Lema, nakuomba ubadilishe muelekeo wa siasa za Arusha

nipe hoja alishawahi kutoa ya kulikomboa taifa hili tangu awe mbunge, wewe ujui ulichoandika, wewe nenda kaandame zako huko arusha bwana,

 
nipe hoja alishawahi kutoa ya kulikomboa taifa hili tangu awe mbunge, wewe ujui ulichoandika, wewe nenda kaandame zako huko arusha bwana,

Masikini vijana wa lumumba wakisikia Lema c.hu zina wapwaya...
 
Upo sahihi kamanda,laiti watu wangemjua lema ana dhamira gani,WASINGEMUITA MTU WA FUJO.ANGALIZO-Lema hakuwahi kushindwa kwa analopigania.
 
Anza na kuwaambia ccm kwani umesikia tayari wanavyosambaza sera za ukabila kupitia Lowasa, naibu waziri na mkuu wa mkoa wa Arusha kuwa wachaga warudi kwao na makabila mengine hao ndio ccm. kwenye ukabila wako, kwenye udini ndo usiseme, kwenye ukanda ndio kama kawaida ili mradi tu wanafaidika kisiasa ili hali nchi iteketee wao safi wapate tu madaraka

Muheshimiwa Arusha sasa imekua kama sehemu ambayo hakuna amani ya kimaendeleo kila kukicha
tumekua tunaendelea kusikia mbunge wetu amefanya hivi anafanya vile sasa sijui kama kuna tija ya
kimaendeleo katika masuala tunayoyafanya ,

Katiba ndio hasa itakayotusaidia kufanya mambo haya mengine ya haki ikaeje na kwamba ni nini cha kufanya
jitahidi kupigana kuwe na uwekezaji Arusha ili wananchi tuliokuchagua tuwe na maisha bora ambapo CCM
wameshindwa hili tayari.
Onesha kwamba kura tulizokupa hatukupoteza........

tukutane hapo nje yaani NMC......................................................

nawsilisha.
 
Wapenda amani tuiombee Arusha kwa ombwe hili la uwakilishi.....tatizo ni "wanainchi" wengi kukaa pembeni kwenye haya mambo ya siasa na kuwaachia "machalii" wafanye maamuzi...matokeo yake wamemchagua mwenzao ndio awe muwakilishi.

Uchaguzi unaofanyika kwenye baa ya mbege...ofcoz kiongozi atatoka miongoni mwa hao wanywa mbege...hawawezi kutoka na kwenda kumtafuta Milard Ayo aende kuwaongoza.

Ndio maana wakati viongozi sehemu nyingine wanahimiza wanainchi wao wajiajiri kwa kuonyesha njia (mifano hai) kama kwa kufuga kuku n.k (Nawanda).....Huku Lema anaishia kutengeneza wanywa viroba na bange na wapenda maandamano.....huku siku zinaenda vijana wapo kule kule vijiweni walipokuwa tangu mwanzo.

Wanaonufaika ni wao mabwana wakubwa wanaonunua majumba kila kona ya dunia na kujikopesha ruzuku.
 
Wewe kweli umeshindwa kuona mantiki aliyotoa mtoa mada ama una lako jambo? Hivi mtu mwenye uchungu na nchi hii lazima arudi aishi Tz, mbona kuna mama waziri wa Uingereza alikuwa na uchungu na Tz hata akawa tayari kupoteza cheo chake kwa kusimamia Tz wanarudishiwa ''chenji ya rada'' Acha zako hizo, Kilombero wanatoka ''great thinkers'' unasema nini wee munthu. Unachezea IFOZA.

Siasa za mitandaoni hazitawasaidia ninyi misukule! CDM daily wapo field nyie mumekazana kulipana buk 7 kwa umbea hapa jf.jitafakarini kama kuna mafanikio toka mzindue lumumba fc!
 
Ni mfanya biashara yupi ambaye ameshindwa kufanya kazi yake kwa sababu ya Lema?

Nakubali wapo waliojiandaa kubebwa na Batilda kwa namna za ki ccm hao ndo wanaolialia
 
Semeni sana juu ya huyu Nguli wa mapambano ya kudai haki nakuta haki ya mtu ieshimiwe kwangu Mungu mzidishie ulinzi Lema
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom