, kofia, kuiba bendera za cdm, kuwa lipa wenye magari ili waweke bendera za ccm, walikondisha gari la matangazo kubwa balaa kwa siku zaidi ya 71, polisi walitumiaka kuzoofisha upinzani hasa cdm lakini mwisho wa siku mama wa watu chali pamoja na kwamba tuliiomba nec imwongez kura 5000..
 
Lema 'pasua kichwa' CHADEMA[/h] * Kauli zake zadaiwa kuudhi wenzake* Mbunge adai zinakidhalilisha chama* Ashangaa baadhi kumwona kama shujaa* Ataka chama kimuwajibishe, vinginevyo... NA STEPHEN BALIGEYA, DODOMA KAULI za majigambo zinazotolewa na mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema (CHADEMA), kwamba ataendelea kuhamasisha maandamano usiku na mchana, zimemweka kitanzani. Hatua hiyo inatokana na baadhi ya wabunge wa CHADEMA, kudai kuwa kauli na matendo ya Lema yamekuwa yakikidhalilisha chama hicho mbele ya umma. Akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, mbunge mmoja wa CHADEMA, amesema kuwa anakusudia kuwasilisha malalamiko ndani ya chama hicho juu ya kauli hizo. Hata hivyo, amesema anatarajia kupata wakati mgumu wakati wa kuwasilisha hoja, hivyo kutokana na viongozi wa juu kukaa kimya bila kumchukulia Lema hatua za kumrekebisha. "Ni mtu anayeshangaza sana, taswira yetu mbele ya jamii imechafuka, lakini jambo la kusikitisha viongozi wa juu wako kimya na wengine wanamchukulia kama shujaa," alisema mbunge huyo. Ameongeza kuwa ni ngumu kwa viongozi na wabunge wa CHADEMA kujivua lawama za kuwa chama kisichojali maendeleo ya Watanzania na badala yake kuhamasisha fujo. "Kweli unaamua kuropoka mbele ya umma kwamba tutaandamana usiku na mchana, mpaka kieleweke, hivi tujiulize anataka kieleweke kitu gani wakati uchaguzi umekamilika?" alihoji. Pia, ameeleza kushangazwa kwake na baadhi ya wabunge wenzake wa chama hicho kujigamba mbele ya Bunge kuwa vyama vingine navyo viitishe maandamano kama vitapata watu. "Huu ni upofu wa kisiasa, hivi unaweza kusema CCM wakiamua kufanya maandamano hawapati watu, na je, unataka kusema CUF wakiandamana hawapati watu? Waache kujidanganya," aliongeza. Alisema iwapo vyama vingine vitakuwa na sera ya maandamano kama Chadema inavyotaka iwe, hakuna shaka nchi itakosa mwenyewe, kwani lazima kila mwananchi ana mapenzi na chama fulani, hivyo kusema hawatapata watu ni hadaa tupu. "Hivi kama sisi tuna watu wengi kiasi hicho, tulishindwa nini kupata viti 50 ikilinganishwa na vile ilivyopata CCM? Pamoja na udhaifu tunaozungumzia, lakini ukweli unabaki kuwa CCM ndiyo chama chenye watu wengi na siku kikiamua kujibu mapigo patakuwa hapatoshi. "Unajua siku ile tunajadili Muswada wa Katiba hapa Dodoma, aliamua kwenda kuhamasisha wanafunzi wa UDOM na kuwapa sh. 5,000 kila aliyekubali kuungana na fujo zake," aliongeza mbunge huyo. Alisema pamoja na Mkuu wa Mkoa Dodoma, Dk. James Msekela, kueleza wanafunzi kuwa anajua mgomo na fujo zao yupo mwanasiasa (mbunge) nyuma, Lema alijitokeza papo hapo na kusema yeye ndiye aliyewafuata. Kwa maelezo hayo, mbunge huyo anasema imefikia hatua watu wenye akili timamu wanaona kwamba, CHADEMA kinaongozwa na watu wasio na uchungu na Watanzania kutokana na matendo yanayoendelea. "Tumekuwa tukiwasema viongozi wa CCM ambao kila kukicha wanakemeana, lakini kwetu hata kumuonya Lema juu ya kauli zake tumeshindwa na badala yake heshima ya chama inazidi kushuka," alisema. Juzi jioni akichangia kwenye bajeti ya serikali kwa mwaka 2011/12, Lema alisema CHADEMA kitaendelea kuandamana usiku na mchana ili mradi taa ziwekwe barabarani. "Tena nataka niwaambie kuwa mimi ndiye niliyezuia maiti Tarime wasizikwe na mwenzangu Tundu Lissu akaja kupigilia msumari wa mwisho," alijigamba Lema. Mbunge wa Mwibara, Alphaxard Lugola, alisema mbunge huyo amezoea kuzuia maiti wasizikwe, hivyo kuna siku atazuia hata maiti za watu wengine ambazo hazijatokana na vurugu kama za Tarime. "Lema, kuna siku ukimaliza kugombea maiti wa Nyamongo, utagombea maiti wanaotokana na vifo vya kawaida, kwani itakuwa mazoea hivyo kuwa vigumu kuacha," alisema Lugola.Source: UHURU
kuna mdau mmoja alisema kuna zengwe linapikwa huko ikulu kuhusu cdm. Sasa wameanzia uhuru
 
kuna mdau mmoja alisema kuna zengwe linapikwa huko ikulu kuhusu cdm. Sasa wameanzia uhuru
Vilaza tu hawa, watafanya zengwe gani kwa sasa maana mambo yote yako hadharini kwa wananchi. Watawadanganya nini watu ili waaminike tena?Wao wakubali yaishe, wamalizie miaka iliyobaki wasepe watu warudishiwe uhuru na haki yao. Na wakizidi kubisha ndo wanaharibu zaidi, itawafanya watu waamue isivyo hata kabla ya 2015. Limeoza karibia robo tatu utafanya nini na hiyo robo peke yake?
 
Najua watu wasiotaka kuambiwa ukweli watakataa lakini huu ndio ukweli wenyewe. Wote wanaweza kuhamasisha maandamano ila wanachozidiana kwa hili ni jee hayo maandamano yana tija yoyote au ni kujitafutia umaarufu?
Nilitakanisijibu ila hasira imenipanda kuona huu upotoshaji wa magamba.They are really going to hell! Kama hii ndo kazi waliyompa Nepi basi amekuja kukimalizia kabisa badala ya kukisaidia. Kama Nepi anataka japo afike 2012 aachane kabisa na cdm apambane na madui wa ndani ya magamba otherwise anakipeleka chama makaburini si muda mrefu.Hizi propaganda za kitoto za kizamani,za akina kingunge labda wasiojua mtawadaanganya! Hatudanganyiki periodHabari hii imetungwa na magamba wamekaa studio wakahojiana wenyewe kwa wenyewe nendeni huko na uchuro wenu. Mtawapata wajinga welevu hamtaambulia matusi kama hapa.Hakuna mbunge mwanamapinduzi atakaye mpinga Lema labda ni magamba. Mbona hamjasema Mdee na Mnyika mbona walisisitiza maandamano yataendelea na huo ndo msimamo wa cdm na wala siyo wa wabunge! Jamani jaribuni kuvvinunua vyombo vya habari ambavyo ni credible kidogo ili uongo wenu uaminike japo kwa siku moja. Yaani unatumia UHURU kuponda CDM hata mtoto wa chekechea atakucheka.Watakucheka watu!!!!!!!!!
 
Km maandamano yana tihja au hayana nakupa assignment......nenda kawaulize ivory coast baada ya hapo nenda tunisia, nenda misri, nenda yemen halafu njoo na jibu sio kuuliza maswali yasiyokuwa ya msingi............
Mkuu, unafananisha maandamano ya Chadema na maandamano ya Misri,Yemen, Tunisia?Maanadamano ya Chadema kina Halima Mdee, Regia Mtema, kabla ya maandano wanaenda salon kutengeneza kucha na kusuka rasta, maandanamano gani viongozi wote wanaandamana wamepanda magari wapambe wao ndio wanatembea kwa miguu, utadhani mnakwenda kwenye Kitchen Party
 
UHURU ni gazeti la unafki $xx***x zao. Hakuna uzalendo hata kidogo zaidi ya matumbo, ni aibu kwa msomi mwandishi wa Taifa hili aliyesomeshwa kwa kodi za waTZ maskini anapomaliza kusoma badala awasaidie waTz, anatumia taaluma waliyomsomeshea kuwadanganya na kuwaibia kama wanavyofanya hawa maXX$**%**$##Xxx wa uhuru. nasema na naungana na Mh Lema kuwa hatutaacha kuandamana mpaka maskini wa Tz atakaposikilizwa,Tutaandamana usiku na mchana mpaka vijana wa Tz watakapopatiwa ajira rasmi na sio hizi za jk za kuokota makopo ya maji ya uhai, sayona, masafi n.k. Mmezoea siasa rojorojo na laini laini nyie magamba, Ngoja tuwape mchaka mchaka wa siasa ngumu kama Igneous rock mpaka mtapike Nyongo, Pancrease, Doudenum na mapafu yenu.nani amewalaani hawa waTz wa uhuru?MUNGU IBARIKI TZ, MUNGU YABARIKI MAANDAMANO YETU YA USIKU NA MCHANA, MUNGU IBARIKI CDM. CDM mwendo mdundo
 
Back
Top Bottom